Na Woinde Shizza,Arusha

IMEELEZWA  kuwa kiasi cha dola za Kimarekani Bilion 148 hupotea katika Afrika kila mwaka kutokana na kuwepo kwa mianya mingi ya rushwa  na badala yake fedha hizo zinapelekwa katika nchi za Ugaibuni hali ambayo inasababisha madhara makubwa sana kwa wananchi wan chi hizo.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Dkt Edward Hosea (pichani kulia) wakati akizungumza katika mkutano wa bodi ya ushauri wa masuala ya Rushwa kwa nchi za bara la Afrika mapema leo jijini hapa

Aidha dkt Hosea alisema kuwa kiwango hicho cha fedha hupotea kutokana na baadhi ya mianya ya Rushwa ambayo imo kwenye nchi hizo na badala yake fedha hizo zinapelekwa kwenye nchi za Ugaibuni

Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo ya upotevu wa fedha hizo unachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kukithiri kwa rushwa ndani ya Nchi hizo hali ambayo nayo inachangia hata maendeleo duni ya nchi hizo za bara la Afrika

“hiki ni kiwango kikubwa sana cha fedha ambazo zinapotea kusikojulikana lakini mpaka sasa tumeshaanza kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa nchi za bara la Afrika hazikumbwi na rushwa ingawaje pia changamoto ya kupambana nayo ni kubwa sana”Aliongeza Dkt Hosea.

Katika hatua nyingine alisema kuwa mpaka sasa kwa Upande wa Serikali ya Tanzania tayari imeshaanza miachakato mbalimbali ya kujenga bodi ya kupambana na Rushwa ambapo mchakato huo pia utasaidia sana kupunguza wimbi kubwa sana la Rushwa hapa nchini.

Dkt Hosea alisisitiza kuwa ujenzi wa jengo la bodi hiyo ya kupambana na rushwa utaaanza mara baada ya Kupitishwa kwa bajeti yake ambapo jengo hilo litajengwa ndani ya eneo la Kisongo mkoani Arusha

“kwa sasa tunafurai sana kwa kuwa ujenzi wa jengo hili umeshawekwa katika mikakati na kitu ambacho tunasubiri ni bajeti yake na tunachokiamini ni kuwa kupitia bodi hii tutaweza kuendelea kudhibiti mianya ya rushwa ndani ya Nchi za bara la Afrika”aliongeza Dkt Hosea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2012

    Mtafanya semina mpaka mwisho wa siku,halafu mutahukumu rushwa ndogo na za wakubwa zinaamuliwa kisiasa ama kuzimwa kabisa. kwani kikulacho kinguoni mwako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...