WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Taasisi ya Brahama Kumar Raja Yoga ya Dar es Salaam, Sista Lalita Patelwakati wa
tamasha la kuadhimisha miaka 75 tangu taasisi hiyo ilipoanzisha huduma ya tafakari duniani, Kituo cha tamaduni cha Russia, Dar es Salaam
Wasanii wakitumbuiza wakati wa tamasha la kuadhimisha miaka 75 tangu taasisi hiyo ilipoanzisha huduma ya tafakari duniani, Kituo cha Utamaduni cha Russia, Dar es Salaam
![]() |
Sehemu ya waliohudhruria wakifuatilia yaliyojiri wakati wa tamasha la kuadhimisha miaka 75 tangu taasisi hiyo ilipoanzisha huduma ya tafakari duniani, Kituo cha Utamaduni cha Russia, Dar es Salaam |
Tanzania imeendelea kusisitiza mashirika ya kiimani, kuhubiri amani, upendo maelewano na mshikamano baina ya waumini wake na waumini wa imani nyingine zate ili kujenga jamii inayoenzi amani, upendo, ushirikiano na mshikamano kama msingi mkuu wa maendeleo na ustawi wa jamii yetu.
Rai hiyo, imetolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma, Mhe. Hawa Ghasia, wakati wa Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 75, kwa Jumuiya ya Brahma Kumaris ya Upanga jijini Dar es Salaam, yaliyofanyikia ukumbu wa Utamaduni wa Urusi hapa jijini Dar es Salaam.
Mhe. Ghasia, ameipongeza jumuiya hiyo kutimiza miaka 75 na pongezi zaidi ni kwa jumuiya hiyo kuhubiri amani, upendo na maelewano baina ya dini mbalimbali kwa kutumia msingi mkuu wa jumuiya hiyo kuwa Mungu ni mmoja na ni Yule Yule kwa dini zote japo anaitwa kwa majina tofauti tofauti.
Waziri Ghasia, ameitaka Jumuiya Hiyo ya Brahma Kumaris, ambayo inamiliki Chuo Kikuu cha Brahma Kumaris World Univeristy, kufungua tawi la chuo inchini, ili Watanzania nao, wapate fursa ya kupata kuelimika zaidi katika masuala kiimani.
Kwa upande wake, Mkuu wa Jumuiya hiyo ya Brahma Kumaris hapa nchini, Sister Lalika Patel, amesisitiza Brahma Kumaris ambayo imekuwepo nchini kwa kipindi cha miaka 26, sio dini, bali ni jumuiya ya kimaani inatoa mafundisho ya kutafakari kwa makini (meditation) hivyo kuimarisha zaidi imani za watu wa dini mbalimbali kwa kuhubiri Mungu ni mmoja.
Katika maadhimisho hayo, mtaalamu bingwa wa mambo ya meditation kutoka nchini Urusi, Sista BK Chakradhari aliendesha mhadhara wa somo la kujitambua kwa kuwasisitiza waumini wa dini mbalimbali kwanza wanapaswa kujitambua wao ni nani wametoka wapi na wameumbwa kwa madhumini gani ndipo watakapo weza kumtambua mungu wa kweli.
Sister Chakradhari, akasisitiza watu wengi wanaogopa kifo kwa kukosa ufahamu kuhusu mwili wa binadamu ya kuwa una semu mbnili ya mwili na roho, kinachokufa ni mwili tuu, hivyo binadamu wakielimina, hawatakuwa na sababu ya kukiogopo kifo bali watajiandaa vyema kupokea kifo kwa sababu watakuwa wamepata ufahamu ni nini kinaendelea baada ya kifo cha mwili.
Watanzania mbali mbali wa dini tofauti, walitoa ushuhuda jinsi mafunzo hayo ya meditation yanayotolewa na watu wa jumuiya hiyo yalivyowasaidia kubadili maisha yao.
Leonada Peter Kisima amesema kabla ya kujiunga na mafunzo hayo, alikuwa ni mtu wa kukasirika, kugomba, na hakupata muda wa kutulia na kuisoma biblia na kuielewa, lakini baada ya mafunzo hayo, sasa amejikuta ana upendo na amani zaidi, hawezi tena kukasirika, wala kugomba, ila pia maisha yake yamekuwa ni ya mafanikio zaidi.
Shuhuda Mwingine, Bw. Leonard Kisarika, amesema kuna watu wengi wanashindwa kupata mafanikio makubwa kimaisha kutokana na kukosa utulivu, hivyo baada ya kuyapata mafunzo hayo, unajukuta unapata utulivu wa ajabu unakubali maisha yako na kujikuta unatenda yaliyo mema tuu.
Maadhimisho hayo yalipambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za kiasili za mataifa mbalimbali zilizotolewa na vikumbi mbalimbali likiwemo kundi la THT.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...