Gari la serekali likiwa lime fungwa pingu tairi ya mbele baada ya kukosa sehemu ya kupaki katika mtaa wa zanaki karibu na DTV,wahusika (yaani wafunga pingu magari) nawashauri kabla ya kufunga gari pingu waadae sehemu ambapo dereva akiwa katika jiji anaweza kuweka gari lake wasikimbilie kufunga magari wakati jiji lenyewe halija jiandaa sehemu zinazo weza kuegesha magari mfano kufunga pingu gari la serekali nadhani siyo kitendo cha kiungwana hiyo nisawa nakumfungia bosi wako mlango wa ofisi

Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. justice for all people whether government or individual, and those governments that are required specifically to see the realities of their city
    just cover them in. They park the car parts they want because they can not walk long term, is due to mismanagement of those serekalini

    ReplyDelete
  2. Kwani ukiwa na plate no. ya serikali hutakiwi kufuata sheria za barabarani? Give me a break!

    ReplyDelete
  3. Kosa ni dereva siyo gari!

    ReplyDelete
  4. I believe no one is the above the law . Haya ndiyo mambo yanayoturudisha nyuma watanzania sababu ni gari ya serikali basi ni sawa kuvunja sheria. Magari ya serikali ndiyo yalitakiwa yafuate sheria kwa hiyo hilo gari limefungwa ni sawa kabisa.

    ReplyDelete
  5. Tena Magari ya serikali ndiyo yanatakiwa kuwa namba 1 kufuata sheria...Leading by examples

    David V

    ReplyDelete
  6. Dreva wa gari ya serikali sio serikali ndio maana anaweza hata kupata ajali. He sould comply

    ReplyDelete
  7. UK au USA huwezi kuzuia gari ya serikali kuegesha maana wako kazini hao. Msikae mkadanganyana bure dola ni dola tu hata kwenye nchi zenye demokrasia.

    ReplyDelete
  8. Humu naona watu wengi bado ni mbumbumbu. Inabidi kisomo cha watu wazima kirejeshwe, ili watu wafunguke kidogo. Gari la serikali linaweza kupaki mahali popote. Maana inawezekana likawa linamfuatilia mtuhumiwa fulani labda kumkamata. Sasa likimwona ameingia sehemu fulani, kwanza dereva alipeleke mita 500 kutafuta parking, unadhani huyo mtuhumiwa atawasubiri. Lazima tujuwe kuwa makachero wanaweza kutumia gari lenye namba zozote, ilimradi waweze kufanikisha malengo yao.

    ReplyDelete
  9. Ni kweli lakini sometimes hawako kazini wako kwenye biashara zao wanafanya shoppiing za nyumba ndogo. Serikali yenyewe imeshindwa kudhibiti utumiaji holela wa magari ya serikali ndo maana watu hawa hawayaheshimu. Sasa gari la serikali unalikuta bar tena saa za kazi au unalikuta guest house baada ya saa za kazi sasa unataka kutwambia tuyaheshimu? yapigeni pingu tu mpaka heshima itakaporudi...tena yanatakiwa yawekwe nembo yote ili tujue ni idara gani inahusika tuyaweke kwenye TV na magazeti na hapa kwa anko mithupu....Mdau, CA, USA

    ReplyDelete
  10. Wewe uliyeandika UK au US huwezi kuzuia gari ya serikali kuegeshwa popote sijuhi unaishi UK au US ipi, pamoja na wewe uliyetoa tangazo hili la gari ya STK kuegeshwa. Gari ya Polisi au Emergency (Fire Engine au Ambulance) TU ndio inaweza kupaki popete pale na pia dereva atakuwa responsible KAMA atapaki mahali ambapo atahatarisha maisha ya wengine - INGAWA yupo kazini. Hata kama ni Doctor (labda awe 'on call') na lazima awe na ishara kwenye gari yaani 'Siren' au 'king'ora) visible au 'off duty duty' Police Officer ni lazima aegeshe sehemu iliyotengwa kwa ajili ya kuegesha kama raia mwingine yeyote yule.

    Kwetu hapa uswekeni utakuta mtu kwa kuwa ana gari ya 'Sirikali' basi hata mke wa bosi akiwa Shopping siku ya mapumziko - yaani Jumapili' basi atataka kupaki popote pale kwa kuwa gari ni ya serikali. Hivyo hao walioi-'Clamp' hiyo gari kama imepaki kinyume cha sheria ni sawa kabisa na dereva wa gari hiyo anatakiwa alipie gharama zote ili iachiwe - Period! Labda awe na sababu itayowaridhisha walio 'clamp' gari hiyo na wakaridhika nayo. Tuwe tunaandika/comment mambo tunayoyajua na siyo kupotosha watu!

    ReplyDelete
  11. kama mwaka umepita, askari kanzu wa malkia walipigwa faini kwa kupaki kiholela, hence no one is above the law.

