Hi Ankal,
Pole sana na majukumu ya kila siku.Naomba tafadhali mie mdau wako wa Uk unitolee Utatanishi wangu!!!!
Mimi ni mwanamke wa Kitanzania, mwenye umri wa miaka 30, naishi UK kwa miaka zaidi ya 16, nafanya kazi, mkristo anaye abbudu sana Mambo ya Mungu, mtulivu, mkweli, situmii pombee ya aina yoyote, sina mtoto na wala sijawahi pata mimba. Nina urefu wa 165cm,60 Kg, mwenyeji wa Arusha na ninaongea lugha mbili tu English na Swahili. Nipo radhi kubadili mazingira ikiwa itabidi(Penzi kubwa halizui jambo!!!!!!!!!!!!!).
Mume nimtakaye anatakiwa awe na sifa sifuatavyo:
Mwanaume asiye chini ya miaka 35, mkristo, aishiye Europe lakini anatoka Tanzania kabila sio muafaka!, ajue malengo yake kimaisha na familia yake mpya!, awe anatambua haki na utu wa binadamu wengine(sio mbinafsi), awe na uzoefu wa kuvumiliana, kujadiliana ,kupanga na kukosoana kiwazi, sio mgomvi au mdanganyifu na awe na msimamo dhabiti na mimi kimaisha( No one night stand!!).
Awe na moyo wa kubadili mazingira yaani makazi(relocate), no show off man!!, katulia na anapenda maongezi ya ana kwa ana na wazi wazi na anayetzaka kuwa na watoto na kulea watoto wake pamoja nami!
Mwisho mwenye interest na mimi lazima anitumie majibu yake akiambatanisha picha yake, namba yake ya simu, email na sykpe name yake bila hivyo sitajibu au kwasiliana na naye. Hii ni Lazima na muhimu kwani wakati wa kuchezeana na kupoteza muda kwa classic love umepita na wakati! Now is I-Communication update!!!Nawatakiieni wadau wote Weekend njema na namsubiri nimtafutaye kwa hamu sana huku Europe!!!!!!!!!!
Majibu yote yaletwe moja kwa moja kwa email: chediel28@yahoo.com ,chediel28@yahoo.com,
Kwa stlye hiyo na kwa matakwa hayo uliyo yaandika na pia kwa kuwa unampenda MUNGU kwa dhati kubwa mweleze basi akutengenezee huyo mwanamme wako..kwani tangu mwanzo ulikuwa haujuwi kuchezeana ni kupotezeana muda?kwahiyo sasa ndio umejua?..ushauri wangu kwako ni kuwa sio lazima uolewe na mtanzania, maisha ni popote na sio lazima atokee ulaya mbona unapenda mtelemko?njoo nyumbani tuko wanaume safi tu ambao tuko tayari kukuoa.
ReplyDeleteVizuri Dada lakini kama kweli unataka mchumba kwa masharti kuwa lazima atume picha si ingekuwa vyema zaidi kama ungebandika picha yako tuione. Mie nipo Ulaya ningependa kupata mke mwenye sifa zako kama zako lakini siwezi kukuandikia bila kuona picha yako.
ReplyDeleteGabriel.
Nipo mamtoni, nina hamu ya muhogo wa kuchoma na chachandu halafu nishushie na kimpumu.
ReplyDeletenimefurahi kusikia kuna mtu mwenye sifa ninazozitaka.
ReplyDeleteTatizo nipo USA, je utanikubali. ninasifa zote ulizozitaja
Mdau USA
sasa mwenye shida ni nani?si wewe ! weka picha yako watu waone kwasababu wanaume wa siku hizi hawauziwa mbuzi kwenye gunia.Hizo zama zilishapita nakushauri weka picha yako wanaume wakusample kama unalipa au la!
ReplyDeleteBibie una elimu gani na unafanya kazi gani?
