NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

WAZIRI wa Ujenzi,Dk. John Magufuli amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo kasi(DART) yenye urefu wa kilomita 21 na vituo vya mabasi 29 kutoka Kimara hadi Kivukoni iliyoko Jijini Dares Salaam kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha .

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Magufuli leo wakati alipotembelea miradi hiyo miwili ili kungalia shughuli za ujenzi ambapo alifurahishwa na kazi hizo huku akiwataka wamalize kwa muda unaotakiwa.

“Mkandarasi unatakiwa kufanya kazi usiku na mchana ili kazi ikamilike kabla ya wakati kampuni yenu ni kubwa kama kuna matatizo yoyote mtuambie sisi serikali ili tuweze kuyashughulikia,” alisema Waziri Magufuli.

Waziri Magufuli pia ametoa muda wa siku saba kwa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO) na Mamlaka ya (DAWASA) kuondoa miundombinu yao haraka ili kuepusha ucheleweshaji wa mradi wa DART.

Waziri wa Magufuli alitembelea ujenzi huo katika maeneo ya Jangwani na Ubungo, ambapo alisema itagaharimu sh. bilioni 240 na ikijumwuishwa na ujenzi mwingine wa vituo utagharimu jumla ya bilioni 288 ambazo zimetolewa na Serikali na Benki ya Dunia.

Awali Meneja wa mradi , Frank Rohde kutoka kampuni hiyo , alisema changamoto inayoukumba mradi huo ni ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi huo kutoka bandarini ambapo vimekaa kwa muda wa siku saba.

Akizungumzia kuhusu tatizo hilo Waziri Magufuli alisema atazungumza na Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato(TRA) ili vifaa hivyo vitolewe haraka.

Aidha Waziri Magufuli amemtaka Mkandarasi na Mshauri wa upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Tegeta kutoka kampuni ya Konoike ya Japan kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12 inayogharimu sh. bilioni 88 kwa muda unaotakiwa na kuacha kusingizio cha mvua kama wanavyodai kuwa umechelewa kwa asilimia saba.

“Mvua zilinyesha siku tatu haiwezi kuwa sababu kuna nchi mvua inayesha muda mrefu kuliko Tanzania na ujenzi wa barabara unaendelea. Sijaridhika na hiyo sababu ninyi nchi za nje mnaweza kujenga hata mvua ikiwa inayesha. Ni lazima wafidie muda … kuongeza kazi ya ujenzi hakutakuwa na ongezeko la muda wala mtaji,” alisisitiza.

Wakati huohuo Waziri Magufuli alitumia nafasi kuwataka wakazi wa Jiji hilo waliojenga katika maeneo ya hifadhi za barabara hizo kuondoka wenyewe kwa kuwa sharia ni msumeno.

“ Tukikuta mradi unakwamishwa sisi tutabomoa.

Akizungumzia kuhusu mradi DART , Afisa Mtendaji wa DART Cosmas Takule alisema utatengeneza ajira 80,000 na kusaidia abiria 406,000. Mradi huo utakamilika katika kipindi cha miezi 36.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam , Mwamtumu Mahiza alitka ajira hizo ziwe kwa vijana wa jiji hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2012

    Nimefurahi sana baada kuisoma habari hii,kwa rais JAKAYA KIKWETE najua sasa hivi unaumiza kichwa kupata baraza jipya la mawaziri,mimi nampigia upatu huyu mh Magufuli abaki hapohapo ili amalizie hii barabara na nyinginezo,huyu jamaa ni mtendaji mzuri nadhani hata wewe unaelewa hili,naomba kuwasilisha

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2012

    TUKISHA CHUKUA NCHI CHADEMA ,TUTAMPA KAZI MGUFULI POMBE.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2012

    mzee piga kazi mana ndio miongoni mwa wachache wanaofanya vitu vinaonekana. hao mawaziri na manaibu wenzio wengine hatakujulikana hawajulikani tangu wamechaguliwa hadi baraza litavunjwa.shame on them.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2012

    Mzaramo kasema kalagabaho na ndoto za alinacha. Fisi aiufuatilia mkono uanguke hata kakata tamaa Chadema haioni ndani ngo labda tumekufa.

    ReplyDelete
  5. mungu akubariki mh wizara zote ulizoshika kazi zako zinaonekana natamani tungekua na mawaziri hata 10 kama wewe.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2012

    Dr wa ukweli Magufuli Ungefaa kuuchukua u Pinda, tatizo sasa barabara zitalega lega! ila ufanisi serikalini utaongezeka! so JK chukua hii msg yangu uitekeleze

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2012

    Mwaka 2015 C.C.M Wakimuweka Magufuli Pombe kuwa Mgombea wao wa Urais, Watavunja nguvu zote za upinzani, maana anakubalika na wengi wakiwemo wapinzani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 03, 2012

    WAKATI MAGUFULI AKIFANYA KAZI, MAWAZIRI WENGINE WANAPANGA MIPANGO YA KUPATA 50% YAO. SIKU HIZI 10% HAITOSHI MAISHA YAMEPANDA, ANGALIENI BANDARINI MAGATI YANAWEZA KUJENGWA KWA $ 300 MIL. LAKINI WAZIRI ANATAKA KAMPUNI ITAKAYOJENGA KWA $ 530 MILIONI, WAKATI HUO MKUBWA WA PCCB BW. HOSEA AMELALA

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 03, 2012

    Duh !! Msukuma wangu, baba Magufuli, itaga milimo baba, achana na hao wezi wa mali ya umma, naomba ukimaliza barabara zote wakupeleke wizara ya madini, nafikiri na Tannesco iko chini ya wizara hii, ni chafu ina nuka, kule itakubidi ufunge kitambaa kwenye mapua yako,maana hizo harufu utakazozikuta huko,lazima utatapika tu. Kuna mhasibu mmoja huko makao makuu ya tannesco Ubungo,huyo nafikiri utamkuta kisha fungua hata benki yake mwenyewe, huyo siyo tu Fisadi ni jambazi, yaani anazichota pesa kama hakuna kesho. Cha ajabu ni msukuma mwenzio. Naona mulikwenda shule tofauti. Lakini Mungu yupo, kumbe siku za mwizi ni arobaini.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 03, 2012

    Huyu ana bahati na mungu aendelee kumbariki....ana bosi anayeona utendaji wake.. Jamni kuna mabosi hawataki kabisa kuona juniors wao wanafanya kazi vizuri wanakaa kufikiri watanyang'anywa vyeo... Nenda UCC mlimani mkaone. mtenda kazi yeyote huchikwa saaaaaana.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 03, 2012

    TUNAOMBA MWENYEZI MUNGU ANGALAU HILO BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LIWE NA WANAOFANANA NA MHE. MAGUFULI.

    SASA IMETOSHA TUMESHA KWAMA SANA KWA KUWA NA UTITIRI WA VIONGOZI WABOVU.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 03, 2012

    JEMBE LIKO KAZINI. SAFISANA.
    .Jamaa waliogopa kupiga mbizi, unadhani hawaogopi papa?

    Baba hata urahisi ukitaka utapata.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 03, 2012

    BABA TUWEKEE FERRY MBWENI/TEGETA HADI POSTA TUTAPANDA NA ITA PUNGUZA FOLENI. NAKUKUBALI JEMBE.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 03, 2012

    JK mpe uwazi mkuu. jamaa ni mtendaji hana siasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...