Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Bwana Peter J Mwenguo amefariki dunia tarehe jana Juni  18, 2012 saa nne asubuhi katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam, kwa mujibu wa taarifa za kifamilia.
 
Bwana Peter Mwenguo aliajiriwa na Bodi ya Utalii tarehe 22 0ktoba 1993 kama Mkurugenzi wa Masoko na kupandishwa cheo kuwa Mkurugenzi Mwedeshaji kuanzia tarehe 6 Februari, 1999 mpaka tarehe 22 Oktoba, 2008 alipostaafu kwa mujibu wa sheria na baadaye kufanya kazi kwa mkataba hadi tarehe 20 Desemba 2009. 
 
Bwana Peter. Mweguo amefanya kazi Bodi ya Utalii zaidi ya miaka 15.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake katika Magorofa ya TRA, Mwenge, Dar-es-Salaam. Taarifa kuhusu siku na mahali pa Mazishi zitatolewa baadaye.

Mungu ailaze roho ya marehemu  
Bwana Peter Mweguomahali pema peponi ! Amen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2012

    Du, nilimfahamu sana huyu mzee. Pia watoto wake akina Gilbert, Gaby, Joseph (bichwa) na Fumio. Alikuwa mzee mwenye busara sana, Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amina

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2012

    RIP Mzee Mwenguo, Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi, kwani yeye ndiye muweza wa kila kitu, na sote tu katika njia moja. Tutakukumbuka daima kwa ucheshi wako na heshima kwa kila mtu, jina la bwana lihimidiwe - Amen

    shark_ham@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2012

    SISI WADAU WA UTALII TULITHAMINI SANA MCHANGO WAKO MZEE WETU TULIKUPENDA LAKINI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI R.I.P

    www.kipepeotours.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...