Kanisa la Redeemded Gospel Church tawi la Tanzania limeikabdihi Tassisi ya Alice Foundation msaada wa vyakula kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji mbalimbali na wale wasiojiweza wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.

Akikabidhi msaada huo leo Mchungaji wa kanisa hilo lililopo Ubungo NHC  mchungaji Damasus Mkenda alisema kuwa kanisa kupitia wachungaji wake mbalimbali limeona kuwa kuna hitaji kubwa lakuisaiida jamii ya watu wenye shida mbalimbali katika kata ya Ubungo ambao wanahitaji chakula.

Alisema kuwa kanisa limeamua kupitia Alice Foundation kutoa msaada huo kwa kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisaidia masuala mbalimbali ya kijamii katika kata ya Ubungo.
Msaada uliokabidhiwa ni pamoja na mchele, Unga, Sukari, Maharage, Unga wa sembe, majani ya Chai ambapo alisisitiza ili kuwa na jamii iliyobora inatakiwa watu wenye uwezo kuwasaidia wale wasiokuwa nao.

"Sisi hili kanisa letu  lina kila sababu ya kuwasaidia  watu wanaotuzunguka katika vitu mbalimbali kama vile vyakula na mengineo muhimu, hivyo kwa sasa tumeanza na hili la vyakula lakini kadiri muda unavyoenda tutawasaidia tena kwa vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu yetu ya mchango kwa jamii"alisema Mchungaji Mkenda

Naye Mwenyekiti wa Alice Foundation, Alice James Dosi alisema kuwa taaisi hiyo imekuwa ikijishugulisha  na masuala mbalimbali katika jamii ikiwa pamoja na kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu na hatarishi ,kuwezesha  akina mama  na masuala ya mazingira na masuala yanayohusu MKUKUTA

Alisema kuwa katika kata ya Ubungo kuna idadi kubwa ya watoto na watu wazima wenye mahitaji maalum ambapo aliwataka watu wengine wajitokeze kusaidia masuala mbalimbali ya kuwaendeleza watu hao..

Alisema kuwa kwa wale wenye kuihitaji kutoa msaada kwa watoto hao na watu wenye mahitaji maalum kuwa wanaweza kupiga simu namba            0713 022 558       au 0756 344 9
24 au wapige             0686 179111       au wafike katika ofisi za Alice Foundation zilizopo Ubungo  (NHC)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2012

    Alice Mungu akubariki sana unafanya kazi nzuri sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...