Mh. Zitto Z. Kabwe |
Juhudi za kurejesha misingi ya uwajibikaji katika utumishi wa umma zimeanza kuzaa matunda Baada ya Rais kutekeleza shinikizo la Bunge la kuwafukuza kazi baadhi ya Mawaziri ambao Wizara zao zimetuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma, rushwa na utendaji mbovu. Mawaziri 6 wamefukuzwa kazi baada ya kugoma kujiuzulu wao wenyewe, manaibu Waziri 2 wamefukuzwa pia.
Ndugu George Mkuchika alitakiwa kujiuzulu, akajiuzulu lakini Rais amemrudisha kwenye Baraza Kama Waziri wa Utawala Bora. Yeye nampongeza kwani hakuwa na makuu ya kuanza kujitetea Kama wengine. Atakuwa ametoa funzo kwa wenzake.
Kwa kawaida wateule hufanya sherehe kwa kuteuliwa kwao. Nitawashangaa watakaofanya sherehe safari hii kwani hakuna cha kufurahia. Nitawashangaa Watakaokwenda kuapa na Maua kwa furaha kwani furaha itakuwa ya muda mfupi tu. Mkutano wa Bunge wa Bajeti ni mwezi ujao tu na Wateule wote watakuwa kikaangoni. Too short honeymoon.
Hakuna cha kusherehekea kwa sababu nchi in changamoto nyingi sana. Changamoto ya kuzalisha umeme wa kutosha na kuusambaza kwa wananchi wengi, changamoto ya kukuza uchumi wa vijijini na kukuza uzalishaji viwandani ili kutengeneza ajira kwa vijana, changamoto ya kuongeza mapato ya Utalii kutoka katika hifadhi zetu na kuvutia watalii zaidi katika nchi yetu.
Nimewapigia simu wateule wengi na kuwaambia, siwapi pongezi Bali nawatakia kazi njema. Nawatakia uwajibikaji mwema. Uwajibikaji ndio msingi wa kupambana na rushwa, uvivu na uzembe.
Kwa Waziri wa Fedha, ambaye mimi ni Waziri Kivuli wake (Kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni hataniwajibisha pia), namwambia uteuzi wake ni changamoto kubwa sana katika maisha yake.
Hivi sasa eneo lenye Bajeti kubwa kuliko zote nchini ni huduma kwa Deni la Taifa (services to national debt). Lazima kuangalia upya Deni la Taifa. Hivi sasa Deni la Taifa ukijumlisha na Dhamana za Serikali (government guarantees) limefikia tshs 22trn mpaka Desemba 2011.
Nimewahi kutaka ukaguzi Maalumu katika 'account' ya Deni la Taifa. Linarejea wigo huu. Tunalipa takribani 1.9trn tshs kwa mwaka kuhudumia Deni la Taifa. Zaidi ya Bajeti ya miumbombinu, Afya, Maji, Umeme nk.
Mfumuko wa Bei, misamaha ya kodi na kodi zinazozuia watanzania kujiajiri ni changamoto kubwa sana Wizara ya Fedha lazima ihangaike nayo.
Usimamizi wa Mashirika ya Umma kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina na hasa usimamizi wa Hisa za Serikali katika kampuni binafsi ni masuala yanayohitaji masuluhisho sasa na sio baadaye.
Kwa Mwalimu wangu dkt. Mwakyembe, utakumbukwa kwa Jambo moja tu. RELI. 'make Railways system work'. Hutakuwa na 'legacy' nyingine isipokuwa Reli maaana Bandari bila Reli ni sawa na Bure.
Tunatumia zaidi ya tshs 300bn kwa mwaka kukarabati barabara wakati tunahitaji tshs 200bn kukarabati Reli iweze kusafirisha mzigo kwenda Bandarini na kukupa Bandarini.
Ndio maana nasema hakuna Jambo la kusherehekea maana wajibu mliopewa na Rais ni mtihani mkubwa kwenu katika kukitumikia Taifa letu. Msipowajibika, mtakumbwa na fagio la chuma!
Mkisha kula kiapo, kimbieni kazini. Nothing to celebrate. Hit the ground running.
--
Zitto Z. Kabwe.
Dar-es-Salaam
Jumamosi, Mei 5 2012
waambie kaka....kama washapanga mbinu nyingine za kula baada ya uteuzi wao wakae wakijua wabunge wetu wapo macho na hadaa zozote dhidi ya rasilimali za taifa letu. wapinzani kazeni buti bungeni hadi mafisadi wajitambue kilichowapeleka sio kushibisha matumbo yao!
