Salaam kaka Michuzi,
Naomba unisaidie kutundili hili Bloguni,Maana nina rafiki yangu huwa twawasiliana, anaishi UK. So ametuma parcel kwa kutumia Capacity Cargo Delivery.
Na akanitumia receipt na tracking number. Nimekuwa nikitruck na kuona kuwa hiyo percel imeshakuwa cleared UK ila itapitia Spain, Malaysia then Tanzania. Inaonyesha kama hivi:
25-05-2012 | 11:30 | United Kingdom | Cleared |
26-05-2012 | 3:20 | Spain | Awaiting Arrival |
28-05-2012 | 10:05 | Malaysia | Awaiting Arrival |
29-05-2012 | 1:45 | Tanzania | Awaiting Arrival |
Sasa kama mnavoona hilo jedwari hapo, halionyeshi so far kama iyo parcel inatembea. Naomba mnisaidie kujua yafuatayo hasa mnaoishi UK
Je hii www.ccdelivery.org ni genuine website? Na Capacity Cargo Delivery ni genuine na reliable company?
Maana nimepigiwa simu toka Malaysia kuwa nitume some amount of money kupokea hiyo parcel ambayo ilishalipiwa malipo ya kutuma toka UK.
Wasiwasi wangu ni kwanini malipo yaende tena kwa western union wakati kama ni clearance fee basi ikiwa hapa bongo imeshafika naweza tu kwenda na kulipa na kuchukua kama ambavyo nikipokea percel kwa DHL ninavyofanya.
Na email walonitumia inaonyesha code number ambayo nimewahi kuiona mtu ana complain kuwa Malaysia wameshikilia parcel yake na akawa anauliza whether alipe au asilipe mana nae alikuwa ana wasiwasi. Nami nashindwa kumuuliza alienitumia maana kasafiri.
Naomba msaada kwa waliowahi pitia Capacity Cargo Delivery na kama huo ndo utaratibu maana hata mie ni mara ya kwanza kutumiwa kupitia hiyo. Nahitaji msaada wenu kabla sijafanya maamuzi.
Asante sana
Ni mimi dada yenu
Angela
DADA ANGELA POLE SANA HIYO NI KANYA BOYA WENZIO WALIFIKA AIRPORT KUSUBIRIA MTU ALIYEMTUMIA PARCEL MPAKA ALIPOGUNDUA NA KUONDOKA BE MAKINI MDAU SOPHIA WA MSASNI.
ReplyDeletekuwa makini dada mara nyingi hao ni matapeli wasiliana vema na huyo nduguyo kama kweli ametuma hiyo parcel kama ulipata ujumbe kwa mail inawezekana wajanja wamehack email addres yake na kuitumia please kuwa mwangalifu katika mambo kama hayo wengi wamelizwa mpendwa
ReplyDeleteHabari yako dada, hao ni matapeli ndo huwa wanajifanya hivyo na ukituma hizo walizokuambia utaambiwa utume zingine tena na walivyo washenzi hawataki utume kwenye jina la kampuni hapana wanataka ulipe kwa jina la mtu wanakutajia tena njia ndo hiiyo western union....
ReplyDeletehuyo alikutumia toka UK anatakiwa aende ofc za hao akawasiliane nao coz walimpa muda wa parcel kufika na sababu atakuwa na risiti. anaweza dai arudishiwe parcel na hela au wakikataa ana haki ya kuwashitaki fairtrade n they will be in shit. thas the only way ila hela usitume hata senti coz its a scam!!
ReplyDeleteNi kweli una rafiki yako anaeishi UK? Rafiki wa kwenye mitandao au rafiki unaye mjua au mmeshakutana ana kwa ana. Maana usikute umedanganywa na matapeli ya kinaigeria kwenye mtandao. Mtu akisha kutumia parcel hamna malipo yeyote unayotakiwa kulipia kabla mzigo haujakufikia. Kuwa makini hapo huenda unatapeliwa.
ReplyDeleteAngalia sana ndungu yangu hapa UK pamejaa Wapopo(Nigerians) Wana makampuni mengi kweli fake ya Kudeliver parcel, wengi wao Wahuni. Wee google kuchek kama ni Scam Companies. Ngoja nianze kukupa Pole
ReplyDeleteDada, kwa hesabu za haraka haraka, hapo ni utapeli mtupu. Ushauri - hakuna cha parcel wala nini na ukituma hela umeliwa!
ReplyDeletePole sana Angela.
ReplyDeleteMuhimu hapo ni kuwapigia Capacity Cargo Delivery hapa UK or Main Office na kuwauliza.Endapo umetumiwa mzigo from UK to Tanzania basi freight charge must be from Uk to Tz.Hizo transit hazikuhusu kabsa,wangepitishia Germany,Kenya then Tanzania is up to wao.So just phone them in main Office wape jina la mtumaji na Ref namba ya parcel.Malsiya waizi hapo,wasije kuwa Wapopo(Nigeria )wame truck parcel hiyo.
in my experience anybody asking for money via western union is a scam artist. yaani msaani. dont send money and wait till you can contact your friend and ask him what is really going on.
ReplyDeleteDada, kwa hesabu za haraka haraka, hapo ni utapeli mtupu. Ushauri - hakuna cha parcel wala nini na ukituma hela umeliwa!
