Kaka Michuzi,
 Nimeokota Leseni iliyoambatanishwa hapo juu---kama kuna mtu anaamfahamu mhusika naomba anitafute kwenye namba ya simu0768106076. Napatikana dar es salaam.
 onesmo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. wewe michuzi hizi data watu wa fraud si wanaiba kabisa.

    ficha tarehe na mwaka wa kuzaliwa basi. picha inatosha jamani na jina.

    ReplyDelete
  2. hey wewe mdau wa kwanza ni namna gani? unataka michuzi afiche vipi zaidi ya alivyofanya? au unataka kuniambia kuwa unaweza kusoma tarehe ya kuzaliwa hapo? Michuzi kaficha number ya leseni, tarehe ya kuzaliwa na hata aina ya gari anayoruhusiwa kuendesha na bado unamlaumu?

    ReplyDelete
  3. Nimependa uaminifu wa aliyeokata, nadhani anasali kwa Kakobe,
    Tanzania wote tungekuwa hivi tusingekosa baraka kwa Mungu.
    God bless u

    ReplyDelete
  4. nacheka sana kuwa tumeingia katika technology kichwa kichwa lakini bado hamna kitu. Hata anwani ya mtu haipo ktk kitambulisho chake sasa huwezi kuitumia kama kitambulisho

    ReplyDelete
  5. ally malaptopApril 04, 2012

    kitambulisho kazi yake nini sasa kama hakuna hata adress ya mhusika, bora muunde vipya tuu vyenye adress.

    ReplyDelete
  6. Wewe mdau wa pili

    ungekaa ukafikiria bila kukimmbilia ku comment kama una akili za nguvu ungejua ilikuwa hivyo na ndio maana niliandika.

    Na nashukuru ysmefutwa.

    tabia hii ndi inarudisha nyuma mtu kama wewe. unadhani wewe ni wa kwanza kusoma blog hii?

    jifunze na iwe fundisho kwa wengi wanaorukia bila kutafakari kwa nini hili au lile lipo lilivyo

    ReplyDelete
  7. Inatakiwe leseni ziwe na sehemu ya anuani au namba ya simu.

    ReplyDelete
  8. Watu wengine sijui wanamatatizo gani. Michuzi amezingatia falagha ya mwenye leseni halafu analaumiwa. Ameficha kila kitu kinachohitajika kuficha. Huko kuishi kwenu nje isiwe shida.

    ReplyDelete
  9. Huu ndio ustaarabu na utu,

    Tujenge tabia ya uaminifu,uadilifu na mwenendo mwema kama Mdau alivyofanya.

    ReplyDelete
  10. Tatizo kubwa kwa maisha ya sasa kila kitu kimekuwa ni biashara, mfano mtu anaweza kuokota afadhali Mdau maeonyesha nia ya kumtafuta mwenyewe ila mwingine atahakikisha anaitumia leseni kwa Maslahi hata ikiwezekana kuiuza au kutumia taarifa zake kwa kughushi !

    ReplyDelete
  11. asije kuwa amepoteza na dola 5,000!!! ikawa kesi

    ReplyDelete
  12. Jamani, nalazimika kushauri kidogo hapa: Katika maisha upoteaji wa vitu kama Leseni, vitambulisho, pasipoti nk ni jambo la kawaida.

    Kama kuna maadili:

    1. Mpotezaji hutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtandao wa polisi unasajili tukio hilo.
    2. Muokotaji wa kitambulisho anapaswa pia kutoa taarifa polisi na kurejesha kitu kilichookotwa kituoni alipotoa taarifa.

    Polisi wanamaliza kazi kwa kumrejeshea aliyepotelewa na kitu hicho. Hivyo ndivyo inapaswa kuwa. lakini hayo mengine ni kwa sababu ya hali duni iliyopo ya utekelezaji wa majukumu tuliyo nayo.

    Vinginevyo: Namshukuru aliyeokota na kutoa taarifa. Kwamba kuna mapungufu kama vile kuweka wazi kila kitu hapa, huo ni udhaifu tu unaorekebishika...sioni haja ya kumlaumu Michu wala kumlaumu aliyetoa wazo la kufuta baadhi ya info. wote tunatakiana kheri katika kutatua matatizo ya kila siku na kutakiana mafanikio katika maisha haya mafupi tuliyo nayo.

    ReplyDelete
  13. Ni kweli kaka umefanya vizuri.Wasiwasi wangu hujui huyo jamaa alipoteza hiyo ktk mazingira gani.Anaweza asiwe mstaarabu akakupa usilostahilimara mtapoonana. La msingi ni kupeleka police tu vitu kama hivyo.ingawa ndo na wao njaa sasa inakuwa shida hapo.

    ReplyDelete
  14. Wabongo sisi jamani vichwa vyetu havijatulia. We weka jina tu, sema leseni yake imeokotwa basi. Hamna haja ya kuweka picha.

    ReplyDelete
  15. Polisi???? Hao wanaosimama kando wakati watu wanataka kuuawa ndo uripoti kitambulisho? Heri kupeleka msikitini au kanisani.

    ReplyDelete
  16. Ukweli TZ na nchi nyingi za Afrika si kila mtu ana anwani posta. Nyumba zenyewe hazipo ktk mitaa inayojulikana kiramani, wala hazina namba kama ilivyokuwa enzi za mwalimu sasa mnategemea anwani gani iwekwe hapo?
    Naomba mnieleweshe maana ya majina yetu haya..
    Family name.
    Given names.
    Kwa hiyo ni family name ndio surname(last name)
    na Given names ni first name na middle name? Naomba maelekezo.

    ReplyDelete
  17. Kuwepo kwa picha ni jambo zuri zaidi kwa vile unaweza kumfahamu mtu kwa sura japo hamfahamiani kwa majina lakini utaweza kumfikishia taarifa ulizoona muhusika baada ya kuona ktk tangazo.

    ReplyDelete
  18. Wasanii wa Kibongo nao 'nyoko' sana huwezi amini kabisa ya kuwa Leseni hizi mpya za TRA za Komputa sasa hivi zinafyatuliwa Uchochoroni mitaa ya Gerezani Kariakoo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...