Gari ndogo aina ya Suzuki Escudo lenye nambari za usajili T 105 ATL likiwa limeingia msingini mchana huu maeneo ya Viwanja vya Furahisha,karibu kabisa na kiota cha Maraha cha Villa Park,jijini Mwanza.Chanzo cha Gari hii kuingia mtaroni,ni dereva wa Gari hii aliekuwa yuko bwaksi (kalewa tilalila) kupita kiasi aliekuwa ametokea Villa Park na kuingia barabarani bila tahadhali tena kwa mwendo wa kasi.alishinda kuuhimili mwendo huo kutokana na kulewa kwake na kujikuta akiingia mtaroni humo.hakuna alieumia kwenye ajali hii.
 Dereva wa Gari hilo akitoka garini humo huku akifurahia kuwa amepona,kiasi kwamba kila aliekuwepo kwenye eneo la tukio alibaki kumshangaa.
 akaina isiwe tabu,maana safari yake ishakatishwa.akavuka kopo moja la bia na kuanza kulikata huku akiwa ameweka na pozi kabisa.
 Hivi ndivyo mitaro ya jiji la Mwanza ilivyo,ambapo ukipoteza stepu kidogo tu kama alivyofanya huyu jamaa.basi ni lazima ukae.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kwa nini haiwezekani kuwekwa vizuizi?? Ulaya mbano wanaweka ,sisi tunapenda sana kutojijali,na pia mwandishi alivyolifanya jambo la gari kuingia mtaroni kama utani vile,au ni kitu cha kawaida bongo,majuu hii ni top news,na angetafutwa mchawi hapa,kama ni manispaa au mkandarasi ,kwa nini hakuweka mabomba ya kutenganisha mtaro na barabara,kwetu aka!! ni comedi,eti kikopo cha bia.Zebedayo

    ReplyDelete
  2. Anko pata yai hapo kwanza!!

    ReplyDelete
  3. Mimi ni mhandisi, lakini kwa kweli kama standard za ujenzi wa mitaro kwa Tz ndo kama hivi, basi naanza kusomea sheria ili niachane na uhandisi. Mtaro wenyewe kuna eneo umebana kabisa, kwingine ni mpana. Nadhani wamefanya hivyo kukwepa hiyo nyumba. Sasa sijui nani kamfuata mwenzie, barabara au nyumba? Pili mitaro inatakiwa kufunikwa. Maana hivyo, ni hatari kwa watoto na walevi.

    ReplyDelete
  4. Hivi tanzania tunaishi dunia gani...yaani inakuwaje mtu anaendesha gari akiwa amelewa na inaonekana ni jambo la kawaida tu.Tusipokabiliana na hili ongezeko la magari na madereva walevi huko mbele kunagiza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...