Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Wanawake katika Taasisi ya (WAMA),Tabu Likoko akifungua semina ya wanawake kutoka vikundi mbalimbali vya kuweka na kukopa vinavyosimamiwa na Taasisi ya (WAMA) kuhusu huduma za Mfuko wa Bima wa Afya NHIF iliyofanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya WAMA mapema leo asubuhi jijini Dar es salaam.Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF),Rehani Athumani,Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti,Michael Mhando na Mkurugenzi wa Uendeshaji,Eugen Mikongoti.
Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizungumza jinsi mfuko huo unavyosaidia jamii kupata matibabu wakati wa semina hiyo iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Taasisi ya WAMA jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF),Rehani Athumani na katikati ni Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai wa Mfuko na Utafiti,Michael Mhando.
 Afisa wa Masoko na Elimu kwa Umma (NHIF) Grace Michael akifuatilia mada katika semina hiyo, kushoto ni Afisa Uraghibishi na Mawasiliano Taasisi ya (WAMA),Philomena Marijani.
Mkurugenzi mifuko ya Afya ya Jamii (CHF),Rehani Athumani (aliesimama) akitoa mada mbalimbali juu ya huduma za mfuko wa bima ya Afya, huku washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza kwa makini.
 Washiriki wa semina hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyojadiliwa katika semina hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya (WAMA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2012

    Mipango kama hii inawafaa wale akina mama wa hukoooo Vijini kwenye mahitaji wa Bima ya afya kwa wanaojifungu chini ktk simenti na kwa msaada wa mwanga wa simu ya Nokia ya tochi !

    Hii sio mipango ya Wanawake wenye nafasi zao, NHIF muendeshe Semina hizi kwa wenye mahitaji zaidi !

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2012

    Ahhh Mjomba sema Viwanja vya Ikulu sio Viwanja wa Taasisi ya WAMA!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2012

    Bandugu hii Mipango ya NHIF ni ya kufikishwa zaidi kwa akina Mama wa kule Manyasini.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2012

    Mr Eugene na Mr Pius Mikongoti lazima watakuwa ndugu wamefanana sana nilisoma na Pius Mikongoti lakini sijui yuko wapi kama anasoma hii tuwasiliane 0754275610

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2012

    Hao akina mama wa matawi ya juu wenye nafasi zao ni kuwa 'TAYARI WAMEKUWA INSURED' ktk sehemu zao huko na hawana umuhimu na mahitaji kama haya ukilinganisha na wale wa huko Kijijini Mibuyu Saba Potwe Ndondondo kwenye kiza kilichotanda wasiokuwa na hata pa kushikia!

    Unakuta Mjamzito anawahishwa kwa kutumia usafiri wa baiskeli kwenda kujifungua njia ni ya gurudumu moja njia ya ng'ombe na mbuzi inayopita baiskeli tu na gari haipiti Km 30 umbali wa kuifikia Zahanati!

    Je kwa nini kipaumbele kisiwe huko Mibuyu Saba Potwe Ndondondo?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2012

    jamani nyie wote hapo juu. Kwanza tuwawezeshe hawa waliovaa bangili za dhahabu,halafu wananukia vizuri kwa parfume ya gift of zanzibar-kisha sasa tutawaangalia hao wa mibuyuni,wanaokoga bila sabuni. i think you know what i mean. Zebedayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...