Kamishna wa Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Madawa ya Kulevya nchini,Christopher Shekiondo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Ofisi hiyo lililojengwa Suma JKT katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2006/07 ambalo limegharimu ya sh. Mil 700.Uzinduzi huo umefanyika mchana huu kwenye Makao Makuu ya Tume hiyo,Upanga Mtaa wa Maliki jijini Dar es Salaam.Wanaoshuhudia ni Baadhi ya Maofisa wa Tume hiyo.
 Kamishna wa Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Madawa ya Kulevya nchini,Christopher Shekiondo akifungua kitambaa kilichokuwa kimewekwa kwenye jiwe la Msingi wakati wa uzinduzi wa Jengo la Ofisi hiyo,uliofanyika mchana huu kwenye Makao Makuu ya Tume hiyo,Upanga Mtaa wa Maliki jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Madawa ya Kulevya nchini,Christopher Shekiondo (mwenye suti) akiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya Maofisa wa Tume hiyo muda mfupi baada ya kuzinduliwa rasmi kwa jengo lao.
Kamishna wa Tume ya Kuratibu na Udhibiti wa Madawa ya Kulevya nchini,Christopher Shekiondo (kushoto) akiongea na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa tume hiyo kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa Jengo la Ofisi hiyo,uliofanyika mchana huu kwenye Makao Makuu ya Tume hiyo,Upanga Mtaa wa Maliki jijini Dar es Salaam.
Jiwe la Msingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2012

    A waste of our tax money... NEXT...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2012

    Madawa ya Kulevya:

    Sasa kazi kwetu, kilichobaki kama wahusika hawakamatwi ni hii Ofisi kuweka uwezekano wa watu kufikisha majina ya wanaohusika na madawa ya kulevya ili mkono wa sheria uwaangukie.

    Tunasumbuliwa na matatizo magumu zaidi kama Kansa (Saratani) ,Rushwa ,Ufisadi na Ukimwi iwe na Madawa pia?

    Madawa ya kulevya sasa basi!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2012

    Jengo la udhibiti linagharimu mil 700 wakati kina mama wajawazito hawana vitanda hospital,madawa ya kulevya yanaletwa na kusambazwa na wenye pesa na wanajulikana hakuna hata haja ya kuunda tume.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2012

    Tanzania kweli ni kichwa cha mwenda wazimu. Unafikiri hayo madawa yakijengewa jengo wataacha kuuza? Imarisheni elimu, wekezeni kwenye miradi ambayo itatoa ajira kwa vijana kama hamtaona madawa yanapungua. Watu wanaingia kwenye biashara ya madawa kwa sababu hakuna njia nyingine ya ajira. Elimu yetu imezorota vijana wakimaliza shule hawawezi kujitegemea wanaota utajiri wakati mikono wameikunja au kutia mfukoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...