Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya (kushoto) na Meneja Mawasliano wa kampuni hiyo, Jackson Mmbando wakijibu maswali ya wanahabari wakati wa uzinduzi rasmi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo leo. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo.
Katibu Mkuu Idara ya Mwasiliano na Teknolojia katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Seychelles, Benjamin Choppy (katikati) akihojiwa na vyombo vya habari katika hafla ya uzinduzi wa wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia mradi huo. Kushoto ni Mwakilishi wa kampuni ya Airtel nchini Seychelles, Gail Talma Jumeau na kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya ( wa nne kushoto) akisaidia kazi ya uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania hadi nchini Seychelles katika eneo la Msasani, jijini humo jana katika hafla ya uzinduzi rasmi wa uwekaji huo ambao Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia utekelezaji wake. Wengine ni mafundi na wawakilishi wa makampuni yanayosimamia mradi huo.
Mafundi wakiwa kazini wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekaji wa mkongo wa mawasiliano kutoka jijini Dar es Salaam hadi nchini Seychelles jijini humo jana. Airtel ni moja ya makampuni yanayosimamia utekelezaji wake.

Waziri wa Maliasili na Viwanda wa Shelisheli Bw. Peter Sinon amesema nchi yake itanufaika na upatikanaji wa mawasiliano ya mkongo wa taifa kutoka Tanzania kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya taifa hilo.

Mkongo wa taifa wa mawasiliano uliozinduliwa miaka 2 iliyopita na Rais Jakaya Kikwete umeweza kuzinufaisha nchi jirani kama Kenya, Uganda, Rwanda,Burundi na sasa Shelisheli.

Akiongea katika fukwe za bahari ya hindi jijini Dar es Salaam eneo la msasani ambako uwekaji wa mlongo huo ndio ulikoanzia mwishoni mwa wiki hii Waziri Sinon amesema kuwa mpango huo ukimalika utaiweza nchi yake kukuza sekta ya mawasiliano na upatikanaji wa taarifa mbalimbali jambo litakalo saidia kukuza uchumi wa nchi hiyo.

“Hii ni nafasi nzuri ya kipekee na ndio maana hata sisi shelisheli tunaipa kipaumbele ili kukamilisha zoezi hili la uwekaji wa mkongo huu wa mawasiliano, tunaamini tukimaliza kila kitu itasaidia sana kukuza pato la nchi kulingana na umuhimu wa mawasiliano” alisema Bw Peter Sinon- Waziri wa Maliasili na Viwanda Shelisheli

Kwa uapnde wake Katibu Mkuu kiongozi kwenye ofisi ya makamu wa rais wan chi hiyo anayeshughulikia ICT Bw Benjamin Choppy ameelezea faida za uwepo wa mkongo huo kuwa ni pamoja na kutoa mawasiliano ya uhakika na bora kwa nchi hiyo

“Sasa hii ni dalili ya kutoa bidhaa bora ya mawasiliano kwa kuwa ukamilifu wa uwekaji mkongo huu tutapata mwasiliano bora zaidi” alimaliza kwa kusema Katibu Mkuu kiongozi kwenye ofisi ya makamu wa rais wan chi hiyo anayeshughulikia ICT Bw Benjamin Choppy

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano Mallya ameelezea upatikanaji wa teknolojia hiyo mpya ya mawasiliano kuwa ni kati ya vitu ambavyo Airtel inavifanyia kazi kuhakikisha inaunganisha mataifa mengi ili kutoa mawasiliano yanayotoa nafasi au fulsa ya kuendeleza nchi hizo kijamii na kiuchumi pia

“tunaamini ushirikiano wetu na wenzetu wa shelisheli ni dhahiri utachangia sana kuboresha mahusiano yetu kibiashara na pia kutoa nafasi kwa nchi hizi kujijenga kijamii ma kiuchumu kutokana na faida ya mahusiano haya ya kulaza mkongo huu wa kuunganisha mawasiliano” alisema Bi Beatrice Singano Mallya

Aitel Tanzania na Airtel Shelisheli kwa kushirikiana na SCS zinatekeleza mpango wa kuweka mkongo wa taifa kwa lengo la kuiwezesha nchi hiyo kuwa na mawasiliano ya uhakika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2012

    Ndio PR inatakiwa, lakini waacheni Mafundi wafanye kazi acheni kuuza sura.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...