Ankal hongera kwa kazi nzuri.

Naomba nianikie hii hoja yangu ya haja kuhusiana na hawa jamaa zetu wa Tanesco na uuzaji wa mita zao za Luku.
 
Kwa wakati na miaka tofauti, Nimekuwa nikifuatilia kuunganishwa kwa umeme, mara zote (4) na miaka yote zoezi hili halijawahi kwenda smooth. kwamba mita zimeisha ama waya umeisha au vyote kwa pamoja, na kwa kusubiria miezi!

swali kwa tanesco na watanzania.

Hivi mita za tanesco huuzwa sh. ngapi toka kiwandani, maana bei ni kubwa sana kuliko around  380,000/= (or exactly figure) ya mita inayotozwa na tanzesco? na kama kiwanda kinachozalisha hizo mita kinazalisha 3 au 4 kwa siku kwamba siku zote hakitoshelezi?

nauliza hivyo nikihisi mita zinauzwa kwa bei ndogo kuliko wanavyotuuzia tanesco- toka tanesco office, hata hivyo, wananchi tuko tayari kulipa hata mara 4 yake ili mradi tupewe umeme, kwa nini wasilete nyingi za kusubiria wateja wakati pesa watu wanatoa tena kwa kubembeleza!
 
waya na luku tanesco nachukulia ni sawa na Mtandao wa simu za mikononi network ipo ila hawatengenezi vocha!!

Sio tanesco, sio wanasiasa ambao hawalioni hili. ni kero ni kero.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. yaani mdau hapo juu nakupa hongera kwa kuandika hili kwa kweli. mimi nina miezi sita sasa nyumba yangu haina umeme kila ukienda Tanesco wanakuambia hakuna Luku jamani hivi tutaishije ??? Tanzania yetu jamani mbona kila kitu ni kero??

    ReplyDelete
  2. Luku zipo nyingi lakini zinafichwa kuna watu wanafungiwa siku hiyo hiyo wanayo omba LUKU kwa zaidi ya shillingi 1.5 million kama ukikataa utaambiwa ngoja ziagizwe hiyo ndiyo Tanzania yetu.

    ReplyDelete
  3. TANESCO NDIO SHIRIKA PEKEE AMBALO WATU WAKE WA STOO HAWAJUI MZIGO ULIPOSTOO,HAWAJUI WANAPOAGIZA MZIGO UNAKAA KWA SIKU NGAPI,HAWAHUJUI MAHITAJI YA WATEJA KWA MWAKA,NDIO SHIRIKA AMBALO MZIGO UKIINGIA STOO HAKUNA STOCK TAKING HADI UISHE NDIO WANASTUKA KUAGIZA TENA.KWAUJUMLA NI SHIRIKA LA WASHENZI TU HATA MACHANGUDOA KINONDONI WANAJUA STOCK YA CONDOM KWENYE MABEGI YAO NAKAMA ZITATOSHELEZA WATEJA WAO KWA SIKU.SHIRIKA LINAVYONIUZI HILI NINGEKUWA NA UNDUGU NA OSAMA TUNGEPAWEKA PALE UBUNGO PALE GROUND ZERO WASIONEKANE KABISA.

    ReplyDelete
  4. Ndg yangu pole sana, Mita za Tanesco haziuzwi kama mtu kakuambia hivyo anakudanganya. Angalia mita zote utakuta zimeandikwa mali ya Tanesco na hurusiwi kutoa wala kuhamisha kupeleka sehemu yo yote pia ukimaliza mkataba nao wanachukua mita yao bila kurudisha hiyo pesa uliyotaja pole sana kama haukulijua hilo.

    ReplyDelete
  5. Mdau mleta maada uko juu sana. kweli tanesco wanaboa sana sana. iweje wanatukodishia mita kwa bei kubwa halafu huduma haipatikani? kwanza kwenda kupimiwa ni mlolongo mrefu, na hasa usipoonyesha kutotoa chochote ndio ujipe pole, ikiwa huna usafiri wako ujute kutokuwa nao! ukishapomiwa kusainiwa eti enginner katoka, njoo wiki ijayo, ukienda supervisor alikuwa hajasaini, njoo baada ya wiki 2, ukishasainiwa kwenda dirisha la mafaili lako halionekani, ukitoa maziwa kidogo kwa ajili ya faili unapewa, kwenda kulipa foleni ileeee, caunta anaongea na shoga. ukimaliza unaambiwa subiri tumeagiza mita, zitakuja wiki ijayo, wiki ijao ukienda wanasema zitakuja baada ya mwezi 1, baada ya mwezi unaambiwa zipo bandarini, baada ya miezi 3 tangu zoezi lianze mita zinakuja unaambiwa service line wire zimeisha!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...