    ReplyDelete
  12. The biggest point katika post ni Jiji kuandaa maegesho ya magari. Yaani kuwa na parking points jijini ambazo watu watalipimia kuanzia a minimum of 1 hour for parking. Then waanze kushughulikia wanaokimbia kwenda kupaki huko

    ReplyDelete
  13. Acha pumba wewe anony wa Sun Apr 29, 06:43:58 PM.
    Unamdanganya nani kwamba magari ya serikali hayatakiwi kifuata sheria USA na UK? Pumba. Gari zinazopaki popote ni gari za polisi tu; usituletee uongo kama kwamba watu hatuyajui haya. Magari mengine yote yanafuata sheria zote ; hata Bus Lane hayapiti; kwa kuwa wanapigwa fine kama wengine. None is above the law. Wewe kama umeshuhudia system za UK na USA nadhani ungepongeza walilofanya hao waliofunga gari.Kama raia anafungiwa, na gari ya serikali ifungiwe dereva akalipe fine.Full stop; usituletee pumba eti kufunga gari ni sawa na kumfungia bosi wako mlango.Kama ni wewe; basi na kibarua kimeota Majani. You have to learn.

    ReplyDelete
  14. Well @ anonys who seem to be educated and great level of understanding and maturity. Anony wa un @ 7.25 na wenzio mnaosema gari imekuwa 'illegaly clamped' rudini upya shule za msingi! Hata kama ni special operation na sio 'marked cars' zinazotumika zinaweza kweli kusimama popote ambapo hazitadhuru raia wengine na pia ni LAZIMA ziwepo 'signals'! kama sirens n.k End of story na comment zinazopotosha!

    ReplyDelete
  15. mdau wa CA, USA...SALUTE!!! anon wa 08:03...SALUTE!!! anon wa 09:40...SALUTE, Kweli tusidanganyane!!! I was in UK 1994, malkia was driving akapita zebra crossing ''akahatarisha usalama wa raia''...it was in magazeti...she wrote an apology to the concerned!...kuna kiongozi wa nchi moja tajiri sana kaskazini kwa saudi, mkuu wao alisimamishwa hajavaa mkanda, askari kuona ni mkuu akaendelea akamlima fine!...mkuu akaendelea na safari yake, jamaa akapandishwa cheo!...now what is this eti gari ya serikali kupaki holela is okay

    ReplyDelete
  16. Mimi nakubaliana na wote ninyi hapo juu,kama ni makachero au serikali iko kazini au vyovyote vile, Hamna shida, wewe si m'babe, mtafute aliye funga pingu hiyo halafu mchukulie hatua za kinidhamu na kisheria ukitaka, kwamba "we njoo hapa kwanini umefunga pingu Gari hii ya serikali, piga magoti au lala chini , halafu fungu haraka iwezekanavyo kabla sijakumeza" si yameisha.
    Mimi nasema huo ni upuuzi kwasababu Serikali ndo inayosababisha miji yetu isiwe na utaratibu unaotakiwa, kwahiyo serikali ndo inayo paswa kupata adhaa hii ya kufungwa pingu ili ikumbuke kutoa maelekezo namna ya kuijenga miji yetu, nadhani mumeelewa.

    ReplyDelete
  17. MIMI NIKO HAPA UGHAIBUN, HUWZI KUFANYA KITENDO HICHI. SERIKALI INAWEZA IKAINGIA POPOTE NA IKAZUIA BARABARA YOYOTE KWA MANUFAA YA RAIA. SASA ALIYE FANYA HILI NADHANI HATUMII AKILI LKN PIA NI MATATIZO YA NIDHANI KWENYE TAIFA LETU. NENDA MAREKANI,UK,S.KOREA,CHINA,NEWZEALAND ALL EUROPE. GOVERNMENT IS RESPECTED NA KAMA KUNA MAKOSA KUNA HATUA ZAIDI ZA KUCHUKUA LKN SI KUDHALILISHA SERIKALI.

    WANTANIA JIFUNZE,ACHA KUBWATUKA TU NA KILA SIKU TUNADHARAU SERIKALI KWA KITU DEMOCRASIA NA UTAWALA SHERIA. KAA MAREKANI AU TAIFA KUBWA UTANIAMBIA SERIKALI ILIVYO STRONG.

    ReplyDelete
  18. hatupigi hatua za maendeleo kwa kuwa na watu wanaofikiria mtindo wa huyu aliyeweka hii pist. wala lengo lake halikuwa kusema eti kukosekana kwa parking but gari ya serikali kuwa clamped. Jamaa kwa mgongo huo huo wa serikali wamekwiba hela waziwazi kesho atasema tusithubutu kuwasema wala kuwachukulia hatua kisa ni serikali. Ona wanavolipana mishahara hewa, ona gharama za magari ya serikali un accounted for eti Sh. trilioni 5 cheki halmashauri zinavyotafuna hela. uozo huo wote unatokana na hii mindset ya kuwa kwavile ni serikali basi tuogope kama shetani. No way, kamata hao wote funga gari zao pingu hata kama ni ya waziri dereva atahusika kwa kuvunja sheria za usalama barabarani...wrong parking!

    ReplyDelete
  19. Alietoa comment wa kwanza kabisa anatutia aibu ya mwaka. Tunaomba comment zifanyiwe editing na kama haiwezekani zisichapishwe kabisa. Lugha ya wenyewe kama huijui ACHA.Ichube

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 03, 2012

    Je GARI YA POLISI 'DEFENDER' mfano Maafisa wamwegesha wametoka kufuatilia kitu, Wajamaa wa Maegesho wataifunga mnyororo Gari ya Polisi kama hii ya Idara ya Kilimo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...