Home
Unlabelled
mambo ya digitali vijijini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Huu ndio Wazimu wa Kitekinolojia,
ReplyDeleteNyumba ya matope na mabati ya kuunga vipande vipande antena ya nini?
Si bora hata asiwe na simu ya mkononi achilia mbali huo ungo ili awe na nyumba angalau yenye hadhi!
Hao wenye Mpango wa Digitali wangesisitiza hadhi ya Makazi kwanza kabla ya Mradi wao huo.
ReplyDeleteHii safi kabisa!!! Maendeleo Oyeeee
ReplyDeleteAhhh nyumba yenyewe hata kwa kupigwa ngumi moja inakwenda chini sasa antena ktk paa la nyumba ya nini?
ReplyDeleteUN-HABITAT mpo wapi?
ReplyDeleteBinaadam ktk uso wa ardhi anakaa ktk nyumba mabayo ni sawa na mtu yupo nje na amejifunika viganja vya mikono !
Mahala penye makazi kama haya Magereza yanafurika kwa vile ni bora uishi kifungoni angalau utalala mahala pa salama na hadhi badala ya kuwa huru !
ReplyDeleteWote mnahitaji Miwani Hilo Dishi lipo Nyumba ya pili kule.
ReplyDeleteIncluding aliyeleta mada...mnahitaji huduma ya macho...!!!
ReplyDeleteMie nawashangaa kweli mijitu mingine! dishi liko nyumba nyingine yenyewe yanapiga makelele!
ReplyDeleteDuhh hata kama picha imepigwa kiudaku na kuwa Dishi lipo nyumba ya pili, lakini haiingii akilini wewe uweke dishi halafu Jirani yako anaishi nyumba ya Udongo !
ReplyDeleteHuko si ndio kuchoreka kwenyewe?
Yaani hata kumsaidia aweze kujenga hata kwa matofali ya bei rahisi ya vipande vipande umeshindwa?
kali ya mwaka, nimeipenda!
ReplyDeleteJamani sio mpaka uwe wewe ni Father Christmass ndio utoe!
ReplyDeleteNi jambo la busara sana tukajitahidi kuondoa tofauti za hali ya maisha ndani ya jamii zetu sisi wenyewe kwanza kabla ya kuziachia Mamlaka za Nchi na Mashirikisho ya Dunia.
Hali zingine unaangalia ubinaadamu na kanuni za ki Imani, jirani yako ana maisha duni anaishi banda la udongo, na ameezeka kwa mabati ya mapende mapande kweli wewe utakuwa upo mustarehe unaweka ungo juu ya paa la nyumba na una sechi chaneli mbali mbali za runinga nyumbani kwako?