Mstahiki meya wa Ilala Jerry Silaa akipata maelezo na vipeperushi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Greencity, Bw Peter Andrew wakati wa maonesho ya ALAT jijini Dar es salaam.Greencity ni kampuni inayojihusisha na uuzaji na usambazaji wa Vifaa na Mitambo ya kufanyia usafi mijini na Viwandani. Green City ambao miaka miwili iliyopita walingia nchini na Mitambo na Mashine za Kiitaliano mabazo kazi yake ni kufagia barabara na sehemu za wazi kama vile katika viwanja vya mpira viwanja vya ndege, migodini, mahotelini n.k Peter Andrew, mkurugenzi wa kampuni, anawahamasisha viongozi na wadau wote wa halmashauri za miji kushirikiana na kampuni hii ya Greencity ili kuweza kusafisha barabara zetu ambazo zinatugharimu mabilioni ya shilingi ili ziweze kudumu kwa muda mrefu. |
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali akiangalia maonesho katika banda la
Dkt Mohamed Ghalib Bilali akiagana na Bw Peter Andrew ambaye ni mmoja wa wajasiriamali wanaokuja juu kwa kasi nchini
saafi saana. Mtahiki Meya tuuze V8 basi tununue hizo!!
ReplyDeleteKazi ni nzuri isipokuwa matumizi ya mashine zaidi yanaongeza Ukosefu wa AJIRA !
ReplyDeleteKazi iliyotakiwa kufanywa na watu 15 sasa inafanywa na mashine moja na mtu 1 tu !
Sasa tusiokuwa na elimu tukale wapi?
yakweli unayoyasema kaka,je nije kwako,athari wanazozipata mabibi wanaosafisha mabarabara,maofisa wa traffic,watoto wanaoenda shule,maswaiba wa bodaboda,wanaoishi pembezoni mwa barabara,na wote wanao tumia barabara kwa ujumla,JE UNAZIFAHAMU????
ReplyDeleteBTW..utajiskiaje ukienda kula kwenye hoteli ambayo iko pembezoni mwa brbr? vp ugali na mchanga/vumbi.....