ReplyDeleteNi kweli kabisa, hakuna sababu ya Sherehe !
ReplyDeleteNi wazi kabisa Mawaziri waliotumuliwa wametuangusha sana Wananchi wote pia wamewagharimu na kuwafedhehesha saana Mhe. Raisi JK pamoja na Mtoto wa Mkulima Mhe.Pinda !
Kwa mtaji huo ni sawa Mhe.Zitto Kabwe akiwashauri kuwa wasisherehekee bali kazi kubwa ipo mbele yao!
BIG UP MH.ZITTO KABWE.
ReplyDeleteKwa nini Wezi waliotimuliwa wasichangie upungufu huu wa mahitaji wa fedha hizi Shs. 22 Trillioni?
ReplyDeleteNi kiasi cha kuchukua calculator na kuchapa wizi waliofanya halafu tunajazia jazia hapo maana Shs. 22 Trillioni sio mchezo kuzilipa,,,au sio?
Wakishindwa wajue chadema wanapewa nchi na kazi kwenu..
ReplyDeleteKuwashauri mawaziri wasifanye sherehe ni sawa,lakini kwenye demokrasia Kila Mtu anao uhuru wa kufanya anachokotaka kwa muda wake binafsi.
ReplyDeleteNi maoni yang tu.
Nakuunga mkono Zitto. Kufanya sherehe baada ya kuteuliwa kuwa waziri, tafsiri yake ni kwamba "umeula". Sherehe hufanywa kwa kujipongeza kwa achievement flani uliyofikia. Kupewa uwaziri si achievement bali ni kupewa jukumu zito la kuwatumikia watanzania. Dr.Magufuli, Dr.Mwakyembe, Dr.Mgimbwa, Kagasheki na Prof. Muhongo mmeshikilia wizara nyeti mno kwa maendeleo ya nchi yetu. Tunawategemea msituangushe
ReplyDeleteWakaribishe hao 'FORM ONE' Bw.Kabwe.Nyongeza kidogo tu-Katiba mpya kwa nini isibadili uwaziri ukawa kazi ya kuomba kwa kutumia CV/Résumé badala huu mtindo wa sasa wa kuteuliwa na mkuu?Watu wengi sana humu jana walitoa maoni ya kuulizia CV za wateule wapya(Bahadhi yetu hatukuwaelewa).Siyo rahisi,rais kuwafahamu Watanzania wote.Ndiyo maana imechukua miaka karibu miaka 20 rais kumspot Prof.Muhongo
ReplyDeleteDavid V
Ahsante Kabwe Zitto kwa ushauri wako kwa mawaziri wateule.Kweli watu cha muhimu ni kazi za wananchi na maendeleo.
ReplyDeleteLakini sidhani kama kusherehekea kunaharibu utendaji wa mtu.Kufurahai jambo jema au mafanikio siono kama ni dhambi.Hata waheshimiwa wabunge pamoja na mhe,Kabwe mwenyewe walisherehekea ushindi wao pamaoja nao walijua kuwa kushinda ni kwenda kazini.
Tusiwatishe wateule kwa hilo,wache washerehekee wanaopenda ,sisi letu si vitisho vya kuzuia sherehe bali tuangalie utendaji wao.Wakiharibu nao waondoke.
Lakini Kabwe na wabunge wote mantenga fedha za kutosha na kuelekeza vipau mbele kwa mawaziri mnaowapo kazi hizo na zenye gharama kubwa?Au manaangalia tu kwa nini hukufanya au hukutekeleza hata kama bajeti finyu kufanya yote!Wapeni vapau mbele basi hukohuko bungeni.
Kwa nini maji na umeme kiala mwak kaial siku havikamiliki?Haya yote ni kosa la waziri kweli!Nadhani kuna kitu hakijapangika hapa.Hakuna mpango mahsusi wa serikali au niseme Bunge.Si waziri tu ni Bunge.Vipaumbele katika matatuizo ya kudumu.
Tuatafukuzana kila siku na hakuna atayeweza kama hakuna vipaumbele au bajeti maalumu kwa maji na umeme.Foleni hadi lini! Kweli hakuna njia?Hii mabasi ya mwendo wa kasi zoezi ni slow mno mno.Majiji na miji yetu majumab mazuri mno,lakini foleni na misongamano vyaondoa uzuri wake miji hiyo.
Wabunifu na watendaji wasaidieni wasiwekewe vikwazo vya kutafuta sifa tu.Hapo wabunge tusaidieni jamani.Wenzetu wanapiga hatua sana sisi siasa zimezidi mno.Fedha tunazo sana wala sio siosiri tujenge mikakati tu.
