Asalaam Aleykum Uncle Michuzi.
Pole kwa mihangaiko na shughuli za kila siku. Ndugu yetu tunaomba utupeperushie website yetu hii kwa wana libeneke ili tuweze “share” maneno mazuri ya Muumba wetu kwa ndugu na jamaa Waislaam na wasiokuwa waislaam. Tunashukuru kwa utu wako na mungu akujaalie kila la kheir.
Masalaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mashaallah

    ReplyDelete
  2. tunaomba msilete udini hii blog ni ya watanzania wote na makabila yote yaliyomo, asanteni

    ReplyDelete
  3. Anony Wed Apr 04, 04:02:00 AM 2012...Unaonekana unamatatito ya kichwa! Watanzania wote na Makabila yote ndani yake kuna wana walio Jisalimisha kwa Muumba wao. Na mwenye hii blog ana dini ndo maana huweka matangazo ya kila dini. Kama hukufurahishwa tengeneza Blog yako uweke mambo unayotaka na usome mwenyewe.

    ReplyDelete
  4. We anonymous wa 04:02:AM acha ujinga. Kuna udini gani hapo, kila mtu ana uhuru wa kuwafahamisha wengine jambo ambalo lina manufaa katika jamii. Hata wewe ukiwa na jambo lipitishe katika blog....usilete chuki binafsi.

    ReplyDelete
  5. Du! Mdau wa pili inaonekana unahasira kweli na hawa jamaa, Kina Mwakasege na wengineo kila siku wanauza sura kwa michuzi lakini jamaa wala hawapulizi upupu ila hili kwako limekuwa issue.

    ReplyDelete
  6. Nanukuu "Sichagui, sibagui, atakayenizika simjui" mwisho wakunukuu,author Michuzi, sasa wewe mtoa hoja kwanini ulete mambo ya dini?? kwa mtaji huo nime goma kutembelea website yako hiyo yenye udini.

    ReplyDelete
  7. Jamni mdau wa pili hapo juu ndo wewe mwenyewe unaonekana una udini,,maana inaonyesha hutaki kusikia kitu chochote kuhusu uislam,,Naomba nikuulize,ni matangazo mangapi Michuzi anayarusha yanayohusu ukristo?,,Na mbona halalamikiwi kuwa ana udini?,,,Yaani umenishangaza,,kweli umekereketwa mpaka unaingia katika comments kuandika hivyo!!!,,,Kuwa muungwana ndugu yangu blog hii ni ya dini zote,,na Tanzania serikali yetu haina udini,,kila mtu anaruhusiwa kufuata madhebu yoyote,,,Acha na wenziwe wajitangaze,,kama hutaki basi ignore jump katika habari nyingine,,sio unashambulia tu watu,,kwani umeambiwa hii Radio ni ya michuzi si nitangazo tu karusha na ni la kupita tu!!!
    Acha hizo Mungu wetu ni mmoja
    Ahlam ,,,UK

    ReplyDelete
  8. mtoa comment wa 2,nakushauri ukachungulie kule jamii forum angalau utapata yale uyapendayo ya dini yako tu na chuki za ajabu

    ReplyDelete
  9. Wekeni juhudi zenu katika maendeleo yenu kama mnavyotapatapata hapa. Hamna mtu anayewalazimisha kwenda kokote. Nyie si watalaamu mnajua mmefika mkabebeshwa maboksi? Wewe mtu na akili zako zote unaiingia kwenye mtandao kuwatukana ndugu zako, wamekufanyia nini? Kama hauna cha kusema si afadhari kaa kimya?kwanza ngoja nimalizie hapa maana naona najibizana na wehu. (Michuzi naomba usibanie.)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...