Mhe. Shekifu na Kamati yake wakiangalia moja ya eneo lililoanza kupata nyufa katika baadhi ya maeneo yaliyoanza kuwekwa lami. Mwenyekiti huyo alimuasa Mkandarasi huyo mambo matatu moja ikiwa ni kupata taarifa rasmi yenye uhakika kutoka kwao kuwa ni lini mradi huo utakamilika ili wawatangazie wananchi wenye kiu kubwa na barabara hizo. Pili wahakikishe ubora wa barabara hizo unazingatiwa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na tatizo la nyufa zilizoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo yaliyowekwa lami. Na mwisho ni kuhakikisha suala la fidia kwa wananchi wanaostahiki linakamilika kuepusha usumbufu wowote ule. 
 Mhandisi Msaidizi Mkazi wa Aasleff Bam International Paul Grument akitoa maelezo kuhusu nyufa zilizoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo yaliyoanza kuwekwa lami, amesema tatizo hilo limeonekana katika baadhi ya maeneo kutoka Laela kuelekea Sumbawanga hali wanayoihisi kuwa ni kutokana na asili ya udongo wa maeneo hayo. Aliendelea kuseama kuwa kwa maeneo yote tatizo hilo lilipojitokeza wameshachukua udongo na kuusafirisha kwenda Afrika Kusini na Ufaransa kwa ajili ya kuufanyia utafiti kujua tatizo ni nini ili waweze kupata ufumbuzi. Alieleza kuwa viwango vyote vya ujenzi katika kutengeneza ngazi zote za barabara hizo vimezingatiwa cha ajabu nyufa hizo zimejitokeza jambo ambalo wanalifanyia utafiti na katika wiki mbili zijazo majibu yatakuwa yamepatikana na hapo watajua nini cha kufanya kunusuru hali hiyo.
Kamati ikiangalia eneo lililochimbwa mchanga katika eneo la Kyanda ambao umepelekwa maabara za nje kufanyiwa utafiti utakaobainisha chanzo cha mipasuko iliyoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo kwenye barabara hayo. Mhe. Shekifu aliwataka wakandarasi hao waharakishe kupata majibu ya utafiti huo kwani wananchi wa Rukwa wana kiu kubwa ya kupata barabara za lami. Mwenyekiti huo aliwataka Tanroads Mkoa wa Rukwa washirikiane kwa ukaribu na wakandarasi hao kwa kuweka utaifa mbele ili tatizo hilo liweze kupata ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto Dkt. Henry Shekifu wa tatu kushoto Meneja wa Tanroad Mkoa wa Rukwa Florence Kabaka na wajumbe wengine wa Kamati hiyo ya Bunge wakishika udongo uliochanganywa na Cement na kushindiliwa ikiwa ni mojawapo ya hatua kuelekea ujenzi wa kiwango cha lami katika barabara ya Laela Sumbawanga eneo la kyanda walipokagua ujenzi wa barabara hiyo.
 Umwagiliaji kuimarisha ujenzi ukiendelea.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Aasleff na Bam International wakiendelea na ujenzi wa barabara hiyo. Mpaka sasa kilomita zaidi ya 10 zimeshawekwa lami ya majaribio na kazi nzima katika barabara hii ya Laela - Sumbwawanga imeshafikia asilimia 37 hadi kukamilika kwake.
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Rukwa Florence Kabaka akisoma taarifa ya mradi wa barabara ya Lami inayojengwa na Kampuni ya Aasleaf Bam International ya Laela- Sumbawanga. Alisema kuwa mpaka sasa barabara hiyo imeshajengwa kwa kiwango cha asilimia 37. Alieleza changamoto kubwa zinazokabili ujenzi huo kuwa ni kuchelewa kwa vifaa kufika katika eneo la mradi, nyufa ambazo zimeanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo katika kilomita 13 za mfano ambazo zimeshaanza kuwekwa lami, na Mkandarasi kuchelewa kuhamisha maji ya mvua kandokando ya barabara yaliyosababisha mmomonyoko wa ardhi kwenye barabara hizo. Hata hivyo Mkandarasia alishaanza kuhamisha maji hayo na kazi imenza kuimarika. Kuhusu nyufa Mkandarasi huyo amesema wamechukua sample za udongo katika sehemu zilizoathirika na kuzipeleka Afrika Kusini na Ufaransa kwa ajili kuzifanyia utaifiti na kupata suluhisho la tatizo hilo.
Picha ya pamoja kati ya Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambaye ni Katibu Tawala Masaidizi Miundombinu Francis Kilawe wa tatu kulia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Dkt. Henry D. Shekifu (Mb) Lushoto katikati. Wengine ni wajumbe wa Kamati hiyo kutoka kulia ni Haroub Shamis (Mb) Chonga Zanzibar, Eng. Ramo Makani (Mb) Tunduru, Juma Sururu Juma (Mb) Bububu Zanzibar, Rukia Kassim Ahmed (Mb) Viti Maalum Kusini Pemba na Herbert James Mntangi (Mb)Muheza.Picha na Habari na Hamza Temba-Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Wa Rukwa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2012

    Tahadhari, ucgunguzi wa udongo hufanyika kabla ya kutuma gharama na namana ya kujenga bara bara na sio baada ya kujenga..hapa ninawsiwasi kuwa barabara hiyo inajengwa kwa njia ya copy and paste!!! kamati tupeni jibu kuwa kwaniniupenguzi haukufanyika kablla??? hii ni sawa na kujenga nyumba ndio tufanye utafiti wa udongo. sasa wakigundua marekebisho yanahitajika pote watarudia kuifanya hii kazi???? tunarudi pale pale...eng.wa TANROAD alikuwa wapi wakati wakupitisha mikataba na kuanza ujenzi?????

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2012

    Safi sana wana kamati.Kutembelea miradi ya huko ndani bara ni suala zuri sana.Kama kuna muda unawatosha mpite nba barabara ya Sumbawanga-Mpanda-Uvinza-Kigoma-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi.

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2012

    Jamani nijuavyo mimi soil analysis inafanyika kabla ya ujenzi kuanza. Kwa maana hiyo tatizo la udongo kuwa na nyufa lingejulikana mapema na hatua zingechukuliwa mapema kuepusha hali hiyo. Sasa iweje huyu mkandarasi aweke lami kwanza, nyufa zitokeze halafu eti ndo udongo ukafanyiwe soil analysis?

    Halafu jamani huu mtindo wa kufuja kodi zetu kwa misululu ya magari maana yake nini? si wangechukua min bus moja wangeokoa pesa nyingi za serikali jamani, kwanini serikali yetu haiangalii kupunguza gharama zisizo za lazima?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...