Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar atafanya mkutano na Watanzania tarehe 11 Mei 2012 mjini Houston, Texas. Watanzania waishio maeneo ya karibu kwenye miji ya Houston, Dallas, Oklahoma, Kensas, Lousiana, New Mexico na kwingineko, wanaombwa kufika kwa wingi siku hiyo.
Aidha, Mhe. Balozi ataambatana na Afisa wa Uhamiaji kutoka ubalozini Washington DC ili kutoa huduma za kikonseli ikiwemo ile ya kupokea maombi ya kubadili pasi za zamani za kusafiria ili kupata mpya (New generated Machine Readable) wakati wa ziara hiyo.
Huduma hiyo itatolewa kuanzia tarehe 11–13 Mei, 2012. Anuani ya mahali ambapo mkutano na zoezi la pasi litafanyika, itatangazwa na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Mjini Houston, Texas.
KARIBUNI WOTE
Imetolewa na:
Ubalozi wa Tanzania, Washington D.C,
1232 22nd St. NW, Washington D.C 20037
Telephone: (202)884-1080, (202)939-6125/7
Fax: (202)797-7408
Tarehe: 27.03.2012
Wabongo wote wanataka makaratasi siyo passport mpya!! Mtajibeba!!!
ReplyDeleteTAHADHARI JUU YA SIFA ZA URAIA:
ReplyDeleteTafadhali sana hatuwezi kugawa Uraia wa Tanzania kama pipi !
Wapo miongoni mwa Waliokuwa Watanzania hapo awali ambao kwa sasa sifa hiyo hawana tena kwa njia kama zifuatazo:
1.Waliopata Uraia wa Marekani tayari lakini wanaweza kujichanganya kwa Misingi ya kujulikana kama wanagali bado ni Watanzania wakachukua nafasi hii wakati Kisheria hawana sifa tena.
2.Maisha Duniani yamekuwa magumu sehemu zote, wapo waliofikiri kuwa na Uraia wa Kigeni ndio suluhisho la maisha kumbe sivyo mambo yako vile vile na sasa wana tapatapa kutaka tena Utanzania.
3.Sheria ya Dual Citizenship /Multcitizenship Muswaada wake haujapita bado Bungeni Tanzania kama utapita itakuwa ni Msaada kwa Ma Diaspora.
Hivyo Muh. Balozi TAFADHALI ZOEZI HILI LIFANYIKE LAKINI HATUWEZI KUTOA HAKI ZA URAIA WA TANZANIA KAMA NJUGU LAZIMA TARATIBU ZIZINGATIWE HATA IKIWEZEKANA KUFUATILIA KWANZA KWENYE MAMLAKA ZA MAREKANI KABLA YA KUBADILI PASIPOTI YA MTU.
Mdau wa kwanza Anonymous wa Wed Apr 04, 04:46:00 AM 2012
ReplyDeleteHao watoa Makaratasi ni Mamlaka za Serikali ya huko Marekani ambazo kwa sasa Dunia nzima imefilisika hawawezi kubeba mizoga na mizigo ya Wahamiaji haramu na wasio kuwa na sifa zenye tija kama Watanzania walioishi miaka kibao huko wakibweteka na maisha !
Makaratasi ktk nchi zote Dunia nzima yanatoka kwa watu wenye sifa za kitaaluma tu.
Mdau wa kwanza,
ReplyDeleteKwa taarifa yako wapo watu kibao huko MAREKANI na Ughaibuni kwingine ambao wanaishi nje ya sheria ambao hawawezi hata kusafiri kwenda nchi zingine wala kusafiri kuja Nyumbani Tanzania.
Lakini cha ajabu bado wanajipa matumaini ya kupata makaratasi!
Wewe Mdau wa kwanza,
ReplyDeleteMakaratasi atatoa nani wakati Serikali zote Dunia nzima zina madeni na zimefilisika?
Unafikiri makaratasi yanagawiwa kama ubuyu?,,,wanajali vipaumbele kwanza kwa wenye sifa za kitaaluma na rekodi nzuri ya kijamii sambamba na kufuata taratibu za kishetia tokea waingie huko.
Zaidi ya hapo kumpa mtu makaratasi ina maana Mamlaka za Serikali zinabeba jukumu la kumpatia haki za mafao ya kijamii muhusika kitu ambacho kinaingiza gharama wakati nchi zimeshafilisika kwa matatizo ya kifedha na kiuchumi Duniani.
Kwa mwenye akili nzuri aliyepo Ughaibuni ni bora akabaki na u Tanzania wake akajirudia nyumbani aje kulima au kukata mkaa Kaliuwa-Tabora!
