Mwenyekiti Kamati ya Michezo, Hospitali ya Taifa Muhmbili Dkt. Raymond Mwenesano
Baadhi ya wafanyakazi wakipasha kwa ajili ya mchuano mkali wa kesho kama walivyokutwa katika viwanja vya netiboli  karibu na hosteli ya wauguzi Muhimbili.


Kesho wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili watashiriki katika Bonanza la Michezo litakalo shindanisha Kurugenzi mbalimbali za Hospitali katika viwanja vya Posta vilivyopo Kijitonyama. Wataalamu hawa watashiriki katika michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete,kuvuta kamba na riadha kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo Dkt. Raymond Mwenesano alisema michezo itashirikisha timu kutoka kurugenzi za utumishi, uuguzi,fedha na mipango, upasuaji, huduma za tiba, tiba shirikishi. Katika michuano hiyo madaktari, wauguzi na watalaam wengine wa Hospitali wataonyeshana uwezo katika michezo ya nani mkali katika fani hii.

Alisema Muhimbili ina historia ya muda mrefu ya kushiriki katika michezo miaka ya 1990 ambapo Shirika la Afya Muhimbili lilikuwa linashiriki michezo kikamilifu ambapo timu ya mpira wa miguu na netiboli zilikuwa zikishiriki michezo ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma Tanzania (SHIMUTA). 

Aliongeza kuwa ushiriki wa timu hizi ulikuwa kwa kiwango kikubwa na wa hali ya juu kwani upinzani wa timu za Muhimbili na timu nyingine za mashirika ya umma ulikuwa mkali.  Katika kipindi cha Shirika la Afya Muhimbili, timu ya mpira wa miguu ya Hospitali iliwahi kuwa mshindi wa tatu na mara kadhaa ilikuwa ikifikia robo fainali katika michezo ya SHIMUTA, alisema. 

Sasa ni wakati muafaka tunataka kufufua michezo Muhimbili kwani inaongeza furaha, upendo miongoni mwa wafanyakazi na kujenga afya kutokana na kushiriki katika mazoezi, alisema Dkt. Mwenesano.

Aliongeza kuwa ushiriki katika michezo uongeza nidhamu kwani ili kushiriki michezo ni lazima ufuate sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa kwa mchezo husika, hivyo kujijengea nidhamu hata  demokrasia  kwani watu wote huonekana ni wamoja wakiwa katika timu, bila kujali cheo ama tofauti ya idara wanazofanyia kazi alifafanua Dkt. Mwenesano.

Alisema, Hospitali ya Taifa Muhimbili ina zaidi ya wafanyakazi 2700 hivyo ni vigumu wafanyakazi hawa kufahamiana kwani wanafanya kazi katika maeneo tofauti na muda tofauti ambapo wengine wanafanya kazi usiku wengine mchana. “Nina amini kuwa michezi hii itatufanya tufahamiane vizuri zaidi  hata kama tupo wengi kiasi hicho”, alisema Dkt.Mwenesano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2012

    It is shame to see unhealthy doctors.

    They dont observe weight and yet they advise us weight is fat and kills. That weight is a risk factor. Fatilicious!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2012

    Hawa ni wafanyakazi wa mambo ya afya, uuguzi, upasuaji, huduma za tiba, etc.. na pengine hufundisha mambo ya afya kwa binadamu halafu wote wanene na wanaonekana hawajali afya zao. Onyesheni mfano basi???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...