Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la
Taifa, Bwana David Shambwe (katikati) akitoa maelezo ya Mradi wa Nyumba za
makazi zilizopo Ilala Mchikichi jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja wa Masoko na Utafiti wa NHC, Bwana
Itandula Gambalagi na kulia ni Meneja
wa Mauzo wa NHC, Bwana William Genya.
Kwa mara nyingine Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo (Jumanne, 24 April 2012) linazindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Mchikichi, Ilala jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kukamilika rasmi Februari, 2013.
Mradi huu upo eneo la Mchikichini karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, huduma zote muhimu za kijamii jijini Dar es Salaam zikiwamo za kiafya, shule, maduka, uwanja wa ndege na masoko.
Pia Mradi huu unatarajiwa kuboresha maisha ya wanunuzi wa nyumba hizi kwani upo karibu kabisa na katikati ya jiji, nyumba zipo ndani ya uzio kwa ajili ya usalama wao na kuna maegesho ya magari ya kutosha .
Mradi una nyumba 48 tu zitakazouzwa, kila nyumba ina vyumba vitatu vya kulala. Kila nyumba ina ukubwa wa mita za mraba 115.8 (sq.m), sebule kubwa yenye veranda, chumba kimoja cha kulala kinachojitegemea, vyumba viwili vya kulala, (vinavyotumia choo cha pamoja), jiko kubwa la kisasa na eneo la kufulia na kuanikia nguo.
Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo la watoto kuchezea, eneo maalum la kukusanyia taka, maegesho ya magari ya ziada.
Kila nyumba itauzwa kwa bei ya Sh 168,239,748.62 (bila VAT).
Tunawahamasisha wenye kuhitaji nyumba hizi wafanye mawasiliano na makao makuu ya shirika na kukamilisha taratibu mapema kwaajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.
Uzinduzi wa mauzo ya nyumba za mradi huu ni mfululizo wa uzinduzi wa miradi ya NHC unalenga kutimiza malengo ya mkakati wa Shirika wa miaka mitano ya kujenga nyumba 15,000 ambazo kati ya hizo, nyumba 10,000 ni za wananchi wa kipato cha kati na cha juu na 5,000 kwa ajili ya wananchi wa kipato cha chini.
Ukiwa mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua nyumba katika mradi huu, tafadhali wasiliana na kitengo cha mauzo makao makuu simu namba 0754 444 333; barua pepe: sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya shirika www.nhctz.com kwa maelezo zaidi.
NHC hongera lakini Du jamani ukiweka VAT inafika Tshs 200 milioni. Hapa mwanangu mnunuzi ni Mwarabu, mdosi, mfanyabiashara au fisadi. Hebu angalia hesabu hizi za kirahisi hapa:
ReplyDeleteMshahara wangu wa mwezi ni wa kima cha kati cha Tshs 500,000. Nikiweza kusavu Shs 100,000 kwa kila mwezi kwa ajili ya kulipia mkopo huo wa shs 200 million kabla ya riba basi itanichukua miaka 167 kumaliza mkopo halisi kabla ya riba yake. (Tshs 100,000 x miezi 12 x miaka 167 = Shs 200m)
Mshahara wangu ukiwa Shs 1m, nikasavu shs 250,000 kwa mwezi kilipia deni kabla ya riba basi nitachukua miaka 67 kumaliza deni. (Shs 250,000 kwa mwezi x miezi 12 x miaka 67) = Tshs 200 million
Sasa weka riba ya asilimia 29% hapo, mjukuu wa mjukuu wako atakuta mkopo bado upo.
Mpo hapo, mdau Alex Bura, dar
Hiyo pesa 168mil(USD105,000) unapata nyumba yenye vyumba vitatu,eneo zuri tu USA.
ReplyDeleteHizi nyumba za NHC mbona hakuna tofauti na zile za mashirika binafsi? maana mkikumbuka kuwa hawa NHC hawakununua hivi viwanja bali waliwanyang'anya wamiliki wa mwanzo(wahindi, nk) na kujidai kuwa zinapewa wananchi wenye kipato cha chini.
