Mwenyekiti wa Chama cha CUF na Mtalamu wa Uchumi wa Kimataifa,Prof. Ibrahimu Lipumba na Mbunge wa Viti Malamu CCM na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria,Mh. Pindi Chana wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini,Ndg. Richard Kasesela walipokuwa katika mkutano wa uchumi na kujadili mgawanyo wa pato la taifa ulio andaliwa na ESRF na Ofisi ya Rais -Mipango, uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Jijini Dar Es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Chama cha CUF na Mtalamu wa Uchumi wa Kimataifa,Prof. Ibrahimu Lipumba akijadiliana jambo na washiriki waliohudhulia mkutano wa kujadili matumizi ya rasilimali na mgawanyo wa pato la taifa.Katikati ni Prof. Ngila Mwase na Bibi Antonina Espiritu (PhD) ambaye ni mtalamu wa wamaswala ya uchumi kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) lililopo hapa tanzania.
Mbunge wa Viti Malamu CCM na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria,Mh. Pindi Chana (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Madini,Ndg. Richard Kasesela wakati wa mkutano wa uchumi na kujadili mgawanyo wa pato la taifa ulio andaliwa na ESRF na Ofisi ya Rais -Mipango, uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Jijini Dar Es Salaam leo.
Baadhi ya wandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo mkutano huo ulikuwa wa siku moja.Picha na Chris Mfinanga wa Globu ya Jamii.
Waandishi wetu wa habari huwa wanahudhuria tu ,hawafuatilii, hawahoji na wala hawatafuti matokeo ya hii mikutano.
ReplyDeleteWajibu wao ni kutupa sisi wananchi taarifa za maendeleo/utekelezwaji wa maadili ya hii mikutano.
Wananchi tunataka uwazi wa mapato ya taifa kupitia maliasili zetu.