Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),Leodigar Tenga (katikati) akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar es Salaam leo wakati wa Mkutano wa kumtambulisha kocha mpya wa Timu ya Taifa (Taifa Stars).Kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambao ni Wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa,George Kavishe na Kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),Angetile Osiah.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambao ni Wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),George Kavishe (katikati) akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani),jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),Leodigar Tenga na Kulia ni Kocha Mpya wa Timu hiyo ya Taifa,Kim Poulsen.
Kocha Mpya wa Timu ya Taifa,Kim Poulsen akizungumza baada ya kuteuliwa kuwa Kocha Mpya wa kuifundisha Timu ya Taifa leo.
Kim Poulsen ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania (Taifa Stars) kuanzia Mei 11 mwaka huu kuziba nafasi ya Jan Poulsen.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema Kim amepewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya Shirikisho kuamua kutomuongezea mkataba Jan. Mkataba wa Jan uliokuwa wa miaka miwili unamalizika Julai 30 mwaka huu.
Amesema kwa vile Taifa Stars inakabiliwa na mechi za mchujo za Kombe la Dunia raundi ya pili Kanda ya Afrika na mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN), TFF imeona ni lazima iwe na kocha mpya mapema kabla ya mkataba wa Jan kumalizika.
Kim ambaye ni raia wa Denmark amekuwa nchini kwa mwaka mmoja sasa akifundisha timu za Taifa za vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) na miaka 20 (Ngorongoro Heroes), hivyo anawafahamu vizuri wa wachezaji wa Tanzania.
TFF imeanza mchakato wa kutafuta kocha mwingine wa timu za vijana atakayeziba nafasi ya Kim. Ili kuwa na makocha wenye falsafa moja, kocha huyo anatafutwa kutoka Denmark.
Naye Kim ambaye Jumatatu (Mei 14 mwaka huu) atatangaza kikosi cha Taifa Stars ambacho Juni 2 mwaka huu kuivaa Ivory Coast katika mechi ya mashindano amesema yuko tayari kwa kazi hiyo na kusisitiza kuwepo ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali ili timu hiyo iweze kufanya vizuri.
Kwanini wawe na falsafa moja tena ya DENMARK,Kwani mpira utakaofundishwa ni wa falsafa ya nchi hiyo au ni wa falsafa ya dunia!
ReplyDeleteKwa hiyo falsafa ya nchi hiyo ikiwa mbaya ndo tumekwisha kabisaaaa!
Tafuteni walimu wanaofaa kutufundisha mpira si kutafuta falsafa ya nchi fulani.
Jamani sisi Watanzania mpaka lini tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu??!!umesikia wapi?coach kufanya kazi ndani ya kazi ya Mtu mwengine si vichekesho!!!! Kama coach kweli within a month anaweza kuipanga team na ikashinda ila ninavyofikiria mimi hawa macoach wanakuja kwetu kutengeneza cv zao wakifanikiwa sawa wasipofanikiwa sawa hawalose kitu au wachezaji wetu hawafundishiki ndio maana tunataka coach ndani ya coach.Ndugu Tenga katafute coach mwenye cv nzuri already usitubabaishe mpaka coach unakwenda kiudugu tena!!!!!!!
ReplyDeleteNilikuwa namuamini sana mzee tenga nikitegemea atainua soka ya bongo lakini naona naye ni walewale..unaleta kocha mpya aanze kazi kabla wa mwanzo hajaondoka?ataita wachezaji?sasa wa mwanzo atafanya nini mpaka mwisho wa mkataba hiyo july?au mmeamua kukatisha mkataba wake wakati bado mwezi na nusu uishe?
ReplyDeleteCHukuweni kocha kutoka HOLLAND wako kibao na wazuri na sio ghali kwani makocha wa kidachi raha zao wanakwambia ni mda gani ataiinuwa timu kwa kiwango fulani
ReplyDeletefuateni nchi nyingi sana wanawatafuta makocha wa kidachi na mpira wao unaukuta uko OK
NYINYI kila leo mnangangania denmark, au mnamkataba nao wakugawa pesa nusu kwa nusu
Hata na mimi nilikuwa na mategemeo makubwa na Tenga. Kumbe ni yale yale, mbona ni aibu na inasikitisha kuwa kiongozi wa biashara isiyoeleweka. Kwani ya kwetu TZ si yale yale, ya JK, na ya wengineo hayana tofauti na yale yaliyokuwa yakifanyika ktk nchi ya Abunwasi: Kusadikika. Yote yanaezekana ktk nchi yetu. Kwanini ujali kai yako unapokuwa umepata uwzo wa kujipatia kilicho chako??????.
ReplyDelete