Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh Freeman Mbowe   akiwahutubia wafuasi wa chama hicho leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa kampeni yao ya VUA GAMBA VAA GWANDA ambayo itazunguka mikoa yote ya Tanzania.
Katibu Mkuu  wa Taifa wa CHADEMA  Dr Wilbroad Slaa akiwahutubia wafuasi wa chama hicho katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa kampeni yao ya VUA GAMBA VAA GWANDA ambayo itazunguka mikoa yote ya Tanzania.
 Mbunge wa Ubungoi Mh John Mnyika akihutubia
 Mbungwe wa Kawe Mh Halima Mdee akihutubia Jangwani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2012

    Hongera chama tukufu cha CHADEMA, pia hao wazungu wapeni kadi,chama kilishakubalika hiki. Mungu ibariki Tanzania CCM hii ni lala salama yenu,jamani jitahidini kuwaondoa hao wala pesa za umma,sio mawaziri tu na wachini yake wengi wao wameoza kabisa, niliwahi kutoa taarifa ya mhasibu wa tannesco hapa makao makuu Ubungo,msukuma mmoja hivi, huyu jamaa anachota pesa kama vile atakufa kesho, jamani mtegeni na pesa za polisi. ni mimi wa Ndagalu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2012

    Yaani hadi wdhungu wapo?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2012

    Hao wazungu wanachama wa chadema?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2012

    Watu wamefika kwa wingi ili kujua hatma ya taifa letu la kaskazini, matokeo yake Mbowe anatuletea habari za utanzania.

    Lakini najua haya yote kayataka yule bwamdogo Nassari kutoa siri wakati jambo lenyewe bado 'premature'

    Tushachoka..!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 27, 2012

    Sasa hawa wazungu ni Chadema, au ndio mamluki, maana hawa wenzetu kwa kuzoa zoa, mradi waongeze idadi.

    ReplyDelete
  6. Che GuevaraMay 27, 2012

    People's Power ni kiboko wajameni! Ilikuwa ni shughuli jana japo niliangalia ktk ITV! hawa jamaa wamejipanga vilivyo na sasa wanatumia falsafa ya CCM ya vua GAMBA! CHADEMA wanasema 'VUA GAMBA VAA GWANDA!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 27, 2012

    CHADEMA mmejipanga bali kuweni macho na wanaotaka kujiunga ili kukichafua CHADEMA kama yule msema ovyo wa Maswa na jiulizeni mbona CCM walimchoka na walifurahi alipoondoka

    ReplyDelete
  8. Che GuavaraMay 27, 2012

    CHADEMA mlitoka wapi na Shibuda?anyway, ktk msafara wa MAMBA na KENGE wapo!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2012

    Sasa unashangaa nini kuona wazungu wao! Ndiyo wanaotaka hiyo M4C na pesa siyo tatizo, hasa kama unawekeza kwa uhakika. Mshaambiwa, Ikulu hakuna biashara labda kama ni kuiweka sokono nchi yenyewe.
    Chagueni, kwenda mbele wenyewe au kurudishwa nyuma, tena kwa support yenu wenyewe!
    Nilikuwepo

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 27, 2012

    Chama chochote makini kingekuwa na tahadhari kubwa san a kutanguliza wazungu. Ukombozi wa nchi yetu utaletwa na watu wetu wenyewe. Naogopa hao wazungu na naiogopa Chadema!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 27, 2012

    HAO WAZUNGU WAKO KAZINI, NGO NYINGI ZINALETA WATU WAKUANGALIA SISASA, UCHUMI ETC ZINAVYOENDELEA NCHI TOFAUTI. ANGALIA KWENYE RELIEFWEB WEBSITE WANATAFUTA WATU WA KAZI HIZI KILA SIKU, WAZUNGU WANAZICHUKUA NA KUJIFUNZA LUGHA YA WENYEJI KIDOGO INATOSHA! ILI MRADI UWE NA ELIMU NA EXPERIENCE YA KAZI ZA UCHUMI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...