Ofisa wa Shirika la Maendeleo Japan (JICA), Minako Yamamoto (kulia), akijadiliana jambo na Ofisa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Irenius Ruyobya huku akiwa amejifunga kitambaa kuziba mafua aliyonayo asiambukize watu wengine, leo wakati wa mkutano wa kukusanya maoni kwa wadau juu ya sensa inayotarajiwa kufanyika nchini Agosti, mwaka huu. Mkutano huo ulifanyika Dar es Salaam leo
Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Albina Chuwa (katikati) akijadiliana jambo na Kamishna wa Sensa, Amina Said (kushoto) pamoja na Mshauri wa Matokeo ya Takwimu, wa Taasisi ya DFID, Phillip Cockerill wakati wa mkutano huo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. VIPI TENA, MBONA MDAU WA JICA ANAZIBA MDOMO NA PUA!!!!!!!!!!!!!!!!!

    KUNA MAGONJWA YA MLIPUKO (KUAMBUKIZA ) KATIKA HUO UKUMBI AU NI ''MTU NI AFYA''

    KAMA NI HIVYO

    MBONA OFISA WA TAKWIMU BWANA RUYOBYA HAKUVAA????

    MBEBA BOX WA KUDUMU

    ReplyDelete
  2. Wajapani wana utamaduni mzuri sana wa kujali afya za watu wengine.
    Kama huyo dada hapo pichani alivyovaa hiyo maski usoni ili asiambukize wengine mafua aliyo nayo yeye.
    Sisi waafrika tukipata UKIMWI tunataka tufe na wengine kwa kuusambaza.

    ReplyDelete
  3. Inbgekuwa sisi Wakonongo ndio kwanza mtu anapenga kamasi tena bila kujali!

    ReplyDelete
  4. Jamaa kachafua hali ya hewa nini?

    ReplyDelete
  5. Michael Jackson (R.I.P.) alipofanya hivyo acha mumpigie kelele, wakati nyie wenyewe mnaziba pua mkikatiza mitaani.

    ReplyDelete
  6. Ona mtu Mstaarabu anavyomjali mwingine!

    Anakukinga dhidi ya Maambukizi ya Mafua.

    Angekuwa mtu mjinga hata Virusi vya Ukimwi anakumwagia tena bila wasi wasi huku akijua kuwa amesha athirika kitambo tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...