Ah, ah, ah, inaonekana watu wengi hamfuatilii habari za Kimataifa!
ReplyDeleteWewe Dunia nzima inamatatizo ya kuporomoka na kudorora Kifedha na Kiuchumi ikiwemo hiyo MAREKANI yenyewe hayo makaratasi atatoa nani kwa wazamiaji haramu wa Kibongo?
Elewa makaratasi yanapotoka yanampatia mtu haki ya mafao ya jamii ambayo yanagharimiwa na Serikali ya Marekani,,,Serikali za Dunia nzima zimefilisika ikiwemo ya Marekani, je unaweza kwenda kuazima jamvi Msibani?
Ni vema watu wakajifunza ya kuwa suluhisho la kudumu la kukabiliana na maisha ni kujenga uwezo wa kujiamini na sio kutafuta Uraia wa kigeni !
ReplyDeleteMiongoni mwa Wakongwe wa Diaspora ni Wayahudi ambao kwa Karne nyingi wamekuwa wakiishi uhamishoni lakini wakapata mwamko kuwa Asili yao ni muhimu zaidi kuliko Uraia wa Kigeni na ndio maana wao ndio Jamii inayoongoza Duniani kwa mipango mbali mbali ya Diaspora.
HONGERA MAMA MAAJAR KWA JITIHADA ZAKO BINAFSI NA KAZI YAKO NZURI INAYOONEKANA. HUKU LONDON SIKU HIZI MIKUTANO YA WATANZANIA IMEKUWA NDOTO. HATA ILE SIKU MOJA YA KILA MWEZI ULIYOJITOLEA KUONANA NA WATANZANIA, IMEOTA MBAWA. PIGA KAZI MAMA, VIONGOZI KAMA NYIE NDIVYO INAVYOTAKIWA KATIKA JAMII
ReplyDeleteWABONGO BWANA, NUKSI VIBAYA MNO! NDIO DOKTA REMMY AKAIMBA UKIWA NA ROHO MBAYA KILA UNACHOFANYA PIA NI KIBAYA! SABABU MOJA YA KUDUMAA KWA MAISHA YETU NI ROHO MBAYA, WIVU NA CHOYO KISICHO KIFANI. KWA NINI YOU BOTHER KAMA MDAU ANASUBIRI MAKARATASI? IWEJE UJIFANYE RAIS WA DUNIA KWA KUTANGAZA SERA ETI KILA NCHI HAITAKI WAGENI SABABU YA KUPOROMOKA KWA UCHUMI WA DUNIA. MCHUMI GANI AMEHUSISHA UMASKINI NA UJIO WA WAGENI. WABONGO VIPOVU VYA KINYWA VINAWATOKA KWA ROHO MBAYA! MWENYE ROHO MBAYA NA ALE JEURI YAKE, MAKARATASI YANAENDELEA KUTOKA SI MAREKANI TU, HATA UK, SWEDEN, UDACHI NA KWENGINEKO! SABABU MOJA YA WAHINDI KUITAWALA DUNIA NI KUJILIPUA KILA PEMBE BILA KUONEANA CHOYO. WABONGO TUNARUDI NYUMA KWA KASI. ACHA ROHO MBAYA WEWE! Mndengereko
ReplyDeleteAnonymous wa Wed Apr 04, 12:40:00 PM 2102
ReplyDeleteRoho Mbaya?,,,kwani Wadau wanaotoa ukweli hapo ndio Serikali zinazotoa hayo Makaratasi Ughaibuni?
DALILI YA KUTEGEMEA MAKARATASI NI UVIVU NA SAIKOLOJIA YA UTUMWA KWA KUPENDA KUISHI UTUMWANI NA ZAIDI NI KUTOJIAMINIA KIMAISHA KAMA MTANZANIA!
NI VILE WENGI HAMFAHAMU LUGHA ZAO HAO JAMAA WAKIKAA KTK MABUNGE YAO KUNA MVUTANO MKUBWA SANA.
WANAUCHUMI NA VYAMA VYA WAFANYA BIASHARA NA WENYE VIWANDA BAADHI WANAKUBALI WAGENI NI UKOMBOZI NA HULETA MAENDELEO NCHINI MWAO NA WENYE MSIMAMO MKALI DAIMA WANAWAHUSIHSA WAGENI NA UHALIFU, KAMA UJAMBAZI,UBAKAJI,UKOSEFU WA AJIRA, UKAHABA NA KUHARIBIKA KWA JAMII ZAO.
KUBALI USIKUBALI UGHAIBUNI NI UTUMWANI WENYEJI 100% HAWAWAPENDI WAGENI WANACHUKIA KAMA HAWAJIONYESHI WANAFICHA LAKINI UKWELI NDIO HUO.
