Nimetua Bongo kutokea ughaibuni tarehe 3 Machi. Wiki moja baadaye, "laptop" yangu imeibiwa hapa Dar es Salaam, eneo la Sinza. 

Ilikuwa ni Apple mpya. Nilikuwa nimeipakia maandishi yangu mengi, miswada na ripoti za utafiti wa kuanzia 1993.Ninachohitaji ni haya maandishi. 

Huu ni mchango wa taaluma ambao natoa kwa wa-Tanzania na walimwengu. 
Miswada ya vitabu viwili nilitaka kuchapisha hapa Tanzania wakati huu, kwa manufaa ya wanafunzi, walimu, na jamii. Hii "laptop" ukiifungua inakupa jina la Joseph Mbele, na unahitaji "password" ili kuweza kuitumia. 

Habari ndio hiyo. Hivi sasa najiona kama mkulima mwenye ari ya kulima, lakini jembe hana. Nakala za miswada ziko ofisini Marekani. Lakini mimi nilipania kufanya kazi kubwa kwa wiki hizi nitakapokuwa hapa Tanzania. Nimekwama 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. pole sana. KWELI NG'OMBE WA MASIKINI HAZAI.

    ReplyDelete
  2. Pole sana Mkulima uliyenyang'anywa jembe!
    Lakini kaka hii ndiyo Bongo yetu tulipofikia, hali siyo nzuri kwa kweli.

    Wadau msaidieni apate jembe lake kusudi Taifa lifaidi matunda ya kazi za wananchi wake jamani.

    ReplyDelete
  3. Pole Professa Mbele kwa mkasa huu,

    Jamani huyo atakaeipata hiyo laptop hana uwezo wa kuifungua hadi awe na hiyo password hivyo ni bora afanye mpango wa kuirudisha hata kwa kuiacha sehemu na atoe maagizo ama sivyo itakuwa ni kama 'Mdoli' kwake.

    Teknolojia inawezesha mambo hivyo usanii una ukomo wake hapo.

    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  4. pole sana Prof. mbogo tambarare.

    umesema zingine zipo USA, ungemuomba mtu huko USA,kama computer ina password mpatie, ukifirudi USA, utabadilisha. afungue computer yako , akutumie , usichelewe kufanya kazi.

    ushauri wa mbule kwa watanzania wote. ni vizuri kuhifadhi vitu sehemu tofauti tofauti kama vile kwenye email, laptop, USB, hard copy . pia viweke seheme tofauti tofauti, ilik kimoja kikipotea au kuibiwa, utatumia kingine.


    mbeba box wa kudumu

    ReplyDelete
  5. pole prof,nadhani vijana waliamua kukukaribisha bongo kwa style hiyo.Wakati nikiendelea kukusaidia kuitafuta,naomba ujibu maswali yangu yafuatayo.1.Uliibiwa ukiwa umeiacha ktk gari hivyo hao wezi walivunja kioo cha gari wakaichukua??2.Ulikuwa unatembea mfano,then ukavamiwa na wezi wakaipora??3.AU uliibiwa kama alivyoibiwa Mh.sana ADAM MALIMA huko MOROGORO??Tafadhali yajibu hayo ili nijue mahali pa kuanzia

    ReplyDelete
  6. Prof. Mbele,

    I can imagine situation uliyo nayo kutokana na thamani ya material ulizoibiwa.

    Nakushauri utangaze donge nono kwa aliyeiba na pia utangaze kuwa umeshamsamehe aliyeiba unachohitaji ni material zako zaidi. Nafikiri itasaidia ku-motivate ili akurudishie.

    Unaweza pia kutangaza kwenye forums nyingine kama EthinkTankTz, hii ni forum ya ICT Professionals in TZ and EA.

    Mungu akusaidie


    Nawasilisha

    ReplyDelete
  7. Hiyo ni karibu bongo babaaa...wanajaribu kukumbusha kwamba hii sio Obama land mzee akili kumkichwa hapa.Mtu hajala toka asubuhi we unamuonesha apple unategemea nini? tatizo mkitoka mtoni mnataka watu wajue mmetoka mtoni na hizo laptop zenu mnazifungulia hata maeneo yasiyofaa kama mnalingishia vile,lazima utendwe mzee, kama una nia na kazi zako hapa bongo just ingia internet cafe ,wasiliana na jamaa zako mtoni wakutumie attachments fasta,kesho nenda benki, draw dola kidogo,ingia mtaani usedlaptop kibao kwa bei chee,hilo apple wacha wajanja walile,usijali kuhusu password, hackers na crackers kibao bongo itatumika kama kawa hiyo si ishu mzeee!