Waheshimiwa tuko pamoja.Wanao kula vya umma warudihe tu hata kuwafunga haitusadii sisi kwani shida yetu ni fedha za umma.
Hongera mhe JK kwa uteuzi,lakini tusiwahukumu bila ushahidi,na ushahidi ukiwepo warudishe fedha za umma.
Barabara za Magufuri weka vivuko watu wanagongwa sana.Hauoni ulaya na kila siku mnakuja huku.Vivuko gharama gani?
Mhe. Zito si vyema kuprempt shughuli za Waziri mpya. Kila jambo lina utaratibu wake. Mimi ninaamini hilo deni linahitaji collective effort ya Serikali kwa ujumla na kuangalia namna ya kupunguza matumizi na kuongeza mapato. Ninauhakika hate wewe ungepewa hiyo Wizara basi usingeweza kuleta maajabu. Ni vyema ikaeleweka kwamba kusema na hali halisi ni vitu viwili tofauti. Zito umekuwa kama mwalimu wa kila kitu. Ninakuhakikishia kwamba mfumuko wa bei haudhibitiwi kwa kalamu na karatasi bali kwa sera endelevu ambazo zinalenga sekta za fedha na uzalishaji wa uchumi bora. Mimi si msomi ila nina mashaka makubwa na mitazamo yako ya kujiona unaweza kuleta wonders. Ninachokioona ni nchi kukosa viongozi waadilifu na wakweli na hii inatokana na mfumo wetu mzima wa kupata uongozi wa nchi. Viongozi wengi wanatumia fedha nyingi kupata uongozi Matokeo yake akili na nfsi zao wakipata nafasi huelekezwa katika kuona namna ya kurudisha gharama zao. Kukemea na kupiga vita ubadhirifu wa mali za uma ni jambo jema sana. Hilo halina mjadala lakini nchi yetu ina matatizo sugu ya mitazamo na usimamizi. leo tujiulize Air Tanzania kuanguka Kigoma Zito umesema nini kuhusu uwanja wenu wa ndege kule. Uwanja wa ndege wa Mwanza kujaa maji sikumsikia hata Mbunge mmoja kulisemea hili licha ya maji kujaa hadi kwenye mashine ya kuscreen mizigo na abiria. Umeme huo zogo lake tunalijua sote kwamba haya makampuni yamepewa tenda uko wapi umeme sasa tunaambiwa kwamba miundo mbinu mibovu. Kwa ufupi Unilateral action pekee haitoshi tuwakwamue wananchi wetu na taifa kwa viongozi kuwa wakweli na wadilifu na sio kuanzan kuwaambia cha kufanya wao ni watu wazima na Rais amewachaguwa na si vizuri kumwambia mtu asifurahie kuchaguliwa kwake hio ni haki na ya kufurahia au vinginevyo.
ReplyDeleteMH. ZITTO, SASA UTAKUWA UNAWATISHA SANA HAWA VIONGOZI WAPYA! LAZIMA WAPEWE HATA MAUA NA WANAFAMILIA WAO IKIWA PAMOJA NA SHEREHE YA KUWAPONGEZA KWA KUTEULIWA KWAO.
ReplyDeleteUKIKARIBISHWA KWA HIYO SHEREHE NDIO UKAWAELEZE HAYO UNAYOYASEMA SASA. LAZIMA KILA JAMBO LIFUANYIKE KWA UTARATIBU. TUNAKUONA KWA MTANDAO HATA UKIALIKWA KWA B'DAY PARTY NA UNAKWENDA KUSHEREKEA, KWANINI HUYU WAZIRI ALIYECHAGULIWA ASISHEREKEE KUTEULIWA KWAKE KWANZA NDO MAMBO MENGINE YAKAFUATA?
Tanzania inakushukuru kwa ujasiri wako Mh. Mbunge Kabwe. Tanzania inahitaji wabunge 30 tu kama wewe. Wawe wa Upinzani, CCM au upande wote mbili wenye damu ya "Tanzania nakupenda kwa moyo wangu wote na nitakulinda kwa nguvu zangu zote na waporaji wa ndani na nje wa fedha na rasirimali za umma". Muda wa watanzania kuwaangalia watu wachache wanaiteketeza (wreck) nchi umekwisha. Kabwe tumia uwezo wako uliopewa na mungu kuwaelimisha wabunge wengine nchi yetu ianze kubadilika kimaendeleo. Watanzania wanakushukuru kwa kazi nzuri sana bungeni, usije ukabadilika baadaye ukatusaliti.