ReplyDeleteMdau mwenzio Europe
kjmalisa@hotmail.com
mama umesubiri hadi unazeeka ndio unashtuka? Nenda bongo kachukue serengeti boy mmoja umalize mambo. Good Luck!
ReplyDeleteInterview yako hakuna aliyewahi kufaulu duniani.Kwa mtajio huo huwezi kuapata wa kupatana na masharti yako.
ReplyDeleteMtu ajipime mwenyewe,na akuambie kuwa ndivo alivyo,sasa wewe utajuaje kuwa hivo ndivo alivo.Huko siko kuchezewa hadi uchakae ndo ugundue kuwa anakulaghai.
Hata Mungu haweki vipimo vyako,bora endelea kukaa peke yako kama ulivyozoea dada yangu maana mtihani wako hakuna anayeweza kufaulu.
wewe unadhani anayekunywa pombe hawezi kuwa mume mzuri?huo ni upotofu.
Vigezo mama yangu vitakutesana sana,na mume wa aina unyotaka hutompata,na yawezekena pia ndo maana umechelewa kujpata mume.
Ache vigezo muombe Mungu sana akuangazie.Hata mkulima ni mume usitake mtelemko wa kupata wa anina fulani.
mtu mkwema al;iomba kwa Mungu apewe hekima,akili na busara.Kmawe hakuomba utajiri au neema ya fedha na usomi.
Huh makubwa..!!
ReplyDeleteMie naona kama vile ulisahau kuset Aram yako ikuamshe vile maana naona umechelewa saana kuamka..!!
Well, kwa vile unaoneka wewe ni mtu wa kuoa na sio wa kuolewa, chukua huo ushauri wa kurudi home na kuoa, huku sisi wabeba mabox hautatuwezi, sie ni maplayboy bwana weweee...!!!.
Weka picha yako. Maana kwa msichana mzuri kidoogo si rahisi kukosa mwanamume UK. Na hivyo umeishi muda mrefu najua utakuwa una permit ya kuishi huko, labda kama unaishi ki-gorila. Kwa hiyo kamata kijana aliyejilipua ziku za karibuni. Funga naye ndoa. Sijuia sheria za huko zinasemaje. Lakini kwa nchi ninayoishi ukishafunga naye ndoa anapewa permit ya miaka miwili kwanza. Kwa muda huo utamchunguza. Ukimkubali, baada ya miaka miwili atapewa permanent permit.
ReplyDeleteSasa wewe kama una permanent permit, utakamata kijana, hata serengeti boys utapata huko huko UK. Hauna haja ya kwenda bongo
usitudanganye mapenzi gani bila kujua background ya mtu sifa za mtu hazitamkwi tu ni matendo we mbibi
ReplyDeleteMtu wa Mungu na tone hiyo, duh hapo umechemsha. Utadhani ni riafande rinataka kupigisha kwata. Unataka picha na skype mbona hukuweka picha na video yako kwanza ili watu wakuone. Ng'ambo wapo watu kibao na wote hakuna ambaye atakuwa tayari kuwa na mtu mwenye masharti kama yako labda tafuta taifa tofauti.
ReplyDeleteUTAISHIA KUDORORA MAANA USHA ANZA KUOTA MNVI HALAFU BADALA YA KUWA WA BEI RAHISI UNAKUJA NA SHERIA KALI KULIKO HATA ZA BEYONCE DADA NAKUAPIA MAMA YANGU MZAZI HUPATI MTU NANI ATAWEKA PICHA YAKE KWAKO WAKATI HAKUJUI? JE KAMA UNAKIPARA KAMA CHA MICHAEL JORDAN ITAKUWAJE? TOA MASHARTI WAKATI UNALIPA LAKINI KIPOFU KIPOFU UTA AMBULIA KAPA. HATA WA KU CHEAT HUTA PATA. POLE SANA DADA TUMA MAOMBI KWA WANIGERIA.
