mimi ni mdau wa globu yako kwa muda sasa, naomba kuleta ombi hili.
Kama kuna mtu anafahamu alipo kijana huyu. Anaitwa Owiso Bwana (pichani) sina taarifa kamili za wazazi wake, mama yake ndiye aliyenipa taarifa hii na baadhi ya mambo niyaandikayo hapa chini niliyashuhudia mwenyewe na pia wapo watu ambao watakuwa mashahidi wangu. Alikuwa rafiki yangu sana nilipokuwa nafanya kazi Buly kwani alinishangaza kwa matendo yake.Mwaka 2007 alikuwa na umri wa miaka 9 na alikuwa amesoma shule ya msingi takribani kwa miaka miwili na hakuwahi kabisa kusoma sekondari, lakini alikuwa akiweza yafuatayo:
1. Tayari alikuwa anasoma Fizikia na Kemia ya kidato cha 3 na 4
2. Alikuwa na uwezo wa kufanya hesabu zote ngumu za kidato cha 3 na 4
3. alikuwa anajua kusoma na kuandika vizuri kiswahili na kiingereza
4. Alikuwa na uwezo wa kutatua jambo lolote la kisayansi
5. Pamoja na kutojua kompyuta ilikuwa akielekezwa jambo moja basi anavumbua mawili mbele ( mfano mimi mwenyewe niimfundisha excel kwa sababu ya kupenda kwake hesabu na nilipomweleza kazi ya cell yeye aliweza kuweka fomula na kuifanyia kaza) achilia mbali kuwasha na kufungua excel yenyewe.
6. Akiwa na miaka mitano (kufuatana na taarifa ya mama yake ) aliweza kufanya hesabu za dada yake za darasa la saba.
OMBI LANGU
Yeyote anayefahamu alipo mtoto huyu, naomba anifahamishe au hata amlete kwenye vyombo vya habari ili kutopoteza vipaji kama hivi adimu. Aonwe na wataalamu na kumpima
ni hilo tu na natanguliza shukrani.
Mdau
Mwanangu wa Miaka mitano anafanya hayo yote bila hata kusita!! anaandika program zake mwenyewe.. yaani simple "hello world"...Yes Jambo zuri kumtafuta na kumsaidia!!
ReplyDeleteHujasema anakaa wapi sasa msaada si itakuwa ngumu sana kupata? Halafu umetoa tangazo kama la mtu anayetafutwa vile.!
ReplyDeleteJambo zuri sana, kila la heri mdau.
ReplyDeleteMdau unajikanyaga. Mara hujui alipo, mara wazazi waje ndio waliokupatia picha a maelezo hayo! Kwanini hao wZazi wake wasikuanmbie alipo sasa?
ReplyDeleteSisi tutajuahe kama una nia njema nae! Jee aa unataka kumdhuru! Kwa ujumla aelezo yako hayajitoshekezi kwetu sisi kukupa taarifa a mtu. Wasikiaa na familia yake lkn kwa njia hii hatupo tayari kukusaidia.
mdau umechanganya madesa inshort hujaeleweka.
ReplyDeletehaba kuna tatizo kapotea au nini hasa?Maana mara hujui alipo mara wazazi walikupa picha jamani kipi ni kipi! Andika tena ujumbe wako ueleweke upatiwe msaada!
Wewe unayemtafuta hakika sio mtu mwema. Umeandika taarifa nyingine umesema umezipata kwa mama yake. Sasa kwa nini usimuulize mama yake kuwa mwanae yupo wapi kama una nia njema naye. Hakika wewe sio mtu wa kupewa taarifa za huyu kijana.
ReplyDeletekwa kweli kwa jinsi ulivyo jichanganya inaonekana humtafuti kwa nia nzuri
ReplyDeletewewe ulimtelekeza mtoto sasa unamtafuta kiaina unadhani watu hawajakugundua nia yako? Tumia njia nyingine ya ukweli ya kuwa unamtafuta mama wa mtoto hyu uliyepotezana naye siku nyingi akuonyeshe mtoto wako alipo.Unazunguuuka ndio mana watu wanapoteza haki zao za msingi kwa mambo ya uongo kuzunguka kuwa mkweli na mungu atakujalia utampata tu mtoto.
ReplyDeleteAmazing!Huyu mtoto ana kipaji cha ajabu!
ReplyDeleteLakini mdau mbona unajicontradict mwenyewe? umesema hujui alipo sasa hiyo picha umeitoa wapi?
Ndo maana Watanzania tunafeli mambo madogo. kujieleza zero. wewe umepata taarifa toka kwa mama yake leo unajidai tukusaidie kumtafuta si umuulize mama yake? na hiyo picha ulitoa wapi? haupo makini na unchotaka
ReplyDeleteHuyo mtoto hajapotea wala nini. Wewe unampiga promotion tu. watoto wa hivyo wapo wengi sana majumbani bongo, tembea uone. Cha muhimu tu mjihimu mlee huyo mtoto to his fullest potential. Kama ni nyimbo basi imeingia kwenye chorus, walisema kuzaa sio kazi, kazi kulea. Msilikwepe hili jukumu.