ReplyDeleteSafi Kabwe. Namkubali mdau hapo juu katiba iangalie sheria ya kuwachukulia wafisaidi! Sio kuiba na kuondoka. Yaani akibainika mwizi ataifishiwe mali na kisha afutwe kazi na utumishi! Kwa nini Watanzania tunajifugia umasikini na matatizo!
ReplyDeleteHebu tuamke ziwekwe sheria thabiti kwa wala rushwa na hao mafisadi.
Karibu.
ReplyDeleteKabwe Kabwe sawa ,lakini usizidi mipaka bwana,yaaani mtu kusherekea uteuzi nako kunaharibu utendaji wa kazi kweli!!! Acha vitisho kwa wateule.Hata watu wakihitimu shahada husherehekea bwana.
ReplyDeleteSisi tuangalie utendaji ndo kipimo,wakishindwa tuwaondoe.Lakini tusiwapime kabla ya kazi wala tusiwapime kwa cv zao.
Cv sio kipimo cha utendaji uliotukuka,huo ni ubora wa masomo lakini si ubora wa kazi.Maprofessor wangapi wameshindwa,madokta wangapi wameshindwa.Tumpe mtu kazi na tusubiri afanye kwanza.
Sasa hivi kila mtu kwetu ataka kuwa daktari wa falsafa,lakini mbona hata katika walionondlewa kuna madaktari?
Wabunge wenyewe na bajeti zao wajenge mikakati ya kufanya kazi na vipaumbele kuliko kusubiri kuwalaumu watu na kuwatimua.
Upuuzi wako Zitto kwani kusherehekea mafanikio kunahusianaje na uwajibikaji kazini?Mbona hata ukifaulu mtihani unafurahia na kusherehekea?mbona ukijaaliwa mtoto unafurahi na kushangilia?mbona ukioa unafanyiwa arusi kubwa na kuzawadiwa,kwani ya mbele yanahusianaje na sherehe hizo?Kwa kuwa unasifiwa basi hata uozo unatuletea hapa au ulitaka upewe wewe huo uwaziri?Halafu umeniudhi unappomtanguliza Dr mwakyembe kwa kile unachoona wewe ndio cha msingi kwani wewe ndio wizara? Kaoe kwanza ili tujue kama kweli una hekima ya kutosha.
ReplyDeleteZitto unawaambia Mawaziri wakafanye kazi wewe kama nani wao?
ReplyDeleteThose of you who question Zitto for airing his views as to what authority does he have, shows how you lack political maturity.
ReplyDeleteOne thing you all fail to understand is that, its your money that these people are stealing and thus anyone can question them on how they appropriate the funds. Which money?? As long as you pay taxes, then its that same money they deduct from your salary with the promise of building you roads, better schools, power and water etc, which unfortunately most of those whom we have elected to allocate our money to better use have been to busy using it for their own means.
So again those who question as to what authority Zitto has to question the ministers I can only conclude to think before you act for its embarrassing to see in this generation people still view public officers as semi-Gods who can do whatever they want with our money. Whose money again?????
Homer
viongozi wote wangekuwa na mawazo kama ya huyu mtu basi tungekuwa mbali sana badala ya kufanya maigizo kwenye maofisi yao
ReplyDeleteZitto punguza sifa na ulevi wa madaraka. Wewe ni kama nani kuwaambia mawaziri nendeni mkawajibike! wewe ndiye uliyewateua?
ReplyDeleteAnoni wa sun may 6, 07.08am umeuliza swali la ajabu sana ambalo sikulitegemea kulisikia katika hii karne ya 21 unawaambia wakafanye kazi wewe ni nani wao? Kwani hujui hawa viongozi wako kwaajili ya kila raia hata wewe una haki ya kuwaambia wakafanye kazi kazi ya Uwaziri siyo sawa sawa na kazi ya ujuzi wowote ambapo boss wako atakuambia fanya hivi hii ni kazi ya kuwatumikia wananchi walio wachagua naomba ujaribu kusoma na politics za nchi za kidemokrasi kama ilivyo Tanzania. Mfano mzuri ni uchaguzi wa mameya nhini UK chama tawala kimepoteza viti vingi
ReplyDeleteWadau hayo ni mawazo yake naomba myaheshimu.asingeandika mngepata wapi muda wa kuchangia?kuoa sio kipimo cha busara ukweli ni kwamba mh zitto anaongea na anatoa mawazo mengi mazuri yenye faida kwa nchi yetu kuliko hayo machache yaliyowKwaza .ni bora alivyopreempt kuliko kukaa kimya then yasifanyike kama wameshindwa kufanya kwa muda wote basi zitto a
ReplyDeleteEwakumbusha ili wasisahau tena