ReplyDeletekweli kabisa!!!!!!!!!!
Deletekweli kabisa!!!!!!!!!!
DeleteWewe Dada mimi nipo USA natafuta mke mwenye sifa hizohizo ulizotaja.Ila mimi sikubaliani na sharti la kutuma email kwako na kuambatanisha na picha na skype name kwa sababu hayo ndo ungeyafanya kwanza wewe ili kuonyesha uaminifu wako katika yale unayoyataka.Naamini kama ulivyojisemea sifa zako na zile unazotaka umpendaye awe nazo wewe uwe wa kwanza kuzitekeleza na ndipo utegemee kwa upande wa pili.Tafadhali weka picha yako hapo ili nami nikutumie yangu.Nisije nikatuma picha kwa mtu ambaye si ajabu anatisha usoni.Fanya kwanza wewe tuone ili tujimwage.Kila la heri.
ReplyDeleteuwezekano wa mwanaume kama huyo kuwa single ni mdogo sana so adjust urself else chukuwa kilichopo kifanye chako nakukipenda (respect ur differences if any)
ReplyDeleteTumapicha yako kwanza tukuone ndipo tusakamane. Unaonekana una makeke sana eti lazima mtu atume picha na skype name, wewe ya kwako iko wapi??
ReplyDeleteMdau wa Kwanza wacha kukufuru kuhusu Mwenyezimungu.
ReplyDeleteKila la heri mama naona umri ukizidi na fustration zinaongezeka.
ReplyDeletewabongo mkiwa nje mnajidaiiii ,etioh hivi vile ,mbona ki bibi ,sasa hivi bongo warembo miaka 16 ndio hao kina lulu washafanya mpaka wamechoka wewe 30 tena hapo umepunguza dah,tafuta kibabu cha kizungu,
ReplyDeleteau uje bongo na vijicent uzalishwe fasta ulee mwanao.
TUMA KWANZA WEWE HIZO PICHA!
ReplyDeleteKweli kumchinja Kobe timing,yale yale ya Mende kasogeza kabati,kula mdogo mdogo mamdogo umekua TBS shilika la viwango unatupima?haki za binadam zikowapi Kama mwendo wenyewe ndo vile unachagua,uvuvi haramu huo utavua pelege,nyumba inaungua hiyo mamdogo,mambo ya "sizitaki mbichi hizi" yashapitwa na wakati utaishia kuwa yule sungura kwenye kitabu cha hadithi shule za msingi miaka ile,kila la kheri Ma mdogo.
ReplyDeleteHuyu mdada jamani anashida. Nadhani ninamjua. Kama ni yeye, basi huwa tunaosha naye wazungu. Kama ni yeye. Ni mtu mwema tu, sema tu mi nilikwisha oa na nina furaha. Nadhani ushauri wa Serengeti boy ni wa maana kwake. Wengine wamebahatisha kwa staili hiyo, ingawaje wengi wao ndoa zinasuasua. Tunakuombea mdau. Mungu yupo!
ReplyDeleteUmri sio kitu, watu wanaolewa mpaka miaka 40. Mwacheni, mwanangu wanaume wa siku hizi si waoaji. Wanataka wakuchezee halafu ndio kwenu wapi. Kwa wengi ndoa hizi hazijadumu. Kama hujampata huyo mwanamme, si una kazi, maana ndicho muhimu, hicho kingine ni starehe tu. Lakini kazi ndio mume wa kwanza, huyo mwingine unaemdae ni wa pili. Tafuta namna nyingine, ulaya huko sio vigeni. Achana na hawa wachangiaje wa humu, watoto wetu wa kiume wanajifanya wanajua kumbe hawana wanaishia hivyo hivyo.
ReplyDeleteMm niko hapa bongo dsm nna miaka 33 na nna mpango wa kuchumpa majuu huko uk. kama unakubali kunifuga basi tuwacliane. nna kadigrii hivo hope nikapata kazi na tukaendesha life. mwaaahhh (kiss hilo lipokee basi mbona unaguna weye mrembo?).
