KAMPUNI ya Push Mobile kwa kushirikiana na klabu ya Simba imezindua kampeni ya bahati nasibu kwa mashabiki wa timu hiyo ambapo mshindi atajinyakulia pikipiki aina ya bajaji yenye thamani ya Tsh 6 Milioni.
Akizindua kampeni hiyo jana kwenye ofisi za Push Mobile kinondoni jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kampeni hiyo itasaidia kuwaweka pamoja na wanachama wa klabu hiyo kongwe hapa nchini.
Mtawala alisema falsafa ya simba ambayo ni timu ya wananchi ni kuwa karibu na wanachama wake popote duniani hivyo kampeni hiyo itasaidia kuiweka karibu zaidi klabu hiyo na wanachama wake .
Naye Meneja wa Kampeni hiyo kutoka Push Mobile, Talib Rashid alisema droo kubwa ya bahati nasibu hiyo itachezeshwa baada ya siku 90 na mashabiki wa simba wanatakiwa kuandika ujumbe mfupi wa maneno (SMS) yenye neno Simba na kuituma kwenda namba 15678 ili kuingia katika droo hiyo.
Rashid alisema mbali na zawadi hiyo pia mashabiki hao watajinyakulia zawadi ya pesa taslimu tsh 50,000 kila siku ndani ya siku 90 pia washindi wengine wawili watajinyakulia pikipiki zenye thamani ya tsh 1.5 Milioni kila moja.
"Kampeni hii itahusisha mashabiki wa klabu ya simba ambao watatakiwa kujibu maswali ambayo baada ya kutuma neno Simba kwenda namba 15678 watatumia kwenye simu zao," alisema Rashid.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...