Salamu Nd. Michuzi,
Nilipata bahati ya kutembelea Kimondo cha Mbozi karibuni na nimeweka katika tovuti hii, picha na maelezo kuhusu hazina yetu iliyofichika kusini mwa Tanzania.
Inafaa sana kuitangaza hazina hii kwa njia zote. Wasomaji wa tovuti yako watapata maelezo kwa picha nyingi za Kimondo cha Mbozi.
Nimeambatisha picha.
Asante,
Naona viluwe luwe. Kimondo ndio nini?
ReplyDeleteati hazina ha ha haa!
ReplyDeleteKwa hakika hii ni hazina iliyosahaulika kabisa!!! I wonder wizara ya maliasili na utalii inangoja nini kutangaza eneo hili?Au hadi iundwe tume ya kufanya uchunguzi kama kawaida yetu?Ifike wakati watanzania tuneemeke na kufaidika na vivutio alivyotujaalia Mungu.Hongera sana Dr Tiwaji kwa jitihada zako za kutufumbua macho juu ya hili kwa kiasi kikubwa hivi.I appreciate your efforts.
ReplyDeleteFor really that is amazing jiwe kubwa kama hilo limetoja mwezini na kuangia tanzania.
ReplyDeletelakini bila shaka wazee wa kazi wameshalifanyia mambo mengi sana kujaribu kutafuta riziki kwa kupitia hilo jiwe
ukiangalia hapo utaona lilishawahi kukatwa kipande ili wazee wa utafiti wakalifanyie utafiti huenda likawa ni dili.
tanzania tukitangaze kimondo chetu nje ya nchi ili tujipatie wageni wengi kuja kujionea maajabu hayo.
MBONA KAMA KICHWA CHA TEMBO
ReplyDeleteKimondo kinachukua sura nyingi kila ukikiangalia pande mbali mbali. Ndiyo kivutio moja wapo. Umbo la kimondo kimeundika kwa kuyeyuka kwa chuma kinachounda kimodo hicho.
ReplyDeletePia ni kweli kwmba watafiti walijaribu kukata kipande chake kidogo kwa ugumus sana kwa vile chuma yake imeungana na NICKLE abayo huifanya kama STEEL, ambayo ni ngumu sana. Hata mhunzi wa kale tunaambiwa alikata kipande na kukitengenezea shoka. kwa sasa serikali imezuia kumegua ovyo vipande vya kimondo hiki.
Dr N T Jiwaji
Kimondo ni kipande cha mada ambayo inatokana na sayari au gimba la angani.
ReplyDeleteKipande cha gimba kikiangukia ardhini huitwa kimondo.
Kuna vimondo vya ukubwa mbali mbali kutoka chembe chembe kama vumbi hadi ukubwa wa matani mengi.
Vimondo vingi huungua kutokana na joto linalosababishwa na msuguwano katika hewa ya Dunia na kimondo. Hii inatoa mwanga na kuonekana kama nyota inayo anguka.
Kimodo kikiwa kikubwa, hakiunguwi kabisa na kipande kinacho baki huwa mara nyingi ni cha chuma.
Kimondo cha Mbozi ni moja wapo ya vipande kama hivyo.
Dr N T Jiwaji