Mwanahabari Sophia Mpunga wa radio Country Fm , Tumain Msowoya wa Mwananchi ,Mahija Zayumba (Nuru Fm)Alein Philip (Ebony Fm ) Godfrey Mushi ( The Guradian ) na Anita Boma (Uhuru )wakivuka daraja hilo la kitalii katika hifadhi ya Ruaha Iringa
Mwanahabari Alein Philip wa Ebony Fm ,Happines Matanzi wa Tanzania daima Iringa ,Paulina Kuye wa Nuru na Laurian Mkumbata wa ITV wakivuta daraja la mto Mdonya katika hifadhi ya Ruaha
Wanahabari wakivuka daraja la kamba ya mto Udonya katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha hakika ni zaidi ya utalii iwapo utafika hifadhi ya Ruaha Iringa
Mwanahabari wa radio Country Fm Iringa Sophia Mpunga (kushoto ) akiwa na mwandishi wa radio Nuru Fm Mahija Zayumba katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha huku nyuma yao kukiwa na twiga
Mwanahabari Paulina Kuye wa Nuru FM akipiga picha na Twiga katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha wakati wa ziara ya wanahabari mkoa wa Iringa katika hifadhi hiyo ya Ruaha
Wataka kujua dhidi ya Swala ?
Mwandishi wa habari wa ITV mkoani Iringa Laurian Mkumbata akijiweka sawa kwa kuchukua matukio katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya ziara ya siku tatu ya kuhamasisha utalii wa ndani katika hifadhi hiyo kubwa kuliko zote Tanzania
Mwandishi wa habari wa Nipashe Iringa VickyMacha akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa hifadhi Bw Marando
Madereva wa gari la wanahabari wakishangaa wanyama katika hifadhi hiyo ya Ruaha
Wanahabari mkoani Iringa wameanza kuhamasisha utalii wa ndani katika hifadhi ya Ruaha kama njia ya kuwahamasisha zaidi watanzania kupinda kutembelea hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa ambayo ni hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania ila pia kuhamasisha utalii katika hifadhi za mikoa ya kusini ikiwemo ya Kitulo, Katavi na Ruaha ambazo bado zipo nyumba kwa uhamasishaji. Picha zote na Francis Godwin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hii imetulia:

    1:Daraja-Wahandisi wa ujenzi wanalifahamu zaidi ili,tulifundishwa kidato cha pili Physics mambo ya Beam,sijui Tension.

    2:Mahija-Ndiyo yule alikuwa redio moja maarufu sana Tanzania??

    3:Utalii wa ndani-Bado sana,sasa mfano mm na na familia yangu nikitaka kwenda kutembelea mbuga say Mikumi au Ruaha ninaanzia wapi,napakiza familia kwenye gari naelekea getini au naingia mkataba na 'tours'?Hizi habari nazipata wapi,ikiwemo suala la gharama za hoteli,nk?Mwenye 'idea tafahdali'.

    David V

    ReplyDelete
  2. Hayo madaraja ya aina hiyo hujengwa kwa kuhimili uwezo fulani. Nyinyi mumekwenda kujirundika kwenye kidaraja hicho halafu kikikatika inakuwaje?

    ReplyDelete
  3. @David D, Kwanza nakupongeza sana kwa kuwaza kwako kwenda na watoto kutembelea mbuga zetu

    kwani hata mimi nimejuwa kitu gani nimekikosa wakati niko tanzania sikuweza kulifikiria suala kama lako leo niko ulaya hapa na nilikuja hapo kama mara 3 na groups za wataliiikanibidi niingie mbugani
    Ni sehemu safi sana kuona wanyama uwapo na watoto wako utasoma mengi na ndio nikagunduwa kuwa hawa wazungu sio wapumbavu kutoa euro zao kwenda serengeti

    ila nakushauri tu kama uko na uwezo tafuta guide ambae atajuwa njia uwapo ndani ya mbuga kwani tatizo sio kufika ila kujuwa wapi utamuona simba kwa mfano na uwapo mgeni huwezi ukajuwa hivi vitu

    siku niliyofika mbugani hata usingizi unalala vizuri usiku kuliko nilipokuwa hotelini dar kwa kuogopa kuibiwa ila uwapo mbugani hakuna mwizi
    jambo moja katika safari zangu zote za tanzania niwapo na wageni wangu nikutoka dar kwenda zanzibar sielewi nikwanini wazungu wanatakiwa walipe ticket kwa dolla ya kimarekani wakati ni watu kama sisi isitoshe hata ticket zao wazungu wamezichapicha rangi nyengine

    wakati sisi hapa kwao ticket tunanunuwa kwa ile ile euro na rangi ile ila ya mzungu sasa hapa sipati jibu hata hawa wageni wananiulizia hili suala

    na nimeshawashauri watu wa TTB walifuatilie hili kwani ni aibu kumbaguwa mtu kwa rangi yake na isitoshe bora umuuzie kwa bei ile ile na aruhusiwe kutumia tsh kwa vile huyu mtu yuko ndani ya tanzania

    Nashauri watanzania wenzangu wenye uwezo waende mbugani ukirudi utapata kujuwa mengi sana

    binafsi mbali kuwa hii sasa hivi ni kazi yangu hapa nilipo ila nahakikisha watoto wangu kila mwaka nawapa raha za kwetu hapo

    @ david kwako wewe gharama sio kubwa kwavile ni mtanzania hulipi usd pale getini ila tafuta mtaalamu akutembeze ukiwa mbugani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...