Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu akiwa Mahakamani mapena leo wakati alipofika kusikiliza mashtaka yake yanayomkabili kuhusiana na tuhuma za mauaji ya msanii mwenzake,Marehemu Steven Kanumba
 Lulu akiwa mahakamani hapo.
Lulu akiwasili Mahakamani hapo.

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu.

Jaji Fauz Twaib leo alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali kuhusiana na maombi ya mawakili wanaomtetea Lulu waliyowasilisha mahakamani hapo kuiomba korti hiyo aidha ichunguze umri wa Lulu anayedai ana miaka 17 au iamuru mahakama ya kisutu kuchunguza.

Baada ya kuwasilishwa maombi hayo leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi mahakamani ambapo wakili Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali maombi hayo kuwepo mahakamani hapo akidai kuwa hayakustahili kuwepo na badala yake yatupwe.

Alidai walichofanya ni kinyume cha sheria ilipaswa wakate rufaa kwasababu maombi yalishafika mahakama ya kisutu inakosikilizwa kesi hiyo na kutolewa maamuzi hivyo haikuwa sahihi kufungua maombi mapya wakati sio maombi mapya.

Aliwashauri mawakili wa Lulu aidha kukata rufaa maamuzi ya Kisutu au kuomba maamuzi yale kufanyiwa mapitio. Hata hivyo alidai kifungu cha sheria kilichotumika kuwasilisha maombi hayo sio sahihi ilipaswa kitumike kifungu ambacho kitaipa mamlaka korti hiyo kusikiliza maombi.

Mawakili wa Lulu, Furgence Masawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama hawakukubaliana na hayo,ambapo Fungamtama aliiomba mahakama kupokea maombi yao na kutolea uamuzi kwasababu ndiko maombi yao yanakotakiwa kupelekwa.

Aliusoma upya uamuzi uliotolewa Kisutu na kudai kuwa haukuwa uamuzi bali maelekezo ya mahakama na wao wamefata maamuzi hayo yaliyowataka kuwasilisha maombi yoyote Mahakama Kuu kwasababu mahakama ile haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.

Baada ya kusikiliza mabishano hayo ya kisheria mahakama hiyo imepanga kutoa maamuzi Juni 16 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2012

    kibinadamu amehuzunika na kifo za mtanzania mwenzetu Marehemu Steve Kanumba, bali wengi wetu tunaamini kuwa sheria itamwondoa matatani Elizabeth Michael (Lulu). Katika fikra za busara hakukusudia kuua. Tunaamini system yetu ya mahakama itakuwa makini kuamua kesi hii. Mungu ailaze pema roho ya Marehemu Kanumba pia ampe ujasili Ms. Elizabeth

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2012

    Kila binadamu amehuzunika na kifo cha mtanzania mwenzetu Marehemu Steve Kanumba, bali wengi wetu tunaamini kuwa sheria itamwondoa matatani Elizabeth Michael (Lulu). Katika fikra za busara hakukusudia kuua. Tunaamini system yetu ya mahakama itakuwa makini kuamua kesi hii. Mungu ailaze pema roho ya Marehemu Kanumba pia ampe ujasili Ms. Elizabeth

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2012

    kumbe jumamosi wanasikiliza kesi

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 28, 2012

    hio yote geresha watu tu huyu mtu yuko huru zamani sana, hata hio vaa yake tunaiyona wewe jela gani bongo unakuwa kama unaenda ofisini hii inakuwa ni ulaya sasa

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 29, 2012

    jamani ni juni 11 sio 16,mungu atakusaidia lulu kila lililo na mwanzo mwisho pia upo mdogo wangu usijali.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2012

    masikini huyu binti , poleni sana wazazi wa pande zote mbili, angalieni mawakili wasiwafilisi tu ,maana mnawezwa kufanywa dili , sisi binadamu tunapita tu,kama hadi Ditopele alishinda kesi . Basi Mungu tu ndiye hakimu wa kweli .Hao mawakili wote gelesha tu .ukweli upo wazi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 29, 2012

    mbona mtoto wa babu sea alikuwa na miaka 17 na kesi yake ilisikilizwa kama mtu mzima?? au ndo upendeleo??? what so special for Eliza (Lulu) haki ifanyike kama wengine sio kupindisha sheria. kama vp msitutangazie habari hizo cos itakera tukisikia yuko huru huyo lulu

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2012

    Kama LULU ana umri chini ya 18 ina maana Kanumba alikuwa anabaka na Lulu alijitetea. Kesi imeishia hapo

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 29, 2012

    huyu bado si mfungwa, yeye ni mtuhumiwa. Watanania bado mna mengi ya kusoma wote mnaowaona wanakuja mahakamani hawaingii na nguo za jela, nyie mnaona katika movie na TV huko nje wanapelekwa na nguo za orange. He jamani wadogo zangu someni muelewi sio kudesa tu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2012

    Mchangiaji wa 10:57.00 usipotoshe jamii. Kuvaa vizuri kwa mtu aliye mahabusu inategemea na matunzo ya ndugu na wazazi wake kuwa wanaenda kila mara kumpelekea nguo na chakula kizuri. wanaokuja wananuka mahakamani ni waliosahauliwa kabisa na ndugu na jamaa zao.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 29, 2012

    LULU POLE SANA HUKUUWA LAKINI SHERIA LAZIMA ICHUKUE MKONDO WAKE. NA TUNAOMBA MAWAKILI WAKO WAIFANYIE KESI HII KWA MAKINI.MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA KANUMBA. AMINA

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2012

    Ijapokuwa wote tulihuzunishwa na kifo cha ndugu yetu Kanumba, nawaomba Watanzania tuache Mahakama ifanye kazi yake. Ripoti ya post-mortem ya Muhumbili inaeleza wazi kuwa marehemu alikufa kwa mtikisiko wa ubongo kichogoni na wala hakuwa na alama ya kuumia au kukwaruzwa popote mwilini. Aidha, kuna taarifa ya uchunguzi wa damu ya marehemu ambayo itawasilishwa kortini. Hatujui inasemaje. Mungu pekee ndiye anayejua ukweli. Mimi binafsi SIAMINI kabisa kuwa eti Lulu aliua kwa kukusudia.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 29, 2012

    anony wa tatu kama mtu hujahukumiwa unavaa nguo za nyumbani pia ruhusa ndugu zako kukuletea msosi na nguo ila ukihukumiwa na kufungwa ndo unaanza kuvaa nguo za jela.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 29, 2012

    Kumbe kweli alikuwa na mimba na imetoka, maana sasa tumbo limeisha kabisa ! loh! haka katoto ! kanastahili kufunzwa adabu

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 29, 2012

    we anony hapo juu ulitaka avae nini? acha mambo yako wewe .faham kua bado yeye sio mfungwa yupotu rumande huku kesi yake ikiendelea.akipatikana na kosa ndio atafungwa na atavaa kama mfungwa,then lamda utafurahi

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 29, 2012

    Kama serikali imeweza kuanzisha Huduma ya basi la magereza kwa watuhumiwa kwa kuwafikisha mahakamani na kuwarejesha rumande au huko jela , nadhani pia ingalifaa kuanzisha huduma ya mavazi kwa mutuhumiwa ili waendane sawa na watuhumiwa wengine hii itasaidia sana kiusalama au hata kuondo huu mjadala wa mavazi ya LULU Elizabeth.

    Ncni nyingi zinafanya mpango huu kwa hivyo sio geni duniani. Vumilia Lulu kwani wewe ni wa thamani kwa wazee wako na wakupendao kesi itaisha ipo siku tu. One day yes

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...