Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Balozi Raphael Lukindo huko Sinza jijini Dar es Salaam aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jumanne tarehe 27 Machi na kuzikwa Ijumaa tarehe 30 Machi katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dare s Salaam.Marehemu Balozi Lukindo aliyestaafu Mwaka 1988 aliitumikia serikali katika balozi mbalimbali nje ya nachi ikiwemo Japan,Urusi,Poland,Hungary na Czechoslovakia.Marehemu ameacha mjane na watoto wanne.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Bibi Tereza Mvaa Lukindo, mjane wa marehemu Balozi Raphael Lukindo wakati Rais Kikwete alipokwenda nyumbani kwa marehemu Sinza jijini Dar es Salaam kuwapa pole ndugu na jamaa kutokana na kifo cha Balozi huyo aliyezikwa juzi Ijumaa katika makaburi ya Kinondoni jijiji Dar es salaam.
Rais Kikwete akiwafariji wafiwa alipokwenda nyumbani kwa marehemu Sinza jijini Dar es Salaam kuwapa pole ndugu na jamaa kutokana na kifo cha Balozi huyo aliyezikwa juzi Ijumaa katika makaburi ya Kinondoni.
 Rais akisalimiana na watoto ndugu wa marehemu


  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwa hili nampongeza Kikwete sana sana ni faraja sana Raisi kuwatembelea wafiwa kwani kwa muda fulani mnapata ahueni na kusahau machungu ya kuondokewa na mpendwa wanu!
    Hongera sana Raisi Kikwete

    ReplyDelete
  2. Babu anapiga mziga kwa prezdaa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...