Je, 168mil mtanzania gani mwenye kipato cha chini anaweza kuwa na pesa hii????????
Nadhani NHC walitakiwa kutoza gharama za ujenzi tu kwa kila hiyo nyumba maana kiwanja ni bure-mali ya watanzania wote.
Huu ni wizi mtupu,walalahoi ndio wanakandamizwa hapa.
mil. 168 ?????? HAHAHA KIBAHA NAPATA NYUMBA 3 NA BADO NABAKIWA NA HELA KIBAOOOOO!!! kaeni wenyewe mjini
ReplyDeletemhhhhhhhhhh jmn wangepunguza pesa ni nyingi sana na izo zote ni za mafisadi na sio za kuendeleza nchi wangefanya hata Million 50 na sie walalahoi tukaweza nunua.
ReplyDeleteThe country is almost going bankrupt while the internal and external debt is huge! This is while getting numerous grants and aids, getting money from direct and indirect sources like Tanesco, Dawasco, TRA etc. But all the money is going in the pockets of corrupt leaders. A friend of mine bought goods worth Tsh.900,000 for personal use and was told to pay Tsh.400,000 as Tax (ever heard such a thing in other countries?). The country leaders ought to be ashamed of themselves and fear God as life in this world is temporary and no one or his material gains will live forever. NHC are showing your greediness by keeping such high prices, your houses might end up empty in the end like many private ones around town, mark my words about this!
ReplyDeleteJe manjua bei ya nyumba magomeni, Sinza, Mwenge hizi zilizojengwa miaka ya 1970 zinazouzwa sasa kwa ajili ya mirathi? Ni kati ya milioni 100 -150 na bado ukarabati. nadhani hizi nuyumba za NHC ni za watu wenye kipato cha kati ( 2,000,000 - 10,000,000). Kama ni kuwataka waje na mpango mwingine wa kujenga numba za bei ya chini sio wazo baya lakini haitakuwa mchikichini jamani. this is a prime area na hata kwenye mipango miji huwezi kuweka kitu pale cha chini ya kiwango fulani. Hizo zitakuwa nje ya mji!!!!!
ReplyDeleteNHC wekeni ramani ya numba na itakavyoonekana ikiisha ili kusaidia watu kufanya maamuzi!!!
MASIKINI MAISHA YAKE YOTE ATABAKI MASIKINI. NCHI, ARTHI, ENEO, SEHEMU YOTE NI MALI WA WATANZANIA. BADO WANASEMA TUNAWAINUA WALALAHOI HAPO BADO SIJAELEWA.................
ReplyDeleteAt Tsh 198.5 9M (VAT inclusive) ignore the costs of financing that capital and other expences, that is too expensive ( around US 124000 )
ReplyDeleteOnly the stronger will survive.
Hivi inamaana mfanyakazi wa kawaida anaweza kununua nyumba ya m.200? Mimi nadhani NHC wanafanya biashara kama watu wengine hivyo mamabo ya kupamba lugha kwa kusema nyumba nafuu waachane nalo kabisa. Kwa wenye uzoefu wa ujenzi, hivi nikiwa na m.50 au 60 siwezi kujenga nyumba "ya bei nafuu"?
ReplyDeleteGHARAMA MILIONI 168/=
ReplyDeleteNYUMBA NI YA PEPONI AU DUNIANI?,,,JE NHC NAOMBA MFAFANUE INAWEZEKANA NIKIFA NYUMBA NAZIKWA NAYO?
WARITHI WA KISASA HAWAKUZOEA KURITHI MADENI, WAMEZOEA KURITHI MALI NINA WASIWASI HAKUNA ATAKAYELIPA DENI HILO ENDAPO NITAKUFA KABLA YA KULIMALIZA MWENYEWE.
Mpango sio kwa Wakata Manyasi!
Inaonyesha NHC wamewalenga 'Wateja' wao MAALUM !
It does not make any economical sense. Whoever atakanunua TAKUKURU wawe nae begi kwa bega. Mmmmhhh! Wizi mtupu
ReplyDelete