ReplyDeletekubali hapa hapa jamvini haafu tutabadilishana mapicha na maimeil na maskypu.
Loverboy
Yaani wewe mdada baada ya kudoda sasa ndo unakumbuka mume? Pole. Nakushauri umeweke picha yako hapa na contacts zako. Haafu waweza kuja bongo ukachukua kijana ukaenda kumtunza akawa mume mzuri tu.
ReplyDeletekazi kwako.
mdau
pole dada mchumba ni majaaliwa na c lazima uwe naye ka una niya basi waswahili husema mchagua jembe si mkulima........na pia ingekuwa vyema ka ungeweza kuweka sura yako pia wakuone wadau na ka ni aibu basi atakaye kuwa interested fanya jitahidi ya kuweza kuonnyesha u seriously need a man in u'r lyf.....kila lakheli.
ReplyDeleteMdau....mchr.
mambo ya kupapatikia wanawake yamepitwa na wakati. wewe jieleze vizuri una unri gani? unafanya kazi gani? n.k.
ReplyDeleteVile vile hutafanikiwa kwa kutafuta bwana kwa vigezo vya makazi / mipaka (lazima awe Europe!!). Mapenzi hayana mipaka. Badili huu mweleleo wako la sivyo utaendelea kutapa tapa tu ma matapeli.We unafikiri watu wa maana na akili zao watatuma picha kwenye e mail ya mtu ambaye sina data za kutosha? NOPE. Kama we mwanaume je?
HIVI WEWE DADA KWELI HAMNAZO, KWELI UNAKAA ULAYA NA HUNA MWANAUME ANAEFANANA NA WEWE? BASI UNA KASORO KAMA UKISHINDWA WATANGAZIE MA NIGERIA KAMA HUJALI KWA SABABU MTANZANIA HUWEZI MPATA, AU NENDA JIWEKE KWENYE MITANDAO YA KI SWEDESH HUKO LAZIMA UTAPATA MWANAUME ANGALAU MWENYE UMRI WA MIAKA 75 NDIO WANAPENDA WANAWAKE WA KITANZANIA KAMA WEWE KWANI WAKO WENGI WALIOFANIKIWA KUPITIA HIVYO. HATA DADA YANGU MMOJA AMEFANIKIWA JUZI JUZI TU ! TUWEKEE BASI HATA PICHA PASSPORT SIZE TUKUONE AU UNA DOUBLE MWANYA? SASA SWALI NIKUULIZE KAMA UKIFANIKIWA KUMPATA NA AKAWA MSHINE NDIO HIVYO HAWEZI KITU AU MTAKUWA MNAKAA MNASALI TU KILA SIKU BILA NGONO? KILA LA KHERI , LAKINI WAULIZE WANAWAKE WA TANZANIA WAISHIO SWEDEN WATAKUSAIDIA SANA WAO WANAJUA SANA KUHUSU KUJIUZA KATIKA MITANDAO ALL THE BEST.
ReplyDeleteacheni hizo, UMRI wake wala si issue. Dada wasikutishe na umri, umri wako uko poa hasa karne hii sio yale mambo ya vijijini wanaolewa wakishapovunja ungu tu. we unaonekana umetafuta maisha kwanza na sasa uko tayari ku-settle. poa sana.
ReplyDeleteIla ushauri wangu ni kuwa jaribu kuwa humble, uwe tayari ku-compromise na wengine, ukitambua kuwa NO ONE IS PERFECT duniani, ati Yesu alisema.
Usiwe na masharti makali sana, maana wengi watakimbia, LOL.
WAKAKA EEH MBONA MMEKUJA JUU KAMA MOTO WA KIFUU?
