Naanza kwa jina lake, Mtukufu Maulana
Atupe rehema zake, Atuongoze bayana
Kila mtu ana yake, Sikuye hawezi kana
Kwaheri bwana Kanumba, Pema Mola akulaze
Shairi naliandika, Kalamu wino machozi
Najikaza kuishika, Nilibuni kwa majonzi
Maini yanikatika, Katutoka kiongozi
Kwaheri bwana Kanumba, Pema Mola akulaze
Majonzi yametukumba, Afrika mashariki
Ametutoka Kanumba, Kifo hakitabiriki
Karudi kwake Muumba, Alotaka afariki
Kwaheri bwana Kanumba, Pema Mola akulaze
Huzuni umenitanda, Moyo ukinenda mbio
Nikiitazama sanda, Kifwatacho ni kilio
Tutaenzi zako kanda, Filamu ndo masalio
Kwaheri bwana Kanumba, Pema Mola akulaze
Safari imewadia, Pasi watu kubaini
Kaka ukafwata njia, Jongomeo kwa manani
Sanaa itafifia, Bila we’ si burudani
Kwaheri bwana Kanumba, Pema Mola akulaze
Msanii ulo bora, Nakusifu hadharani
Sio Tanga si Tabora, Wewe ndio namba wani
Filamu zitadorora, Umetutoka rubani
Pole sana ankal pole kwa sote inshaalah mwenyezi mungu amuondolee adhabu y kaburi. Ameen.
ReplyDeleteJAMANI KWELI KIFO CHA KANUMBA NI PIGO KUBWA KWA TANZANIA.
ReplyDeleteNAUNGANA NA MTUNZI WA SHAIRI HILI KWA UCHUNGU MKUBWA NIKIANGALIA PICHA HII YA MTOTO WA MWANAMKE MWENZETU. MUNGU AKUTIE NGUVU MAMA KANUMBA NA MTEGEMEE MUNGU KATIKA MAISHA YAKO
AMINA
shairi zuri
ReplyDeleteJinale nitangulize, Mtukufu Rahmani,
ReplyDeletePenye kheri tuongoze, tungalipo duniani,
Nuruyo utuangaze, kesho kifika usoni,
Rabi pema akulaze, Kanumba hatukuoni.
Nchi nzima sikitiko, bara hadi visiwani,
Wengi pata mshituko, anguka zimia chini,
Shitushwa na kifo chako, pasi umwa wala nini,
Rabi pema akulaze, Kanumba hatukuoni.
Katu kukuona tena, randa mote duniani,
Hakuna atofanana, mithiliyo abadani,
Tachukuwa muda sana, kifo chako kuamini,
Rabi pema akulaze, Kanumba hatukuoni.
Ghafula umetutoka, wengi hilo katu dhani,
Mamia tumeshituka, hawa ngumu kuamini,
Mola kwita meitika, nasi tupo safarini,
Rabi pema akulaze, Kanumba hatukuoni.
Pengo katu kuzibika, hata ajaribu nani,
Daima takukumbuka, khasa kwenye yako fani,
Kwa mazuri wasifika, nje ya nchi na ndani,
Rabi pema akulaze, Kanumba hatukuoni.
Kifo ya wote safari, tunapita duniani,
Huzuka bila khabari, hakichaguwi fulani,
Hiyo ni ya Mola siri, kwetu waja tu kizani,
Rabi pema akulaze, Kanumba hatukuoni.
Pema Mola akulaze, dua katu kukukhini,
Nuruye akuangaze, kutuliza kivulini,
Pepo yake akwingize, ya hesabu kijawini,
Rabi pema akulaze, Kanumba hatukuoni.
Real the great Steven Charles kanumba your always in our mind but dah................!,any way rest in peace Steve Charles kanumba
ReplyDeleteIle siku ya mwisho ya Kanumba,Ijumaa Kuu,wanaohusika na uchunguzi wa tukio zima wajaribu kufuatilia kwa karibu sana ratiba ya kutwa nzima ya Kanumba siku ile,alizungumza na nani kupitia simu yake,alikutana na nani wapi na saa ngapi,nini kilifanyika katika makutano hayo,kuanzia giza lilipo ingia alikutana na nani na wapi saa ngapi,alirudi nyumbani kwake saa ngapi akiongozana na nani kwa usafiri gani,chakula cha jioni alikula wapi akiwa na nani na nani alietayarisha chakula hicho,na je aliporudi nyumbani usiku alikuwa katika hali gani,kalewa au hapana,alianza kunywea wapi akiwa na kina nani,aliporudi nyumbani je aliongeza kilevi zaidi au hapana,akiwa na nani nknk, haya na maswali mengine mengi zaidi yatahitaji kujibiwa ili kujiridhisha kwamba kifo cha Kanumba kilikuwa "ni cha Mungu mwenyewe,wakati wake ulikuwa umetimia na hapakuwepo mkono wa mtu".Yakipatikana majibu ya maswali hayo hakika "yatatuwezesha kupata usingizi na kusahau yaliyopita maana ni kazi ya Mungu".Theory za kusukumwa na Lulu au Ugomvi kwa sababu tu Lulu alikataa kutoka na Kanumba kwenda kwenye kumbi za starehe usiku ule binafsi hazina uzito wa kutosha na zinajaribu kuficha ukweli halisi wa nini kilichotokea!Lulu anaweza kuwa amebambikiziwa Zengwe hili bila ya yeye mwenyewe kutambua nini hasa kinacho endelea.Maana Kanumba alishafikia uwezo na hatua ya kuweza kuwapa kazi au kuwaajiri Wasanii wenzake ambao alianza nao kazi pamoja kwa mara ya kwanza kabisa.Ukitilia maanani alikuwa katika hekaheka za kuaga wasanii wenzake kwamba anakaribia kusafiri kwenda Marekani kufanya shootings za filamu mbalimbali,hilo nalo ni jambo ambalo pengine halikuwapendezesha baadhi ya wasanii na marafiki zake wa karibu! naomba kwa unyenyekevu mkubwa masuala haya na mengineyo yaanyiwe kazi ili ukweli halisi ubainike tupate amani ya roho.Kifo cha ghafla cha Kanumba kimetuuma sana!
ReplyDelete