ReplyDeleteMimi nipo London hizo company ulizotaja sio zakuaminika naona kama kunamchezo hapo kama nikulipia ingetakiwa mzigo ufike Tz ndo wakati unapoendakuupokea ndo ulipe something sio utume hela Malaysia,kua makini dada maisha yamekua magumu kila mahali hivyo watu wanatafuta njia yoyote yakupata hela hata kama sio halali.
ReplyDeleteNawakilisha.
Mdau london.
Tuwasiliane 0774350355
ReplyDeleteMay 0713225845 na mi yamenikuta hayo nipigie nikufahamishe, ni matapeli kwangu ilikuwa ultimateexpresscourier@asia.com
ReplyDeleteAsanteni sana jamani mana dah. Ila nsingetuma hadi niwe na uhakika. Ila nawashukuru wadau wa UK kwa ushirikiano na wengine wote.
ReplyDeletesi umwambie aliyekutumia afatilie huko alipopeleka mzigo na kulipia FULL STOP
ReplyDeletePlease visit this site for more complaints about capacity cargo delivery. Http://www.consumercomplaints.in/bycompany/capacity-cargo-delivery-a140924.html
ReplyDeleteChonde x99 Dada Yang don't send any penny - utalizwa asubuhix2
NINYI WA TANZANIA MIMI NAONA BADO MNA TONGO TONGO ZA USINGIZI WA 1942,HIVI KWELI WEWE UNAWEZA KUKUTANA NA MTU KWENYE NET ATI MPAKA UKAMPENDA NA AKUTUMIE PARCEL WEWE? YEYE HANA DADA HUKO KWAO HATA KAMA N I MZUNGU AU ANA KASORO AU NI MGONJWA WA UKIMWI ANATAFUTA WATANZANIA WANAWAKE NDIO WAJINGA DUNIANI KWA KUTAPELIWA ,KWA SABABU WANAWAJUENI KANA KWAMBA HAMNA ELIMU . HIO NI NIGERIA CONNECTIO KAMA HAMJUI HIVYO WANAWAKE WENGI WAISHA TAPELIWA NA HAO MA NIGERIA, SHAURI ZENU, NDIO MAANA MNAAMBIWA MBADILISHE SIASA SASA MAANA WENGI WENGI BADO MNAFIKIRI NYERERE BADO YUPO NA TANU AU CCM, ALISHAFARIKI CHAGUA CHADEMA CHAMA CHA KUPANUANA MAWAZO. ACHENI AKILI YA ABOUD JUMBE MJANJA WA UNGUJA MIAKA YA 1960 WAKATI HAKUNA TV ZANZIBAR AKATAPELI HUKO KAWAACHA WATU WAMELALA MPAKA LEO WANA FIKIRI UISLAM NDIO MAISHA, BADALA YA KUSOMA SHULE ZA KISASA WAO MPAKA LEO BADO WANANGANGANA NA MADRASS ETI KUMSOMA NABII WAKATI HATA KUTENGENEZA SINDANO HAWAJUI WALA KULIMA HATA TOMATO KWAO NI NGOMA.
ReplyDeleteBURE GHALI:
ReplyDeleteKwa nini aliekutumia mzigo asitumie huduma za Kampuni ya kueleweka kama DHL, USPS au FEDEX?
Tatizo mnabana sana matumizi matokeo yake mnapigwa sasa.
We uliendika na herufi kubwa hapo juu nahisi huna akili nzuri, zimekuruka. Hafu huwezi tofautisha issue moja na nyingine, pia huwezi fikiri kuwa kwa huyu dada kuomba msaada huu inasaidia na wengine kujifunza. Inaonyesha hata utumiaji wako wa keyboard ni wa kudonoa, ndo mana hata unasahau unataka kusema nini. Uwe unakaa kimya kama huezi kuongea sense. Nakushauri urudi darasani kujifunza consistence ya unachokiongea. Sio kila mtu lazima atoe maoni humu, naona wengine wanajifunza tu kuandika.
ReplyDeleteWewe uliyeandika in capital letters kama mngelikuwa mmeendelea na kusoma kila krismas mngelikwenda kunywa mbege na kila mkifa lazima mkazikwe migombani ndio mnaona maendeleo hayo. Kumkabili mungu na mini na mpasuo mpaka matakoni huko ni kuendelea na kusoma. Acha ujinga. Kama wewe unaona dini yako ni nzuri na anaeabudu miti na majabali nae pia anaona dini yake ndio ya kweli, vilevile kuna budha nae humwambii. Baniani hapeleki hekalu lake ambapo anajua hakuna waumini.
ReplyDeleteSantacy Delivery Company ndo ilikuwa yangu hao ni matapeli wa kinigeria kama ulikutana na huyo rafiki yako kwenye mtandao, na sikuwatumia hata senti tano na niliwaambia hizo hela sina na huo mzigo urudishwe kwa muhusika na wanavyojidai kukwambia kuna vitu vya thamani. Nigerian ni wezi wa mitandao hakuna mfano...
ReplyDeleteDunia ina wengi!!!
ReplyDeleteDada Angela anaonekana amenaswa na wapopo na bahati yake ameomba msaada tutani.
Wadau mbalimbali wamajaribu kumfumbua macho dada yetu pamoja nasi wadau wengine kuhusu usanii wa wapopo ulivyomahili.
Lakini jamani, wadau wengine, TANU, CHADEMA,UISLAMU,ABOUD JUMBE, MADRASS, Krismas, Kuabudu miti, mpasuo matakoni na mbege vina uhusiano gani na hii mada??!!