ReplyDeleteMtumieni email na picha hata ya kutoa kwenye google kwani anawajua? Kisha na nyie muombeni picha yake kama analipa skype her umuone ukweli kweli kwani naye anaweza kukopy picha za mamodel akawatumia pia.
Kutaka mtu kwa umri huo sio kigezo cha kuwa yeye ni mbaya pengine keshatendwa huko nyuma sasa anaamua kurudi tena kwenye relations. Kwa mfano mimi nimekaa kwenye ndoa 20yrs sasa ila nimechooka kweli kweli nitabreak kidogo nipumzike kisha baada ya miaka 2 nilete tangazo langu kwa Michuzi ila mimi nitataka mtu ambaye ameshapitia machungu ya abused marriage ili tuliwazane!!
dada yangu usikate tamaa na maneno ya humu ndani yasiokichwa wala miguu
ReplyDeletewewe ni msichana mzuri wala usijali na yote uliyoyaandika uko sawa kabisa usiwasikilize wabongo hawana mpango, huu ni uwamuzi wako unataka mtu unayempenda na masharti yako ndio hayo uliyosema anaekutaka mwache akuandikie kwenye e mail yako usijali na mijineno ya watu
mungu atakupa mutakaofanana kiyote bora umekuwa mkweli kuwa unataka anaeishi hapa ulaya, achana kabisa na wabongo,
wapo wengi wanakupenda na kama utaweza kubalisha dini tu basi yuko mtu anakuhitajia wewe wakati wowote ule hapa hapa ulaya
mimi kama sijaowa ningekufuata tukamalizana wala bila ya matatizo yeyote dada yangu,
endelea na msimamo huo huo jiheshimu tu wewe ndio kitu kikubwa sana na usijali uko umri gani kama unajiheshimu utapata mume wewe wa maana sana tu
nitakuandikia kwenye e mail zaid dada kukutanisha na huyu mdau wa hapa ambae pengine munaweza kufikia makubaliano ya kiugwana
mwanaume mwenye sifa unazotaka hawezi kuwa single hadi awe above 35yrs. Wazungu wamekuchosha halafu unaleta jeuri na masharti ya kijinga. Inaonesha huwezi kuwa mke mwema. Pambana na wazungu ndo wanakufaa wewe.
ReplyDeleteSASA NYIE WACHANGIAJI TATIZO LENU NINI? YEYE ANATAUFUTA MUME, KWANI NYIE SHIDA YENU NINI? ANAEONA ANAWEZA HAYO MASHARITI YAKE NA ANATAFUTA MKE, NDIO HAPO PA KUANZA KOMMUNICATION, MSILETE ZENU ZA KIBONGONGO, NA STORY ZISIZO NNA MPANGO, MANAKE NAONA JINSI MLIVYO MSHOBOKEA DADAQ WA WATU, AU WENGI WAO NDIO ZILE ZA KUSHINDA KUTWA NZIMA KWENYE BENCHI NA KUSUGUA MATAKO. HAMAN HATA SHUGHULI ZA KUFANYA,
ReplyDeleteDada endelea na uzi huo huo. Wanaolalamika waache walalamike na wanaona sifa zako zinawafaa watakutafuta. Uzuri ulishaweka wazi ni nini unachotaka, wenye nia watajitokeza.
ReplyDeleteduuh.... dada unataka kuoa? tafuta mzungu au muhindi... utoe mahari.. mila na desturi za kiafrika mwanaume hutafuta mwenza wake. mambo yako yakufanya shopping... cjui.... umri umeenda kaza buti... chagua nazi huishia kupata koroma.
