Balozi Mteule wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Benjamin M. Rugangazi akiwasilisha nakala za hati za utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (MB) ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Dkt. Benjamin M. Rugangazi baada ya Balozi huyo kuwasilisha nakala za hati za utambulisho ofisini kwa Waziri leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. mbona wazungu wana washilisha Ikulu kwamwenye nchi mwenyewe?

    mdau paris

    ReplyDelete
  2. Tafadhali soma vizuri. Hizo ni "nakala"; huwa zinawasilishwa Wizara ya Mambo ya Nje. Originals huwa zinawasilishwa kwa Rais, Ikulu.

    Hakuna cha wazungu hapa, bali ni taratibu zinafuatwa.

    ReplyDelete
  3. bila kuwakumbatia wazungu hatujafurahi ,tupendane afrika kila balozi walitakiwa wawakilishe kwa huyo waziri lakini !!!!!!

    ReplyDelete
  4. Mdau Paris wacha ujinga! Kumbe kukaa huko hakujakusaidia: protocali ni kwamba kwanza unawakilisha nakala Wizara ya Mambo ya Nje na kisha hatua ya pili ndo anawasilisha hati original kwa Mkuu wa nchi!

    ReplyDelete
  5. Mh. Michuzi,
    Asante sana blog yako inatupa sana elimu nyingi.

    ReplyDelete
  6. Vijana wetu wajuvaji (wajuvi) lakini hawajui chochote, waambie kushabikia siasa ambayo vilevile hawaijui

    ReplyDelete
  7. watalaam wa foreign affairs naona mmewakilisha vizuri kwa majibu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...