Wafanyabishara wa mbolea waliokamatwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma jana kwa tuhuma za kuuza  chumvi walioiweka katika mifuko ya mbolea na kuwauzia wananchi kama mbolea aina ya SA, kutoka kushoto Abdilai Abdala(42) Yasin Gawaza(48) Festo Sanga(25) na Ajda Halfan(36) wakiwa katika kituo kikuu cha polisi mjini songea.
PICHA NA MUHIDIN AMRI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Maustadhi mbona mnatia aibu namna hiyo. Nyinyi badala ya kuwa mfano wa jamii mnakuwa mfano wa mashehe wezi. Kumbukeni aya ya Mwenye Enzi Mungu inayosema kuwa "adhabu kali itampata mnafiki". Mnavaa kanzu kumbe wezi!!

    ReplyDelete
  2. Mtoa maoni wa kwanza acha kuingiza udini, hapa hawakuandika kwamba ni masheikh wamekamatwa kwa kuuza mbolea feki. Fikiria kabla ya kuandika.

    ReplyDelete
  3. hapo juu mtoa maoni wa pili hajaandika kitu...hapa inatakiwa maoni.wa kwanza katoa maoni yake. Wanaotufunza maadili mema ni viongozi wa dini. Sasa mwenzetu katinga na vazi la heshima kidini, then anatenda maovu....ni bora angekuwa katika vazi la kawaida. Sasa wewe mtoa maoni wa pili hapa udini uko wapi? Nani asiyejua padri kiibada huvaaje na mashehe au waislamu wenye kumcha Mungu huvaaje!

    Pole

    ReplyDelete
  4. Wadau Kumbukeni:

    KUWA:

    1.Ubaya hauna kwao wala hauna Kabila!

    2.Matatizo ya Dunia yakikufika hayapigi hodi!

    3.Shida, Misukosuko na Raha ni sehemu ya Maisha ya ki Dunia!

    Kilichobaki,,,,DUNIANI; TUCHAPE KAZI, TUWE MAKINI KTK KILA MATENDO YETU KIMAISHA NA TUZIDISHE IBADA !

    ReplyDelete
  5. Watu wengine bwana eti matatizo ya kidunia, Hayo ni matatizo ya kidunia au ni matatizo ya kujitakia??

    ReplyDelete
  6. Wewe mchangiaji wa kwanza ni vizuri ukafikiri kabla ya kuseme unachotaka sema,,,taarifa tu 'kila avaaye kanzu au baragashia si shekhe/muislam'

    Ila nakubali kuwa hawa jamaa yawezekana wakawa waislam ila sina hakika kama ni ma-shekhe.

    ReplyDelete
  7. jamanmi eh maisha yamekuwa magumu watakula wapi? hiyo ni moja kati ya Technic-ability za kukubalika kwa jamii hasa vijijini huko.

    ReplyDelete
  8. TUSITOE HUKUMU YA MOJA KWA MOJA:

    Hatufahamu wengi wetu undani wa Mkasa mzima, kwa vile hawa ni Watuhumiwa bado hawajafikishwa Kizimbani ambako ndio itathibitika zaidi msimamo wa tuhuma zao.

    TOENI MAONI ILA ACHENI KUWACHAFUA WATU KWA MISINGI TU KWAMBA MMEONA MUONEKANO WAO NA KUWA WANA KANZU, BADO HAWAJAINGIA KATIKA HATIA KAMILI !

    ReplyDelete
  9. mchangiaji wa pili. huyo hapo ni shehe mimi namjua. usihamaki kwani hata mashekhe wanavunja sheria tuuu.
    wewe eleza point. alivyovaa tulitegemea awe mfano boraaaa... au basi na sisis tuvae hivyo na kufanya makosa??? hiyo ndio point ya mchangiaji wa kwanza. pole

    ReplyDelete
  10. Pia hili ni Somo Kamili na Changamoto tosha ya hali halisi ya kimaisha.

    Ugumu wa Maisha unachochea kufikia hata yule ajuaye Maadili na taratibu za mwenendo mwema wa kimaisha anazikiuka ili mradi Mkono wende Kinywani!

    Njaa haina Ujasiri !

    ReplyDelete
  11. Wadau tuache Maoni ya KUCHAFUANA KIDINI KWA KUWA MMEONA WAISLAMU HAPO.

    Sawa, hawa Wandugu wameingia ktk hatia kwa jitihada za kutafuta 'Chakula cha maisha' ingawa njia walitumia siyo sahihi.

    Je, mbona hamshangai PADRE SIXTUS KIMARO (WA KANISA KATOLIKI UBUNGO DAR ES SALAAM) ALIYEMLAWITI KIJANA WA CHINI YA MIAKA 18 ,MATOKEO YAKE PADRE AKAFUNGWA JELA MIAKA 15 ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...