Bw Rena Calist, Mwenyekiti wa Miss East Africa Pageant

*JUMLA YA WAREMBO 3,120 WAMESHAJIANDIKISHA KATIKA NCHI 16 ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI TANGU KUTANGAZWA RASMI KWA MASHINDANO YA MWAKA HUU HADI SASA KWA LENGO LA KUTAKA KUSHIRIKI MASHINDANO YA UREMBO YA MISS EAST AFRICA 2012 AMBAYO FAINALI ZAKE MWAKA HUU ZITAFANYIKA MWEZI SEPTEMBER JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA

IDADI HIYO NA INAYOZIDI KUONGEZEKA, NI KUBWA ZAIDI KUWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA MASHINDANO HAYO YA MISS EAST AFRICA

*WAREMBO WOTE WANAOJIANDIKISHA KATIKA NCHI ZAO WATACHUJWA
KATIKA MASHINDANO YA AWALI YATAKAYOFANYIKA KILA NCHI ILI KUPATA WASHINDI WATAKAOZIWAKILISHA NCHI ZAO KATIKA FAINALI
ZA MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA 2012

*MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA MWAKA HUU YAMEFANYIWA MABADILIKO MAKUBWA KWA AJILI YA KUYABORESHA ZAIDI IKIWA NI PAMOJA NA KUBADILI MFUMO WA UENDESHAJI WA MASHINDANO HAYO AMBAYO NDIO MASHINDANO MAKUBWA YA UREMBO KWA UKANDA HUU WA AFRICA

*MIONGONI MWA MABADILIKO YALIYOFANYIKA, NI KUANZIA
MWAKA HUU MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA YATASHIRIKISHA
MREMBO MMOJA KUTOKA KILA NCHI INAYOSHIRIKI MASHINDANO
HAYO TOFAUTI NA MFUMO WA ZAMANI AMBAPO KILA NCHI ILIKUWA
IKIWAKILISHWA NA WAREMBO WAWILI

*MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA 2012  YANATARAJIWA KUVUTA HISIA ZA WATU WENGI AMBAPO YATAONYESHWA “LIVE” NA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISION NA KUTIZAMWATIZAMWA NA MAMILIONI YA WATU WENGI NDANI NA NJE YA MIPAKA YA BARA LA AFRIKA.
* NCHI 16 ZITAKAZOSHIRIKI MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA 2012 NI
TANZANIA, KENYA, UGANDA, RWANDA NA BURUNDI, ZINGINE NI SOMALIA, DJIBOUTI, SUDAN, MALAWI, ERITREA,ETHIOPIA, PAMOJA NA VISIWA VYA REUNION, MADAGASCAR,COMOROS,MAURITIUS NA SEYCHELLES.

*FAINALI ZA MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA HUANDALIWA NA KAMPUNI YA RENA EVENTS LTD YA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAYO PIA NDIO WAMILIKI WA MASHINDANO HAYO.

Rena Callist,
CHAIRMAN,
MISS EAST AFRICA PAGEANT

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hivi mabinti zenu nao hushiriki au mna 'parade' mabinti wa wenzenu tu!!

    ReplyDelete
  2. Huyu jamaa bado yupo tu?

    ReplyDelete
  3. wewe ulijua kaenda wapi?

    ReplyDelete
  4. Wewe ulijua kaenda wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...