Habari Ankal,
Naomba kuwasilisha taarifa hii ya kuwatahadharisha Watanzania juu ya wizi wa kupitia mtandao wa kusafirisha pesa kwa simu za mkononi unaoendelea nchini kwa kasi ya ajabu. Watu wengi wamelizwa. Na ukifika huko makao makuu ya kampuni husika mnajikuta mko wengi mnaolalamika.
Jana nimelizwa laki tano. Wezi wanatengeneza namba mbadala na kublock ya mwanzo, baadaye kuitawala na kutuma messeji ya amri/order kwa watu wako au wasaidizi ili watume pesa kwa mtu Fulani na kwamba ni haraka.
Message zinatumwa hivi;
Mwizi: Hapo kuna sh.ngapi nijibu nikuagize?.
Mwizi: Embu mtumie huyu jamaa laki 5 fanya haraka kidogo namba yake 0656685054 anaitwa Ricky halafu nijulishe.
Kama mtandao mbovu wa Tigo anasema- “Ngoja nikupe ya voda”
Ya voda 0769870813
Mwizi: Mbona unijulishi chochote fanya haraka anasafiri
Ujumbe wa Mtandao; G42UO138 Imethibitishwa Tsh500,000 imetumwa kwa JOEL MOSHA Tarehe 3/5/12 saa 12:48 PM Salio lako la M-Pesa ni Tsh4,300.Umeingia kwenye droo!
Ukifyuatilia *Pesa unaamiwa ameshazichukua tena kwa kutumia Mawakala wawili na ni hapa Dr es Salaam.
Wengine wanajifanya wako kwenye kikao cha harusi na hivyo pesa zinahitajika haraka.
Yaelekea kuna ushirikiano kati ya wezi na vijana waliopo kwenye mtandao. Kumbe mtu anaweza jifanya ametumwa kuchonga namba ya mtu baada ya kupoteza simu. Eti hapo anahitaji kutaja namba tatu za watu alowasiliana nao karibuni.
Sasa iweje hao agents wa mitandao wasihakiki vya kutosha kabla ya kubadilisha laini ya simu?. Nimefika makao makuu lakini nikaambulia hadithi tu zaidi ya kurudishiwa namaba yangu . Eti wizi wa mtandao uko kila mahali hata mabenki. Sielewi maana ya zoewzi la kusajili simu kwa kutumia picha.
Huu uzembe wa makampuni ya simu utatuliza wengi.
Richard.
Wafanyakazi tanzania hawajui maadili ya kazi hata siri zakazi wanazitowa ovyo hata siri za wake za watu na wanaume zawatu wanaziuza na ndio maana watu wanafumaniana sana ulaya kampuni inafungwa na inalipa mapesa mengi kwa kutowa siri za watu!
ReplyDeleteHawa watu wa makampuni inabidi washtakiwe kwasababu ni mbinu zao ama sivyo waache hiyo biashara watu waendelee kutumia mabank tu kama mtu ameibiwa kwanini msifuatilie kina ni nini? you have to take good care of your customers sasa kama kuna wizi katika mabank ndo nanyie mfungie macho hilo? thats total nonsense wizara husika ya mawasiliano mlifanyie kazi hili sio semina na kusafiri tu bila kuangalia wananchi wanaibiwa tu
ReplyDeleteRichard, tuliza boli,kwanza kabisa pole kwa yote na hongera kutupa huu ujumbe wa maana kabisa , hapana shaka makampuni yote ya simu yanaumiza kichwa sasa hivi kutaka kuupata undani wa majizi haya. Sasa wamefika mwisho, najua wazi kwamba hata Ulaya kuna ujanja kama huu hutumika ,yaani watu kujaribu kwenda ndani ya technolojia na kutibua mambo-lakini huwa hawaendi mbali sana, juzi juzi tu hapa Montreal Canada ,jamaa waliprint card za kutumia kwenye mabasi na train,million 2 ( card) feki na zikatumika bila wasi wsi-lakini shirika halikukaa kimya ,likaunda njia mbadala ya kuzitambua hizo Card na zilikamatwa nyingi tu, kwa hiyo Richard, Ufisadi siyo wa mawaziri tu, binadamu wote tuna uroho wa kuwa na maisha mazuri bila ya kuyafanyia kazi, huku Ulaya watu kama hawa wanapokamatwa ,hulipa mara tano zaidi ya walichoiba ,bongo ni hakuna hiyo ndo kwanza wanahamishiwa kitengo kingine.
ReplyDeleteSijaelewa! hapohapo, mjini shule pole
ReplyDeleteWizi uko kila mahali katika ngazi zote yaani mtu bnafsi hadi serikali. Sasa tatizi hapa Tanzania kwetu tunafuga na kulea wizi ndo maana umeshamiri. Labda Yesu akija atatukomboa sioni kama binadamu wa Kitanzania ataleta ukombozi. Kila nikiangalia naona wizi wizi kila mahali.
ReplyDeleteHii ndio changamoto ya Maendeleo, Teknolojia na Utandawazi !
ReplyDeleteRichard pole sana na hongera sana kwa kutoa taarifa hii kwa umma, na Ankal big up kwa blog hii.
ReplyDeleteUSHAURI; Richard peleka malalamiko rasmi TCRA na tume ya mlaji FCC iliopo Ubungo Plaza watashugulikia hii issue. Una haki ya kulipwa fedha zako na usumbufu uliopata wa kuwa blocked....