    ReplyDelete
  8. professa pole kwa yaliyokufika.

    ila nakupa ushauri kuwa sikuzote unapokuwa safarini usitegemee laptop pekee. kuwa na flash drive kama back up ya documents zako muhimu ili yakikufika kama hayo unaweza kuretrieve docs zako.

    jee kama laptop ingecorrupt unagewezaje kuendelea na kazi zako? hivyo ishu sio wizi tu ila kuna mengi kama kuanguka, kuingia maji au kuharibika kusikoweza kupata tena hizo files zako. ni vyema uwe na back up means.

    pole sana prof....

    ReplyDelete
  9. Pole sana Profesa, sasa hii ndio BONGO. walio iba hawata soma hi makala katika blog na hivisasa weshapelekea "wataalam" wa masuala ya "password" na mambo yote yamefutwa na laptop imeshauzwa ki aina.

    sasa we pumzika kisha rudi USA uka anze upya.... usipate presha na kujiumiza, wala usitegemee msaada wowote kupata hiyo laptop. Bongo yunagawana umaskini ndio socialism.

    ReplyDelete
  10. Pole, Laptop mali kweli bongo haswa za kuchori kama hiyo. natumai una backup - ukija bongo lazima uwe mbilimbili au sivyo utalia.

    ReplyDelete
  11. Dude :( isn't that the reason we have Cloud Storage?????? What the heck!! I am sorry but hey lessons Learned!!

    ReplyDelete
  12. karibu bongo braza mbele...hii ndio bongoland...tusio nacho tunawarukia mlionacho...mlidhani ninyi mkiishi maisha ya neema ss tutawaangalia tu??

    ReplyDelete
  13. Prof I thought they taught you about back up!

    ReplyDelete
  14. pole mkulima, hapo ndio bongo. ila next tym kwa vitu muhimu kama hvyo ni lazima ufanye online back up coz unaweza access them from anywhere na haviwezi potea. pole

    ReplyDelete
  15. Wewe kweli ni Prof au basi tu. Maana kama unavyojidai unaishi ughaibuni basi lazima mambo hayo uwe umejitayarisha nayo. Password ya Windows ni rahisi sana kujulikana. Hata ukiweka katika Bios basi pia ni jambo dogo tu hilo. Kama wadau waliotangulia wewe utakuwa kama wale wazee waliokuwa wakihifadhi pesa kwenye magodoro au wanachimbia kwenye ardhi. Unanikumbusha mbali sana, jaribu kutumia elimu yako vizuri umeshaanza taratibu kuadhirika.

    ReplyDelete
  16. Pole Prof. Mbele kwa balaa hili!

    Kwa kweli wanakurudisha nyuma sana, wanawarudisha nyuma wanafunzi wako na jamii na kukwamisha jitihada zako!

    Sasa hili si litakuwa ni balaa kubwa sana kwa Maktaba ya tokea mwaka 1993 kuibwa?

    ReplyDelete
  17. Watafute vijana wa kijiwe hapo hapo sinza, wape chochote kitu wakupe.

    Kwa sasa hivi, mtu akiwa na access ya kompyuta iliyowekwa password, kuiondoa password ni kitu kidogo sana. Hivyo kuhusu hilo Prof. usijipe moyo sana. Omba na tangaza dau tu wakurudishie....!

    Pole kwa msala....

    ReplyDelete
  18. Kama una series namba ya kompyuta unaweza kuwapa vyombo vya usalama TZ au Marekani. Wataipata tu. Maana kila kompyuta inapowashwa unaweza kuitrace kwa kutumia series namba yake. Angalau Uingereza wezi wa vyombo kama kompyuta na simu hukamatwa hivi. Jaribu kuzungumza na apple, na kama bado unayo risiti itakuwa na namba muhimu za kompyuta hiyo. Hiyo itakufanya uipate tena. Ila bado una kazi kubwa.

    ReplyDelete
  19. Pole professor, external hard drives zenyewe si za kuaminika. Kuna mdau mmoja amesema kuhusu Cloud Storage na mimi namuunga mkono 100%. Good luck labda unaweza kuipata mashine yako iliyoibiwa.
    Mdau Edina, MN

    ReplyDelete
  20. Wewe tupe p/word tukutumie hizo info hii mac watu wanahitaji mtaani kwa ajili ya facebook!!!!

    ReplyDelete
  21. Ukisikia Laana ya Elimu ndio hii!!!

    Mijizi ya Bongo ina laana, mnawaibia hata Maprofesa wa Elimu?

    ReplyDelete
  22. Mdau Anonymous wa Fri Mar 16, 05:34:00 PM 2012

    Ktk jamii zilizopiga hatu Watu kama Waalimu wanaheshimika kujaliwa na kuthaminiwa kama walivyo Viongozi wa Dini.

    Yaani akiacha kitu chake lazima atapelekewa, na kamwe hadanganywi ni vile wanaaminika kuwa wenye (kipawa) au uwezo wa Juu !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...