Raisi mteule wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Duniani (AIWJ), Mheshimiwa Jaji Eusebia Munuo, (katikati) akisikiliza kwa makini wajumbe wengine wakichangia mada kwenye Mkutano huo, mara baada ya kukabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa Raisi wa Chama hicho.
Ujumbe wa Majaji na Mahakimu kutoka Tanzania, wakiwa kwenye picha ya pamoja, mara baada ya kukabidhiwa rasmi Bango la Chama hicho cha Majaji Duniani(AIWJ) na kupewa nafasi ya kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu ujao wa Chama hicho utakofanyika Mwezi Mei, 2014 Mjini Arusha – Tanzania.
Raisi Mteule wa Chama cha Majaji na Mahakimu, Mhe. Eusebia Munuo akikabidhiwa Bango na aliyekuwa Raisi wa Chama hicho, Lady Brenda M. Hale.
Sherehe, nderemo na vifijo katika Ukumbi wa Mikutano, mara baada Mheshimiwa Jaji Munuo kutangazwa rasmi kuwa Raisi mpya wa Chama hicho na Tanzania kukabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa Mwenyeji wa Mkutano ujao wa Chama hicho Mwaka 2014.

Chama cha Majaji Wanawake duniani (IAWJ) kilikuwa na mkutano wake Mkuu uliofanyika London Uingereza tarehe 2-5 Mei 2012.

Kwenye Mkutano huo Tanzania, iliwakilishwa na Majaji na Mahakimu ambao ni wanachama wa IAWJ (International Association of Women Judges) na Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (TAWJA).

Katika mkutano huo, viongozi mbalimbali walichaguliwa kushika nyadhifa kukiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka miwili.

Mhe. Jaji Eusebia Munuo, ambae pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania alichaguliwa kuwa Rais wa chama hicho.

Pamoja na kuchaguliwa ktk nafasi hiyo,Mheshimiwa Jaji Munuo, pia alikabidhiwa rasmi Bango la chama hicho. Kwa kukadhiwa Bango hilo, Tanzania sasa imekabidhiwa rasmi nafasi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano mkuu ujao wa chama hicho. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwezi Mei 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC Arusha Tanzania.

Ujumbe wa Tanzania uliokuwepo kwenye mkutano huo ulipokea wadhifa huo kwa shangwe na furaha kubwa kama inavyonekana kwenye picha.

Tanzania itashikilia nafasi hiyo ya Urais wa chama hicho mpaka mwaka 2014.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2012

    HONGERENI SANA, LAKINI HIZO SARE MIE HOMA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2012

    Hongera sana mama, Umekuwa mstari wa mbele siku zote katika kuchangia maendeleo ya kijijini kwako Uru-Moshi, Tulijua utafika mbali maana ni mnyenyekevu na umekuwa ukijishusha siku zote, Na hotuba zako zilionyesha ukomavu wako katika elimu na matumizi ya madaraka. Waonyeshe ukomavu wako huko duniani.SONGA MBELE MAMA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 10, 2012

    NAUNGA MKONO HOJA YA KUMPONGEZA MAMA YETU LAKINI NAMI NIMEONA KASORO KWENYE HIZO SARE KAMA ALIVYOSEMA MWENZANGU WA KWANZA. WANGETAFUTA MTU WA MAANA DESIGNER AKAWASHONEA KITU KIZURI CHA KUVUTIA.
    ANY WAY TUNACHOOMBA NI KAZI NZURI NA MUNGU AMBARIKI

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2012

    Yaani mimi ndiyo zimenifurahisha kweli kweli hizo sare. Hakuna cha designer wala nini mumeonyesha mfano mzuri wa kutumia kitu original - kanga za nyumbani.

    Hongereni saaaaaaana majaji

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2012

    Hongera sana mama. Kama mdau wa kwanza, sare jamani mweee.......

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 15, 2012

    Kweli uwe mwaminifu hata kufa nami nitakupa taji ya uzima. Hongera sana mama safari imekuwa ngumu na mabonde mengi lakini endelea kuwa mwaminifu Mungu anaendelea kukupigania!! Aluta Continue!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...