Usiliaachie hapo eti uizi upo kila mahali" au kuridhika na majibu yasiyo siluisha kosa la hii Company ya Simu.
Kila la heri na pole: Tupe taarifa kama FCC na TCRA wametatua kesi yako: Umma unaitaji kulindwa, na hizi kampuni zitakua makini zaidi....jasho la mtu lisipote hivi hivi tu
Richard pole sana na hongera sana kwa kutoa taarifa hii kwa umma, na Ankal big up kwa blog hii.
ReplyDeleteUSHAURI; Richard peleka malalamiko rasmi TCRA na tume ya mlaji FCC iliopo Ubungo Plaza watashugulikia hii issue. Una haki ya kulipwa fedha zako na usumbufu uliopata wa kuwa blocked....
Usiliaachie hapo eti uizi upo kila mahali" au kuridhika na majibu yasiyo siluisha kosa la hii Company ya Simu.
Kila la heri na pole: Tupe taarifa kama FCC na TCRA wametatua kesi yako: Umma unaitaji kulindwa, na hizi kampuni zitakua makini zaidi....jasho la mtu lisipote hivi hivi tu
Dawa ni kutotuma hizo PESA, We kwanini unatuma hata kama wamekutisha?
ReplyDeleteKama hawajui PIN yako PESA zako zipo salama hata kama watabadilisha line yako.
Nanyi makampuni ya simu mtu akija kuchonga LINE/CHIP basi achonge yake na alete kitambulisho na kamwe asichonge KWANIABA YA MTU MWINGINE.
Hio itasaidia
Lakini TIGO wamezidi... helpdesk / service desk yao hawapokei simu! sehemu za huduma kama mlimani city au barabara ya Nkrumah pamejaa sana. kwa ufupi huduma imewashinda! wa-outsource huduma zao ili kuongeza ubora na kupunguza au kuondoa wizi kabisa!
ReplyDeleteJamani hasa mtandao wa tigo,hovyo kabisa,na wafanyakazi wake nadhani wanashirikiana na wezi.Hallafu ukifika ofisini kwa tatizo hilo wala hawakupi majibu ya maana.Na ile system yao ya ku renew line vichochoroni ndio imeleta matatizo yote
ReplyDeleteTCRA wanajua na wamekaa kimya kwani ni WANUFAIKA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeletelakini pamoja na hayo inakuwaje unaambia mtumie mtu hela wakati ulikuwa huna mpango wa kumtumia?sio unaambiwa tuma hela wakati mtu alikuwa hakudai wala hamna miadi yoyote ya kutumiana hela ghafla tu mtu ankwambia tuma hela nawewe unakurupuka kutuma ni kama watu wanavyotapeliwa dhahabu feki unakutana na mtu mara hii dhahabu thamni yake ni sh.kadhaa wakati mimi tangu nizaliwe hatadhahabu sijawahi kuiona au jana,juzi au siku mbilizilizopita sina mpango wowote wa kufanya biashara ya dhahabu unatoa hela unanunua kioo cha chupa halafu eti wamenifanyia uchawi hakuna tafakari kwanza kabla ya kuamua kutenda ila pole mdau kwa yaliyokukuta na asante kwa kutu habarisha
ReplyDeleteTigo wamezidi sana ni mtandao mzuri lakini watendaji wake sio waaminifu,siku moja nilinunua vocha ya shilingi 2000 nilipokuwa ninaikwangua nikafuta namba moja nilijitahidi kuihisi nikashindwa jamaa yangu akaniambia maadam serial namba ipo wapigie customer services watakusaidia nilipiga mara zote hawa jamaa hawapokei,mwisho nikaenda center yao mojawapo mjini nikawaelezea kila kitu wakanipa form moja nikaijaza wakaniambia baada ya wiki mbili watanirushia vocha mpaka ninaandika hapa ni miezi 9 hakuna kitu,tatizo ina wafanyakazi wana njaa iliyopitiliza,kwahasira nikahama mtandao kwasasa nipo vodacom na Airtel
ReplyDeleteacha namie nikupe no. yangu unitumie mihela.kumbe ukiambiwa tuma unatuma! lakina kuna miandao mingine wakali kweli kurenew line bila ya valid ID. jaribu kwenda voda-Mlimani walishanitoa barua tatizo lao ni wabahiri wana wahudumu wachache na foleni huwa ni ya kutisha.unaweza kukaa zaidi ya 2hrs. lingine,namba ya siri ndo hela yenyewe bwashee sasa ata akichukua line atatoaje hiyo mihela?!!!
ReplyDeleteNyinyi wadau munaong'ang'ania kutumia mtandao wa tigo, kwani mumelazimishwa na nani?
ReplyDeleteOndokeni na mukiwa wengi basi watajirekebisha au watakufa.
Huu ni ulimwengu wa ushindani.
Asante Ankal kwa BANGO! Hili ni Jukwaa la Watu la ukweli.
ReplyDeleteWadau niwashukuru kwa michango yenu. Ushauri wenu wa kwenda FCC au TCRA nitazingatia na nitarudi kuwapa Feedback. Hata hivyo kuna ambao hawakuelewa mada kabisa wakachangia ju ju na kupotosha, Nimeelewa kwanini watu wanapata ZERO/ DiV IV DARASANI. Thanks ALL.
Mazingira.