Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25, Mhandisi wa Maji Wilaya ya Geita, Daud Sweka kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo za kusaidia mradi wa visima vitatu vya maji safi na salama ya kunywa kwa wakazi wa Kijiji cha Mkolani-1 wilayani humo hivi karibuni. Katikati ni Meneja Mauzo wa TBL Geita, Issa Msuya.
Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamakale, Sizya Mulelemi Mashilungu akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 25 Enock Kangasa, mkandarasi anayatekeleza mradi wa visima vya maji safi na salama ya kunywa kwa ajili ya wananchi wa kijiji cha Mkolani-1 Geita Mwanza, muda mfupi baada ya hundi hiyo kutolewa na kampuni ya Bia nchini (TBL). Kulia anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa TBL Editha Mushi.
Baadhi ya wananchi wa Nyamakale Mkolani -1 wakiwa na hundi ya sh. milioni 25 walizopewa na TBL


Hakika nchi imebinafsishwa, yaani madawati ya shule msaada kutoka PLAN kisima cha maji msaada kutoka TBL. Hivi kodi zetu zinafanyiwa nini?
ReplyDeleteTaifa la walalamishi.
ReplyDeleteJiulize wewe umechangia nini. Kwetu
moshi bado tuna moyo wa kujitolea barabara, shule, madawati tunafanya kwa moyo wa harambee, kukaa kungoja serikali ni ulemavu wa kujitakia. Kama madawati yakitolewa bure huwa ni ya wahisani hivyo hayana uchungu kama tungechangia wenyewe. Kodi zitumike kulipa askari,waalimu, miundombinu, nk... Pale manzese uzuri wananchi walimkamata seremala mmoja akiiba madawati na kutengeneza samani(fanicha) akauliza kwani zenu? Hata ukikuta mtu anaiba mfuniko wa mtaro au bomba za kingo za barabara watu watatetea, anatafuta kula !!!!
Oneni aibu kutegemea misaada huku mmevalia ma wax ya kushiba. Kuomba hudhalilisha utu. Acheni hizo wabongo.
ReplyDelete