Chama cha Wamiliki wa Vyombo Vya habari Tanzania, kwa kushirikiana na Taasisi ya Afrika inayojihusisha na mambo ya habari, AMI, kesho wanatarajia kuzindua Muongozo na Kanuni kwa wamiliki na mameneja wa vyombo vya habari nchini, katika hoteli ya Serena ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Pichani juu ni kamati ya Maandalizi, kutoka kushoto ni Mmjumbe wa Kamati Abdallah Mrisho, Mshauri wa Habari kutoka AMI Wangethi Mwangi, Mwenyekiti wa Kamati Theophil Makunga na Katibu wa Kamati, Henry Muhanika, wakati walipoongea na wanahabari leo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Ndugu Muhanika (katikati) akifungua mkutano huo.
Ndugu Wangeti (wa pili kulia), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kushoto kabisa ni Mjumbe wa Kamati, Steward Kasambala.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi Dk. Roukaya Kasenally (katikati) akiongea na wanahabari, kulia ni Ofisa Msaidizi kutoka AMI, Noreen Wambui.
sehemu ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo leo
Huu utakuwa muda mzuri wa kubadilishana mawazo na Rais Kikwete..Si mara moja nimemsikia rais analalamikia upotoshaji wa habari kutoka kwenye media.Juzi kwenye hotuba yake ya mei mosi bado aliongelea media kupotosha habari.Alisema,kwa hisia kali, namnukuu..."ukiwa kiongozi lazima uwe na ngozi nene".akiwa anaongelea vyombo vya habari vinavyopotosha habari
ReplyDeleteDavid V