SASA KWA UKWELI HUU HAKUNA DALILI YA ROHO MBAYA ISIPOKUWA HAPA HABARI KAMILI NDIYO HIYO Mndengereko WEWE NI BORA URUDI RUFIJI KULIMA MPUNGA NA KUVUA KAMBALE UKIWA HURU KWENU!
Ati nini?
ReplyDeleteKuishi kwa msaada wa Makaratasi?
Maisha ya Kitumwa ya Ughaibuni siyawezi na wala siyataki bora nilime Kijijini Tanzania!
Acheni wandugu kutuaibisha sisi ndugu zenu mkiwa huko Ugenini.
ReplyDeleteSawa mjaribu hayo Makaratasi kuomba wakikataa bora mrudi kuja kushiriki kilimo Nyumbani Bongo!
Mndengereko Wed Apr 04, 12:40:00 PM 2012
ReplyDeleteUNASUBIRI MAKARATASI?
HUU NDIO UPUUZI GANI SASA???
MNAPOTEZA MUDA MREFU SANA UGHAIBUNI MNASUBIRI KITU AMBACHO WENGI HAMFANIKIWI ILA MNAJIPA MATUMANINI TU NA MUDA UNAKWENDA.
NI AIBU MNDENGEREKO KUWA MTUMWA UGENINI WAKATI KIASILI WEWE NI MWINYI UNAYEVAA MSULI KIUNONI NA FULANA LAINIII KABISAA, UNATAKIWA KUWA NA MASHAMBA YA MPUNGA RUFIJI,,,AHHH KAMA MAMWINYI WENYEWE WANAKUWA HIVI SASA BASI,,,YA NINI UWE MTWANA UGENINI?
MAKARATASI UNASUBIRI HUPATI RUDI RUFIJI UJE KULIMA NA KUVUA SAMAKI!.,,,,,,,
Hivyo muda Mndengereko unasubiri hayo makaratasi ndio kusema mwanaume upo Jikoni kwa Mzungu unapika?
ReplyDeleteAu upo Jumba la kulelea wazee unawatunza kwa posho la nusu mshahara la kujitolea?,,,maana huna status kamili Ugenini hivyo unalipwa kwa 'panga' la maana au nusu BEI !
KWA TAARIFA YENU WADAU, MNDENGEREKO NI KATIKA WANAOAMINI KUWA ULIMWENGU UMEUMBWA NA ALIYEUUMBA AMETOA RUHUSA YA VIUMBE WAKE, WAKIWEMO BINADAMU, YA KUISHI POPOTE TU. UTUMWA NI VITENDO SI PALE UNAPOISHI. NYIE WADAU MBONA MMEKIMBILIA KWETU PWANI MKAACHA UNYACHUSANI, UCHAGANI, UHAYANI, UMACHINGANI, UPARENI, UKINGANI, USAMBAANI NA URANGINI? JE HUO NI UTUMWA NAO? ALHAMDULILLAAH NIMESHAKUMBA MAKARATASI, NIKASOMESHWA NA KUPEWA KAZI YA MSHAHARA WA WAZUNGU. NA SI MIMI TU, TUKO WENGI HUKU "UTUMWANI" NA MASHAMBA PIA TUMENUNUA NA TUNASHIRIKI KILIMO KWANZA. NA ALHAMDULILLAAH TUKISHUKA UKONGA TUNAHESHIMIKA KAMA NYINYI MLIO HURU JAPO SISI NI WATUMWA. IT'S LIKE THAT WATANZANIA WENZANGU MLIO HURU. ILA ACHENI ROHO MBAYA. Mndengereko, ukerewe
ReplyDeleteEhee wabongo kweli niwaosha vinywa, mnaongea sana. Ebu pungezeni hasira za kuwachukia kaka na dada zenu wa Ughaibuni bila sababu. Mtasema mpaka mtachoka, jamaa bado watachomoka bongo. Na nyie na kelele zenu wote mnatamni kuchomoka hamna ujanja.
ReplyDeleteWewe Wajanja wamechomoka wameona Ughaibini ni kutwanga maji ktk kinu wamerejea Nyumbani wanavuta pesa zao ndefu tu!
ReplyDeleteNi bora mrudi kuja kulima na kufanya Umachinga badala ya kupoteza muda bureee na kujenga matarajio msiyoyapata huko Majuu.
Majuu ilikuwa miaka ileee na siyo sasa, mkae mkijua!
Mrudi na muanze na Vibaru na kazi za muda huku mkisubiri kazi za Taaluma zenu:
Kazi za muda mfano:
WANAUME:
1-Kuchoma vitumbua ,maandazi na chapati kwa Wahindi mjini jioni na usiku.