ReplyDeleteHABARI DADA, POLE MANENO YA WATU WALA YASIKUKATISHE TAMAA, MUNGU AMEKUANDALIA MUME MZURI TU ITAFIKA WAKATI UTAKUTANA NAE, UMRI WALA SIO TATIZO, MIAKA 30 MBONA MIDOGO SANA, WATU WANAOLEWA NA MIAKA 35 SEMBUSE WEWE,WEWE UNA VYOANGAIKA KUTAFUTA WAPO NA WATU WANATAFUTA HIVYOHIVYO, CHA MUHIMU NI KUMUOMBA MUNGU,
ReplyDeleteILA NAKUSHAURI KITU KIMOJA HIVYO VIGEZO ULIVYOTAJA HUWEZI PATA MWANAUME, MWANAMKE NDIYE ANAYEMTENGENEZA MWANAUME ANAYEMTAKA BAADA YA KUMPATA,NA SIYE KUWEKA VIGEZO VYA KUMPATA UNAYEMTAKA WEWE, NA JITAHIHI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI, NA INGIA KWENYE MITANDAO , NENDA KANISANI, NAAMINI UTAMPATA WEWE UNAVYOTAFUTA WAKO WANAUME NAO WANATAFUTA HIVYO HIVYO, MAANA ULAYA WENGIWAO WANA VIBIBI VINAWALEA WANATAMANI KUPATA MSICHANA KAMA WEWE, NAKUOMBEA KILA LA HERI, IKIWEZEKANA WEKA EMAIL YAKO TUWASILIANE, MIMI NI MSICHANA NA UMRI WAKO MTANZANIA. BYEE
Huku bongo siku hizi wanaume hawaoi mpaka wampe mwanamke mimba.... yaani leo ndoa kesho yake mtoto anazaliwa. Sasa haya mambo ya mara oohh one night stand, mara picha, mara skype yatakupeleka wapi sijui???? Ila kwa kua unataka wabeba box, all the best.
ReplyDeleteKwa taarifa yako:
ReplyDeleteMashariti yako ni magumu na yanasababisha ndio maana umechukua muda mrefu hivi kumpata mtu huko Ulaya!.
SHARITI LA:
''MWANAUME ANAYEISHI ULAYA LAKINI ANATOKEA TANZANIA''
ELEWA KUWA WATU WAPO KIMASLAHI NA IDADI KUBWA YA WATU WA ULAYA KWA ULAYA HAWAOWANI KAMWE !
KWANZA WANAONANA KINYAA !
MARA NYINGI NIMEONA INAWEZEKANA KAMA UNGEBADILI LOCATION KABISA KAMA UPO ULAYA FIKIRIA MUME WA NYUMBANI TANZANIA AU MAREKANI AU NJE KWINGINEKO !
IDADI KUBWA YA WANAUME WA KITANZANIA HUKO ULAYA NA NJE AU WENYE ASILI YA KITANZANIA SIO WAOAJI WENGI NI MA 'PLAYBOYS' LICHA YA KUWA WENGINE WANA UMRI MKUBWA WANAKUWA (MAKACHALA) HAWAJATULIA NA HAWAAMINIKI KABISA !
WENGI WANAUME WA HUKO MAJUU WANATAKA WANAWAKE KIMASLAHI ILI WAPATE NAFUU YA MAISHA KWA MWANAMKE MWENYE KIPATO UA NAFASI, AU WAPATE MAKARATASI, NDIO MAANA USISHANGAE MWANAUME WA MIAKA 30 AKAOA MWANAMKE WA MIAKA 65 LAKINI KWA AJILI YA KUPATA MAKARATASI.
MFANO NIGERIA (HATA WAKRISTO-KAMA MZEE ZUMA WA AFRIKA YA KUSINI) WANAKUWA NA WAKE ZAIDI YA MMOJA UNAKUTA MNIGERIA ANA MKE KWA AJILI YA MAKARATASI ULAYA NA ANAKUWA NA WAKE (WENGINE KADHAA)MARA NYINGI KWA SIRI KWAO NIGERIA-AFRIKA !
DADA UNAONA HII?
Chediel??????Huyu dada nahisi anaweza akawa anaishi Denmark, may be I know this lady!!!! Kama ni yeye mh!
ReplyDelete