Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Emmanuel Nchimbi akiongea na baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Ahamadiyya nchini walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salam leo.
Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya Tanzania Tahir Mahmood Chaundry wakati Uongozi wa Jumuiya hiyo ulipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Benjamin Sawe.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi ameitaka jamii ya Wahamadiyya nchini kuendelea na utaratibu wa kuhamasisha amani na kutojihusisha na chuki za kidini.

Waziri Nchimbi ameyasema hayo leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam alipotembelewa na viongozi wa jamii hiyo waliofika ofisini hapo kwa ajili ya kujitambulisha.

Waziri Nchimbi pia ameitaka Jumuiya hiyo kuendeleza vijana kielimu ili kuwa na taifa lenye vijana wenye maadili mema na hekima kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Kiongozi wa msafara huo Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema kuwa Pamoja na mambo mengine jamii hiyo imekuwa ikijishughulisha na masuala ya maendeleo ya Elimu na Afya nchini ambapo kwa upande wa Afya, Jamii hiyo inamiliki hospitali binafsi ya Jamii ya Waislamu ya Wahamadiya iliyopo mjini Morogoro na kwa upande wa elimu wanamiliki shule ya Sekondari Kitonga iliyopo nje kidogo ya jiji laDar es Salaam.

Aidha, Sheik Chaudhry amesema kuwa Jamii hiyo pia inajihusisha na maendeleo ya Michezo mbalimbali ikiwemo riadha, mpira wa miguu, kuvuta kamba kupitia chama chake cha michezo kiitwacho ‘Safina Athletics’ kilichopo jijini Dar es Salaam.

Jamii ya Wahamadiyya iko kwenye zoezi la kujitambulisha katika taasisi mbalimbali hapa nchini ili kujenga uelewa kwa umma kuhusu kazi wananzozifanya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kapewa nini?

    ReplyDelete
  2. kupeana zawadi huzidisha mapenzi dhidi yetu,na sio lazima ufahamu alichopewa,huo utakua umbea sasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...