Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Linah Sanga akiwa jukwaani akiimba moja ya nyimbo zake katika shoo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Cafe Rendez-vous jijini Oakland California,Marekani.
Linah akiwachengua mashabiki wake katika ukumbi wa Cafe Rendez-vous jijini Oakland California
Lina katika picha ya pamoja na shabiki wake aliyejulikana kwa jina moja Teddy
Linah akipozi ndani ya Hammer mara baada ya kumaliza show yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2012

    AH inamaana show hii ilikua nyumbani kwa mtu ?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2012

    haa haaa haaa jamani kweli wabongo kwa uzushi eti akiwa na mashabiki wake wakati hapo ni sebuleni tu panaonekana wala sio ukumbi,si bora arudi tu aje dar live jamani haya mambo ya kishamba sana eti uko nje unafanya shoo sebuleni au uani kw watu yuache ujinga

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2012

    Lina utaharibikiwa sasa hivi; ipende nchi yako, ipende jadi yako wamarekani wangependa na kufurahi kukuona ukiwa ki-afrika zaidi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2012

    Wasanii wa kibongo ni waongo wanadanganya kuwa wanakwenda kutumbuiza mtoni kumbe wanakwenda kutumbuiza kwenye nyumba za watu au kwenye pub za waafrika ambazo hata azijulikani.
    Tatizo wasanii wa nyumbani kuimba kwa kiswahili akutawafikisha kwenye anga za kimataifa labda kwa afrika njia nzuri ni vizuri muuanze kujifunza kuimba kwa kiingereza kama kweli mnataka masoko ya kimataifa, zaidi ya hapo mtabakia kuimba kwenye pub huku ulaya. Jaribuni kubadilika ili muuweze kupata mapromota wa kimataifa na muweze kutumbuiza kumbizenye hadhi.
    Pole dada Lina kwa kutumbuiza sembuleni.
    Mdau UK

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2012

    Mdau unayesema ni lazima wasanii wetu waimbe kiingereza wala sio kweli, jana Diamond kapiga bonge la show kwa kiswahili ndani ya BBA na watu wakaburudika, kuna nyimbo za kihindi, kifaransa, kizulu na lugha nyingine kibao watu hatuelewi kinachoimbwa ila ngoma inakubalika, sipingi wasiimbe kiingereza ila napinga wewe kusema ni lazima waimbe kiingereza kwa wao kukubalika hilo hapana hata kwa kiswahili watakubalika tu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2012

    Waandaaji wa show angaliaeni mnawatia aibu wasanii wetu ni bora mkafanya nao projekt nyingine kuliko kulazimisha show zisizoeleweka.
    Si bora kufanya show Dar live kuliko kufanya show nyumbani kwa mtu kisa nje.Show za nyumbani siku hizi zipo bomba na msanii anaeshimika.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 30, 2012

    wadau msifanye hivyo, tupendane jamani amnataka awe Dar live kila siku? hata kama msanii anaitwa na familia ya juu kama inamlipa aende kibongo bongo hamna ucelebrate. celebrate anaishi uswazi, isitoshe watanzania wachache sana wananunua kazi original. mnyonge mnyongeni jamani lakini haki yake mpeni. Much respect Linah.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 16, 2012

    WABONGO wacheni hizo,kama analipwa hata ikiwa chooni imba simjui huyu dem lakini wabongo mnapenda kuua sana,ukiwa na mahela star yoyote anaweza kuja living room yako kuimba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...