Picha zinaonyesha hali halisi ilivyojionyesha jana Jumatatu, Machi 26 wakati sayari mblili na Mwezi hilali zilipo jipanga kwa mstari ulionyoka na kutoa mandhari ya kusisimua kipekee.

Katika picha, hilali ya Mwezi imebeba sayari ya Zuhura (Venus) inayowaka kama moto angani. Chini yake kushoto katika mstari, ni sayari ya Sambula (Jupiter) ambayo pia inang'aa.vikali.

Mpangilio huu hutokea kwa nadra sana kwa vile sayari na Mwezi kila moja huzunguka kwa mpangilio wake wa kasi na umbali. Mkusanyiko kama huu na wa karibu zaidi kuliko huu hautatokea tena hadi Juni 20, mwaka 2015.

Ingawa sayari na Mwezi ziko mbali mbali kwa umbali mkubwa sana kati yao. Mwezi upo kilometa kiasi laki nne kutoka kwetu, Zuhura iko kilomita milioni 110, na Sambula iko kilomita milioni 870 kutoka kwetu. Ni kama vile unaziona karibu karibu lakini zimejipanga moja nyuma ya nyingine.

Dr N T Jiwaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Asante sana Dr Jiwaji, nimeona hiyo mandhari mwanana, na kuwaelekeza hasa wanafunzi wa sekondari. Yaelekea wengi wetu hatujafahamu hiki kinachoendelea au hatuna mazoea ya kuangalia anga (mwezi, nyota, mawingu, machweo na mawio ya jua). Endelea kutushirikisha na yanayoendelea angani.

    ReplyDelete
  2. Dr, can you talk anything about why rainfall are not raining at this month,does is it relate with what you demonstrated

    ReplyDelete
  3. AHSANTE SANA DR.JIWAJI, NIMEKUWA NATOKA NJE KARIBU KILA SIKU KUANGALIA ANGANI NA NIMEWAAMBIA WATU KADHAA NAO WAMEPENDA PAMOJA NA WATOTO ZAO. LAKINI MIONEKANO ULIOTOA KTK PICHA IMEFIFIA, KWA WALE TULIOONA JUZI JAPO KULIKUWA NA MAWINGU ILIPENDEZA SANA NA JANA NDIO KUZIDI KWA VILE KULIKUWA HAKUNA MAWINGU. ENDELEA KUTUJUZA MAPEMA TENA INGEFAA NA KTK MAGAZETI/REDIO N.K. THANKS AGAIN DR.J.

    ReplyDelete
  4. The Moon the planets do not affect the weather or the climate.

    Weather and climate are caused by the radiation from the the Sun which heats up the land, water, plants and all things on the surface of the Earth. This causes the atmosphere (air) surrounding the Earth and the water vapour that is in the air to heat up. This in turn causes winds that move the clouds that form when the water vapour condenses in the upper atmosphere.

    The Moon the planets and stars are too far away to affect the weather.

    The distance and orientation of Earth from the Sun changes over many thousands of years and this causes long periods over which the whole Earth has been covered by ice in the past.

    Dr N T Jiwaji

    ReplyDelete
  5. Dr. N T Jiwaji unastahili pongezi endelea kutuelimisha kuhusu sayansi hii ya angani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...