Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi mwandishi mahiri wa Mwananchi Bw Neville Meena tuao ya mwandishi bora wa mwaka 2011 wa Jumla katika hafla iliyoandaliwa  Ijumaa usiku na Baraza la Habari Tanzania (MCT) ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar es salaam
Mshindi wa Tuzo ya Fanaka ya Maisha (Lifetime Achievement Award) Mzee Fili Karashani akipongezwa kwa shada la maua na mwanahabari machachari kutoka Lindi Bw Abdulaziz Video
 Mwanahabari mkongwe Ben Kiko akiwa na Tuzo yake 
 Ankal akimpongeza Ben Kiko kwa kuwa mteule wa wanahabari waliotukuka
Mama Edda Sanga akishuka jukwaani baada ya kupokea tuzo yake toka kwa Rais Kikwete.
Orodha kamili ya walioshinda tuzo BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi ya tukio hili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera waandishi wa habari! Nauliza hivi Ezekiel Mwalongo yupo wapi siku hizi? Maana simsikii tena kati ya wapiganaji.

    ReplyDelete
  2. Jamani Mzee Ben Kiko ndiyo kwanza nione picha yako.

    Nakumbuka sana vituko vyako kwenye vipindi ulivyokuwa unaripoti.

    Unakumbuka kisa cha yule mama Jaji aliyempiga kiatu cha ghorofa (rhizone enzi zile) mtuhumiwa mmoja wakati alipomshambulia mama mwenzake ambaye ndiye aliyeleta mashtaka.

    Kwa kweli ilikuwa ni furaha tosha kukusikiliza ulivyokuwa ukiripoti na unastahili zawadi hiyo.

    Mungu akupe umri mrefu uendelee kudunda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...