ReplyDeleteKama unampigia promotin kujisifu pole. watoto wa hivyo wapo wengi sana majumbani bongo hii. Sio wa ajabu sana mtoto huyo. Kama ni nyimbo ndio iminia kwenye chorus. Msomeshe huyo mtoto. Wahenga walisema kuzaa sio kazi kazi kulea. Wasaa umewadia huyo mtoto mleeni to his fullest potential.
ReplyDeletejamani mdau ameomba anaejua alipo means walishapoteana muda, mbona watu wengine mnapenda tu kulaumu? km hujui basi nyamaza
ReplyDeleteHello Mdau.Yote ulioyasema kuhusu Owiso ni kweli and for more details regarding this boy.Plz call 0784 792324.
ReplyDeleteHello Mdau,For more updates regarding the Owiso Bwana plz call 0784 792324.
ReplyDeleteyupo nyumbani kwao
ReplyDeleteWatoto kama hao wenye uwelewa mwepezi wapo! kuna watoto 2 walikuwa wanasoma pale forodhani primary (academy)yaani walikuwa wanarushwa madarasa yaani wanaakili hao balaa. cha muhimu huyo mtoto atangazwe kwenye television zote, watanzania tutamsaidi tu
ReplyDeleteHAUKO MAKINI. ULIPOKUTANA NAYE ULIMKUTA PORINI AU NJIANI. SIULIMKUTA NYUMBANI KWAKE, HATA KAMA ULIMKUTA KWA NDUGU JE HAO NDUGU SI WATAKUWA NA TAARIFA NAYE. NAFIKIRI UNAVYO PRESENT TAARIFA KWENYE PUBLIC UWE MAKINI. HUYO MTOTO AKIPOTEA KUANZIA LEO KWA MAZINGIRA YASIYO ELEWEKA UTAPATA SHIDA. UNAMTAFUTA WA NINI UNAMPANGO GANI NAYE. NENDA KIJIJINI KWAKE AU ULIPOMKUTA KAONGEE NAO. NA KAMA UNA NIA NZURI NA HUYU MTOTO MBONA UNAFICHA JINA LAKO UNAJIITA MDAU, MDAU GANI MDAU WA KUIBA WATITO AU MDAU WA MABO YAPI. KUWA MWAZI.
ReplyDeleteUlivyomwona kipindi hicho kwanini hukuonyesha nia ya kumsaidia, ulishindwa nini kuongea na wazazi wake. Ingekuwa picha ya mtoto ninayemfahamu umeweka ilitangazo ningekuchukulia hatua za kisheri, mtu usiye fahamika unamtafuta mtoto wa watu kwakutumia vigezo gani, wewe ninani. jitambulishe kwanza ufahamike.
Muuu pengine ni mwanao!!!
ReplyDeletepeleka katika Tv upampata mara moja,,Lakini Ha!ha! ha inaonyesha ni mwanao,,itakuwaje mama ndo akupe hii habari na baba yake Je?
ReplyDeletesasa huyu kapotea ama la? habari hizi wamekupa wazazi wake then waulize alipo, mara huna taarifa za wazazi wake mara mama yake amekupa taarifa hizi, then kama we ungekuwa mara ya mwisho ulimuona akiwa na miaka 9 sasa mbona picha hii anaonesha akiwa zaid ya miaka 9? waulize wazazi wake..tangazo lako ungesema unaomba wadau wamsaidie ili afikishwe kwa wataalamu na sio unamtafuta wakati una contact na wazazi wake..mdau kutoka lagos..mshaka kondo ngozi
ReplyDeletewaulizeni CIA pengine wameshamchukua na hivi sasa yupo Marekani kwani wao hawaachi vipaji kama hivi.
ReplyDeleteanonymus wa kwanza, naona na wewe huyo mtoto wako ana kipaji maalumu, wasiliana na huyo mhusika pia ili awekwe kwa vyombo vya habari apate msaada zaidi wa kuendeleza kipaji chake........... Mama Lulu, Tabata
ReplyDeletejamani watanzania tutajifunza lini kusaidiana na kuacha kulaumiana? sasa mdau ameuliza tu mtu aliekuwa na taarifa za huyo mtoto waliotakiwa kujibu ni wale wanaomjua na ndio wangemuuliza hayo maswali sasa nashangaa wengine wanauliza maswali tena badala ya kujibu after all nimeona kuna mdau kampa namba ya simu nadhani anamjua watajadiliana jinsi ya kumpata, hebu tujifunze kupendana watanzania na si kuchukiana na kupenda kulaumu, kama hujui jibu ya swali acha kucomment.
ReplyDelete