Kikosi cha Simba kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidhi ya Al Ahly Shandy ya Sudan uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 3-0.
 Mashabiki wa Simba wakifurahia ushindi wa timu yao.
 Wachezaji wa akiba wa timu ya Al Ahly Shandy wakiwa wameduwaa baada ya mchezo.

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akishangilia bao la tatu aliloifungia timu yake. Kulia ni Patrick Mafisango.
Waziri Mkuu mstaafu, Mh Frederick Sumaye akipokea zawadi ya jezi kutoka kwa Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage baada ya kumalizika kwa mchezo. Picha zote na Francis Dande
Timu ya soka ya Simba jioni hii imeifunga bao 3-0 klabu ya Al Ahly Shandy kutoka Sudan katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Wekundu wa Msimbazi ndio timu pekee kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyobaki katika michuano yote ya kimataifa inayosimamiwa na CAF, ambapo pia ni  wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa.


Simba imejiwekea mazingira mazuri ya kuingia kwenye hatua ya Nane Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kuifunga Al Ahly Shandy mabao 3-0 jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba sasa inahitaji sare yoyote kwenye mchezo wa marudiano, au kufungwa si chini ya mabao 2-0 ili kuingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.


Timu nane zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa zitaungana na timu nane zitakazofozu katika hatua hii ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, kuchuana kuwania nafasi nane za kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hongera sana Simba kwa ushindi huo mzuri na wakutia Moyo.ni mwanzo mzuri kuelekea pambano la marudiano huko sudan, mmetupa raha watanzania.Hongera sana wachezaji na benchi la ufundi pamoja na viongozi wa simba na mashabikikwa ujumla wake.

    ReplyDelete
  2. Mkuu,

    Nimefurahi kupindukia.

    Mnyama ana historia ya kuwatafuna Waarab tangu Mehala El Kubla, National, Al Ahly, Zamalek nk.

    Ushabiki mbali kwa heshima na taadhima nakuomba wewe binafsi na wadau wengine wote wenye kumbukumbu watupe historia ya Mnyama na Waarab kuanzia 1973 hadi leo.

    Mwana Simba, Helsinki, Finland.

    ReplyDelete
  3. Big up Mnyama. Onesha cheche kama za mwaka 1993. Maana ni muda mrefu toka tushuhudie mafanikio kama hayo. Muhimu mjitahidi kutokuuza wachezaji wenu mapema. Maana Rage ni 'bussines man'. Mjue kuwa baada ya kuitoa hii timu, bado mtakuwa ni kibarua kingine kigumu cha kupambana na timu mojawapo toka timu zitakazikuwa zimeshindwa kuingia nane bora ya Club Bingwa Afrika. Kwa hiyo kaza msuli. Kuingia kwenu ktk ligi kutasaidia kujingaza ninyi wenyewe nje ya nchi. Muda si mrefu mnaweza kuwa mabilionea, kama mkija kucheza Europe.

    ReplyDelete
  4. Simba Oyeeee, oyeee mwana simba hongera, simba spoti klabu....

    ReplyDelete
  5. Hongera Simba lakini safari ndio kwanza mbichi.
    Mkuu Simba sasa inahitaji kufungwa si chini ya mabao 2-0 au hayo ni makosa ya kiuchapaji tu?

    ReplyDelete
  6. Hivyo vivest vya njano ndo vimesababisha mnyama kuwa na hasira zaidi hata akawachanachana kwani ni rangi ambayo myama hataki kuiona kabisa, yaani kama Hispania wanapotumia kitambaa chekundu kuamsha hasira za ng'ombe dume wakati wa mchezo na ng'ombe huyo ndivyo hasira ya myama inapoamshwa hapa TZ kwa kumuonyesha kitambaa cha njano au kijani, atakuchana chana usijaribu.

    ReplyDelete
  7. yaani rage nakushangaa kitu kimoja unavaa kofia imeandikwa mexico hu sio uzalendo kwahiyo we wa mexico si uvae ya tanzania mambo gani hayo

    ReplyDelete
  8. Wale ndugu zetu wa KIBELAAAH jana walikuja kushangilia wasudan lakini walilala mapema kwa roho mbaya zao!!

    ReplyDelete
  9. Wallahi Haadha 'shai',,,twaibb,,,malesh?

    Kul 'shai',,,kul 'mandash'?

    Nilipoona Mwarabu anaingiza Mathemosi ya Chai Uwanjani nikajua leo Mnyama amepata 'Kibonde'!

    ReplyDelete
  10. Sasa Bwana Rage kofia iliyoandikwa Mexico ya nini??Hata kama ina rangi nyekundu.Tulitegemea iwe imeandikwa Simba ili ziingizwe sokoni na Klabu ipate mapato.Hata hivyo nawapongeza Simba kwa ushindi

    David V-Yanga Daima

    ReplyDelete
  11. Hongera Simba na uongozi. Mh. kofia ya Rage nzuri lakini ingeandikwa Simba si Mexico. Au basi angeondoa hayo maandishi. Huo nao ni mradi wa kuingiza hela. Mhe. Changamkia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...