Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kiaro
----
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA(JWTZ)
12 Aprili, 2012

Rejea taarifa yetu kwa Vyombo vya Habari iliyotumwa kwenu juzi tarehe 10 Aprili, 2012. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kufanya masahihisho.

Jenerali Ernest Mwita Kiaro alizaliwa tarehe 01 Januari 1923 badala ya tarehe 01 Julai 1925.  Aidha, alistaafu utumishi Jeshini tarehe 31 Machi 1994 badala ya tarehe 25 Februari 1992.  Tunaomba radhi kwa tofauti hiyo.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania pia linaomba kuwatangazia wananchi wote kuwa, mazishi ya Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kiaro yanatarajia kufanyika tarehe 14 Aprili 2012 nyumbani kwao Tarime mjini, kwa heshima zote za kijeshi.  Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 13 April 2012.

Imetolewa na 
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu:             0764-742161      
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Daah! Inabidi muombe radhi tena. Maana tarehe za mazishi ziko mbili. Hiyo kurugenzi ya habari inabidi kupigishwa rigwaride kwakweriii!

    ReplyDelete
  2. Hiyo ndiyo Tanzania. Hata Mkuu wa Majeshi hatujui alianza kazi lini na kusitaafu kwake. Na hata mazishi yake pia. Hii kali kwelikweli.

    ReplyDelete
  3. pole familia ya kamanda na mzee kiaro akapumzike mahali pema peponi. Nataka kusema hili kwamba ni aibu kwa kubwa saaanaa kwa jeshi kushindwa kuwa na server yao yenyewe mpaka wanatumia email ya yahoo..AIBU !!

    ReplyDelete
  4. Mdau wa pili 12,10AM,mambo ya kukanganikiwa (kuchanganikiwa) yapu hata huku MAMTONI, don`t be too hard on Bongoland.

    ReplyDelete
  5. email address ya jeshi letu ni ulinzimagazine@yahoo.co.uk, sasa hili jeshi ni la Tanzania au la UK?

    ReplyDelete
  6. kweli nyie kazi yenu inatumia nguvu tu sio akili.sasa umeweka kosa jingine ili uombe tena radhi kesho?

    ReplyDelete
  7. Mmekosea, yaani kataarifa kafupi namna hii kanakuwa na makosa?!

    ReplyDelete
  8. Aisee sasa mazishi ni tarehe 14 au 13??? Mbona haileweki hii!!! Halafu nyumbani kwao au kwake??? Hiki ni kichekesho kwa kweli isitoshe kwake sio Tarime mjini ni kijijini. Senki yuuu.

    ReplyDelete
  9. Mnaolaumu mnajua kazi ya Jeshi lakini? Haya masuala ya kuandika na kuweka kumbukumbu sio kazi ya mwanajeshi. Mafunzo ya Jeshi ni juu ya kupambana na adui. Wanafundishwa sehemu za kupiga ili adui afe. Akifuzu mafunzo hayo amemaliza basi.

    ReplyDelete
  10. Tangu Jenerali Kyaro afariki dunia, hatujaona wasifu wake wowote zaidi ya sifa za juu juu. Hii ni kwa sababu makamanda wa Tanzania ni wagumu sana kukubali kufanyiwa mahojiano wakiwa hai. Niliwahi kumfuata Jenerali mmoja aliyepata kuwa Mkuu wa JWTZ kule KUrasini akanitoa nduki akisema magazeti pekee aliyoyajua ni Daily News na Uhuru!!

    Huyu Kyaro kafariki bila kuacha wasifu wake mwenyewe. Lakini wanaomfahamu wanasema alikuwa kamanda makini sana. Sasa Jenerali Musuguri naye ni mzee kweli kweli kiumri. Si ajabu Mungu akamuita, lakini kama wenzake waliotangulia mbele ya haki, naye hataki kabisa kuhojiwa kuhusu maisha yake.

    Wakati Fulani Rais Kikwete akiwa Kaboya mkoani Kagera akataka waandishi wa historia wawaandikie vitabu majenerali hawa wakiwa hai, lakini hakuna utekelezaji wowote. Juzi hapa kuna kitabu cha Vita ya Comoro, wakubwa wamekikalia kabisa. Yaelekea hawataki kiandikwe ili siku moja baada ya miaka mingi sana, kiandikwe na mtu ambaye hata Comoro haujui inafanana vipi.

    JWTZ lazima wabadilike kwa kuruhusu makamanda hawa wazungumze wenyewe wakingali hai.

    Mdau

    ReplyDelete
  11. Apumzike kwa amani kamanda kiaro. Bado taarifa zina utata - ina maana alistaafu akiwa na umri wa miaka 71

    ReplyDelete
  12. Wote mnao laumu hamjui kuwa kazi kubwa za jeshi ni vita na intelijensia, haya mambo ya yahoo.co.uk na kuweka kumbukumbu ni zenu nyie mnaotumia muda mwingi kwenye computer. Tuko bize na usalama wa nchi, hakuna kuremba ebo!

    ReplyDelete
  13. JWTZ tengezeni anuwani yenu wenyewe bila kutumia Yahoo ili msiripuwe wenyewe.

    mazishi siku mbili tarehe 13-14 Fatuwa.

    ReplyDelete
  14. Halafu sahihisho lingine ni kuwa vyombo vya habari vinaandika jina lake ya mwisho kuwa ni: KYARO, je ni KYARO au KIARO? Tunaomba ufafanuzi kwa kumbukumbu kwa bado vyo vya habari hadi leo, 04/13/2012 nimeona vinaandika KYARO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...