(MTAJI NI KARAI NA MWIKO WA CHUMA, LITA 1 YA MAFUTA YA KUPIKIA,NGANO KILO 1, MCHELE KILO 1 NA HAMIRA)
2-Kazi za usafi wa mazingira kama kuokota chupa za plastiki za maji ya kunywa,kuzibua mitaro na kutapisha vyoo.
(MTAJI NI MFUKO MKUBWA WA PLASTIKI WA KUBEBEA MGONGONI NA NGUVU ZAKO)
3-Kuokota vyuma chakavu na kuwauzia mawakala.(MTAJI NI WEPESI WAKO KUOENYA KATIKA MAGEREJI YENYE BIDHAA NA NYUNDO,BISIBISI NA SPANA YAKO YA KUFUNGULIA ILI KUKUSANYA)
WANAWAKE:
1-Kuwa mama ntilie/ mama lishe
2-Kulima mboga na kusindika matunda
3-Kuuza maji ya jumla na vocha za simu.
kwa vile wengine elimu mnazo mmezipata huko Majuu mtasubiri kwa kazi hizi za muda na baadae mtapata kazi za kudumu au mipango ya Kujiajiri ya kudumu kulingana na Taaluma zenu.
Wabongo Majuu:
ReplyDeleteHatuwezi kuwapa Pasipoti zetu Tanzania kirahisi hivi, kwa kuwa wengi mpo nje ya Sheria haijulikani mko wapi (MPO KAMA MMEKUFA VILE),,,Nchi mlizopo wengi mnaishi nje ya Sheria na huku nyumbani mlikiuka muda wa kukaa Ugenini mnahesabika kama Watoro nchini!
Anonymous wa Thu Apr 05, 03:52:00AM 2012 na Anonymous wa Thu Apr 05, 05:24:00 AM 2012
ReplyDelete....Na nyie na kelele zenu wote mnatamani kuchomoka hamna ujanja.....
Nyie Wadau wa juu wala hatutamani kuchomoka kwa vile tupo Bongo na pesa tunapata!
1.Sasa mtu pesa unazo hapa Bongo ya nini ukabebeshwe mabox Majuu?
2.Mtu pesa unazo Bongo kwa nini ukafanyishwe kazi kwa masaa Majuu?
3.Mtu unazo pesa Bongo ni Ubalozi gani utakunyima Visa kwenda Majuu huku ukiwa nazo pesa za kutosha ktk Akaunti Benki huku vigezo vya ziada ,shughuli za kuaminika,rasilimali ukitimiza?
Bora nifanye kazi ya kuuza Genge Bongo kuliko kubeba mabox Majuu!
ReplyDeleteLOHH,
ReplyDeleteNiiache pesa Bongo nikabebeshwe mabox huko Majuu?
Hata kwa visa na tiketi ya bure sitaki!
Labda niitwe Mahakama ya Dunia-The Hague Uholanzi, huko Majuu au Marekani nikituhumiwa ugaidi kwa mabavu wanipeleke !
ReplyDeleteWandugu Majuu mnaitia hasara nchi ktk uzalishaji mali:
ReplyDeleteKumbukeni mezaliwa Tanzania na Mkadirio ya maisha kwa Mtanzania (Life expectance) ni miaka 56.
Sasa hebu tupige hesabu za Kiuchumi, mfano wewe unaondoka ukiwa na umri wa miaka 20-25 hivi wastani ni miaka 23
56-23=33 unmebakiza miaka 33 ya kuishi ,
Endapo utakaa miaka 10 ukingoja Makaratasi na bado hujapata.
33-10=23 hebu angalia ulichofanya tokea uzaliwe hadi sasa inakuwa 23-23=0
Huku ukiitia hasara nchi kwa kushusha GDP uzalishaji mali kiuchumi kwa miaka ya umri ulioishi hadi sasa huku ukizalisha (sifuri) NA KUMI YA KUKOPA 23+10=33 HADI SASA.
Kama ungelima Mbaazi mfano kwa mwaka unavuna Gunia 10 kila gunia ni wastani wa US$ 100.00X10= US$ 1,000.00
KWA MIAKA 33 X US$ 1,000.00 =US$ 33,000.00
UTAKUWA UMEITIA HASARA NCHI KWA US$ 33,000.00 HUKU WEWE UKIWA HUNA KITU HADI SASA NA SHERIA UGENINI HUJAPATA !HUKU UKIBAKIWA NA MIAKA 23 TU YA MASIAH UKIONDOA KIFO KUPITIA AJALI, KANSA NA UKIMWI !