Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akifungua pazia kushiria uzinduzi wa Jengi jipya la kituo cha Afya cha kutoa huduma za Mama wajawazito na Watoto huko Kizimkazi Mkunguni jana,alipokuwa katika ziara ya kutembelea maendeleo ya miradi mbali mbali ya Kijamii katika Wilaya ya Kusini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akifuatana na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi,pia Waziri wa Kazi,uwezeshaji wananchi Kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman,walipotembelea Shmba Darasa la kilimo cha migomba la wananchi wa Kijiji cha Tasani makunduchi leo,akiwa katika ziara ya Wilaya ya Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akifurahi na wakulima wa shamba darasa la kilimo cha migomba wa Kijiji cha Tassani Makunduchi jana,alipofika kuona maendeleo ya kilimo hicho na kuzungumza nao,akiwa katika ziara ya Wilaya ya Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Affani Othman Maalim,alipofika Kijiji cha Tasani Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja leo,kuangalia ukulima wa kilimo cha Migomba,cha Kikundi cha Tujaribu Tasani Makunduchi,alipofika kuona maendeleo ya kilimo hicho na kuzungumza na wananchi wa Eneo hilo,akiwa katika ziara ya Wilaya ya Kusini Unguja.
Msomaji wa Risala ya wakulima wa Bonde la Mpunga la Muyuni,Wilaya ya Kusini Unguja,Maimuna Mwinyi,akisoma risala kwa niaba ya wakulima wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipotembelea maendeleo ya kilimo katika bonde hilo leo.
Wazee wa Kijiji cha Mtende Wilaya ya Kusini Unguja pamoja na wanafunzi wa Skuli ya Msingi ya Mtende wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipokuwa akizungumz nao wakati alipofanya ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya Skuli za Kijijini hapo leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2012

    MASHALLAH, angalia dada zetu na mama zetu walivovaa kiheshima and yet participate in the daily livelihood development.
    This is how we can reduce rape and HIV in our societies, SIO KUKUMBATIA TAMADUNI ZA MAGHARIBI!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2012

    Ustaarabu wa kuvaa ulianza huko huko kulikokatika mpini na kubakia jembe. Watu wamevaa jana mvaa leo kavaa nini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...