Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh Freeman Mbowe akiwahutubia wafuasi wa chama hicho leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa kampeni yao ya VUA GAMBA VAA GWANDA ambayo itazunguka mikoa yote ya Tanzania.
Katibu Mkuu wa Taifa wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa akiwahutubia wafuasi wa chama hicho katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam kwenye uzinduzi wa kampeni yao ya VUA GAMBA VAA GWANDA ambayo itazunguka mikoa yote ya Tanzania.
Mbunge wa Ubungoi Mh John Mnyika akihutubia
Mbungwe wa Kawe Mh Halima Mdee akihutubia Jangwani
Hongera chama tukufu cha CHADEMA, pia hao wazungu wapeni kadi,chama kilishakubalika hiki. Mungu ibariki Tanzania CCM hii ni lala salama yenu,jamani jitahidini kuwaondoa hao wala pesa za umma,sio mawaziri tu na wachini yake wengi wao wameoza kabisa, niliwahi kutoa taarifa ya mhasibu wa tannesco hapa makao makuu Ubungo,msukuma mmoja hivi, huyu jamaa anachota pesa kama vile atakufa kesho, jamani mtegeni na pesa za polisi. ni mimi wa Ndagalu.
ReplyDeleteYaani hadi wdhungu wapo?
ReplyDeleteHao wazungu wanachama wa chadema?
ReplyDeleteWatu wamefika kwa wingi ili kujua hatma ya taifa letu la kaskazini, matokeo yake Mbowe anatuletea habari za utanzania.
ReplyDeleteLakini najua haya yote kayataka yule bwamdogo Nassari kutoa siri wakati jambo lenyewe bado 'premature'
Tushachoka..!!
Sasa hawa wazungu ni Chadema, au ndio mamluki, maana hawa wenzetu kwa kuzoa zoa, mradi waongeze idadi.
ReplyDeletePeople's Power ni kiboko wajameni! Ilikuwa ni shughuli jana japo niliangalia ktk ITV! hawa jamaa wamejipanga vilivyo na sasa wanatumia falsafa ya CCM ya vua GAMBA! CHADEMA wanasema 'VUA GAMBA VAA GWANDA!!!
ReplyDeleteCHADEMA mmejipanga bali kuweni macho na wanaotaka kujiunga ili kukichafua CHADEMA kama yule msema ovyo wa Maswa na jiulizeni mbona CCM walimchoka na walifurahi alipoondoka
ReplyDeleteCHADEMA mlitoka wapi na Shibuda?anyway, ktk msafara wa MAMBA na KENGE wapo!
ReplyDeleteSasa unashangaa nini kuona wazungu wao! Ndiyo wanaotaka hiyo M4C na pesa siyo tatizo, hasa kama unawekeza kwa uhakika. Mshaambiwa, Ikulu hakuna biashara labda kama ni kuiweka sokono nchi yenyewe.
ReplyDeleteChagueni, kwenda mbele wenyewe au kurudishwa nyuma, tena kwa support yenu wenyewe!
Nilikuwepo
Chama chochote makini kingekuwa na tahadhari kubwa san a kutanguliza wazungu. Ukombozi wa nchi yetu utaletwa na watu wetu wenyewe. Naogopa hao wazungu na naiogopa Chadema!
ReplyDeleteHAO WAZUNGU WAKO KAZINI, NGO NYINGI ZINALETA WATU WAKUANGALIA SISASA, UCHUMI ETC ZINAVYOENDELEA NCHI TOFAUTI. ANGALIA KWENYE RELIEFWEB WEBSITE WANATAFUTA WATU WA KAZI HIZI KILA SIKU, WAZUNGU WANAZICHUKUA NA KUJIFUNZA LUGHA YA WENYEJI KIDOGO INATOSHA! ILI MRADI UWE NA ELIMU NA EXPERIENCE YA KAZI ZA UCHUMI.
ReplyDelete