Mshauri wa Huduma Umoja wa Mataifa nchini Bw.George Otoo akifanya Presentantion juu ya ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mawasiliano kwa Maafisa Mawasiliano na Uhusiano waliohudhuria mafunzo hayo.
 Washiriki
 Bw. Yusuph Al Amin kutoka Umoja wa Mataifa nchini akichambua vipengele vinavyohusiana na jinsi mawasiliano zinavyoweza kuchangia maendeleo. 

 Mtaalam wa masuala ya Teknolojia ya Habari Bw. Ayub Rioba akitoa somo kuhusiana na mipango na mikakati ya Serikali ya Mawasiliano ambapo pia alizungumzia juu ya umuhimu wa kufata maadili wakati wa kufanya mawasiliano katika semina ya mafunzo ya siku moja kwa Maafisa Mawasiliano wa Idara mbalimbali za Serikali.
 Kaimu wa Mwakilishi Mkazi Dkt. Julitta Onabanjo akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Uhusiano wa Wizara mbalimbali nchini iliyoandaliwa na United Nations Communications Group kupitia Ofisi ya Rais iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nchini Tanzania Bw. Salva Rweyemamu akitoa nasaha na shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo amesema ni muhimu kwa ajili ya kuongeza ufahamu kwa maafisa mawasiliano na Uhusiano wa Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali.
Washiriki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mawasiliano katika idara za serikali na mashirika ni kitu muhimu sana ila cha kusikitisha ni kwamba hapa Zanzibar kitu kama hiki hakipo na kama kipo basi hakitiliwi maanani kabisa. Na mbaya zaidi pale kinapokuwapo basi hufanywa na watu wasiokuwa na sifa za kielimu za fani hiyo! Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilione hili, sijui Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar ana kazi gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...